Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka

Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka

Kwa upeo wangu mdogo nadhani kilichofanyika ni kutaka kuiumbua serikali baada ya ile mikwara mbuzi ya Chura kiziwi.

Tigo hana kesi maana Mabeberu wako mbele ya Muda. Kampuni ya Millcom alishajiongeza muda akauza mtandao wa Tigo Kwa Rostam Aziz na huenda hata hawakumuuzia bali waliingia kati na Rostam wakasajili kampuni nyingine Rostam akakaa front kama mmiliki. Akili ni mia.

Ukienda mahakamani huwakuti.

Hao wapuuzi wako mbele ya muda.
Kwa hiyo waliuza kwa sababu ya hilo saga?
 
I know...

Kwamba wengi wa viongozi wa serikali hii pamoja na serikali yenyewe ina hisa ktk makampuni haya na hivyo na part of the owners of these telecommunication companies....

If that is the case, then it's obvious that wana wafanyakazi wao mapandikizi ambao sio waaminifu na hao ndiyo huvujisha information za wateja wanaotafutwa kuuwawa na wabaya wao....

Bila shaka hawa wafanyakazi waliopandikizwa na serikali au na baadhi ya hawa viongozi wa serikali "wasiojulikana" lakini ni watekaji na wauaji hawa ndio hu - disclose information za wateja targeted na wauaji bila ridhaa ya kampuni kwa ujumla wake....

Kama ndiyo hivi, basi ni jukumu la makampuni haya kuzi - secure information za wateja ktk namna ambayo ni ngumu na pengine isiwezekane kabisa kwa mtu mmoja au wawili kuzichokonoa na kuzigawa....

So, don't worry. I know that already....
The it is the responsibility and reliability of the company to employ unethical employee and to let the company easily manipulated.

Hapa hakuna kukwepa lawama Shekhe.

Kwa mtindo huu Tigo au Milcom wamechafuka kibiashara popote watakapo tia mguu duniani.
 
Kwa hiyo waliuza kwa sababu ya hilo saga?
Ndo maana yake walishaona mbele nini kinaweza kuwakuta.

Kumbuka kesi ipo London na Makao makuu ya Millcom/Tigo yapo London. Jiongeze.

Tukio la 2017 kesi ipo mahakaman toka 2019 na Millcom kamuuzia Rostam Tigo 2022
 
Mambo hayafanyiki kwa mihemko kama unavuodhani!
Kwa hiyo yafanyike hayo kisa Lisu alifanyiwa hiyo!
Who is Lisu mpaka tigo ifanyiwe hivyo?
Juzi hapa maandamano umeona kilichotokea?
Kwanini mlitaka kumuua?
Kwanini mlitumia policcm kuyadhibiti ?
 
Ulikua haujui hizi kampuni zipo kwa ajili ipi na zipo chini ya nani yaan mwenye mamlaka na kampuni zote ambae hata sasa akikuhitaji kwa kuzitumia hizo kampuni anakupata haumjui?

Rejea yule mzee wa Tanga aliedakwa kwenye gari na wale mabwana wakaondoka nae, tupo kwenye msiba wa mtumishi wa Halmashauri alieungua vibaya akiwa kwenye gari huko Tanga unganisha dots
Kama ni tushauriane ni mawasiliano yapi yatakuwa salama kwetu maana hatupo salama kwa namna hii ya tunaotumia mawasiliano yao kutuuza kwa watu wabaya.
 
Tuko nyuma sana kwa technology. Wametupita kwa kila kitu . Mzungu anatuchungulia mpaka ndani ya mapafu, acha vyumbani. Simu ni zao, satellite ni zao, hata savers ni zao, mimi siwabishii.
Asiyejua atakubishia
 
TIGO wameyatimba kwa mara nyingine
 

Attachments

  • 20240925_081628.jpg
    20240925_081628.jpg
    80.4 KB · Views: 3
Huyu Lissu sio mjinga,hii toka toka ya kwenda Ubelgiji uwa kuna vitu anafuatilia sio bure……….

Kuna nyakati Mungu,kwa makusudi kabisa anaruhusu mtesi wako akutese apendavyo Ila hawezi kuruhusu ufe,sio kwa sababu hakupendi la hasha!!! Ila anataka kupitia kwako ajidhihirishe ya kuwa hakuna mkubwa kuliko mwingine kwenye hii dunia………..rejea habari ya Ayubu na shetani,Daudi na Goliath,Mussa kwa farao NK.

Kupitia LISSU ndio tunapata ile dhana ya Mungu ndani ya mtu
Sahihi kabisa
 
Kama ni tushauriane ni mawasiliano yapi yatakuwa salama kwetu maana hatupo salama kwa namna hii ya tunaotumia mawasiliano yao kutuuza kwa watu wabaya.
Tupa laini tupa simu tumia njia ya barua kupitia kwa mtu kwenda kwa mtu ukiweza nenda mwenyewe ukamfuate usipige simu usitembee na simu haupo salama
 
Tigo Tanzania ilivujisha data za simu za Lissu kwa serikali ya Tanzania kabla hajapigwa risasi September 7, 2017. Mahakama ya Uingereza imeanza kusikiliza kesi.

Michael Clifford alikuwa mfanyakazi wa Tigo Tanzania ameiambia mahakama huko Uingereza kuwa aliachishwa kazi na kampuni ya Tigo Tanzania ambayo ipo chini ya Millicom kwa sababu alionyesha kutoridhishwa na Tigo kuvujisha taarifa za mawasiliaon ya Lissu.

Tigo ilivujisha mawasiliano ya Lissu na location yake kuanzia August 22, 2017. Tarehe 29 mwezi huo huo Tigo iliendelea kuvujisha location na mawasiliano ya Lissu kwa serikali muda wote (24/7) na kwa kasi hadi siku anashambuliwa Dodoma.

Clifford ni mpelelezi/ mchunguzi wa ndani wa mitandao ya mawasiliano wa Tigo.

Tigo haijakataa kubujisha mawasiliano na location ya Lissu kama ilivyo daiwa na Clifford.

Clifford alianza kufanya uchunguzi siku tano baada ya Lissu kushambuliwa, hii ni baada ya kusikia kwenye conference call kuwa Millicom illikuwa inatoa data za Lissu kwa serikali ya Tanzania bila idhini yake. Baadaye akakabidhi majibu ya uchunguzi kwa maboss wake.

Millicom ilikuwa inapeleka data za Lissu kupitia WhatsApp na baadaye kuwaambia wa-delete kila kitu kwenye WhatsApp.

So, Clifford anasema alifukuzwa kazi na Tigo kwa kuonewa kwa sababu ya kufichua mpango mbaya wa Tigo kuvujisha taarifa za Lissu kwa serikali ya Tanzania na kushambuliwa kwa Lissu.

Imechukua miaka minne hadi kesi hii kuanza kusikilizwa (trial) kwa sababu Kulikuwa na jitihada nyingi za kutaka isikilizwe sirini (restriction).
 
Sasa Tigo ni ya Rostam, huyo huyo anapambania favours kwenye makampuni yake mbele ya serikalii, hapo taarifa lazima zimwagike tu
 
Kwahiyo Clifford anatuambia kuwa kampuni ya TIGO ni kampuni ya KIGAIDI?

LISSU anaenda kuwa billionaire katika hii kesi.
 
Aibu kwao sasa.....tutende mema,ubaya unamwisho kufichika
 
Uzuri Mheshimiwa mwenyewe aliyenusurika kuuwawa alishawahi kuwataja wabaya wake kupitia mahojiano aliyofanyiwa na vyombo vya habari. Na kupitia huu ushahidi, ni wazi wahusika ni wale wale.
 
Back
Top Bottom