Boycott Tigo now.
Na kwa sasa tigo ni mali ya Rostam kwa 100% hakuna aliye salama anayetumia line ya tigo.
Issue siyo kuwasusa (boycot) huduma zao tu....
Hii kampuni kama ilivunja sera na sheria ya usiri wa kumlinda mteja na kushirikiana na baadhi ya viongozi wahuni na majambazi ya serikali ya Magufuli na CCM ktk tendo la mauaji ya kikatili (ugaidi) kwa Tundu Lissu, basi washitakiwe na kulipa fine kubwa itakayowafilisi moja kwa moja....
Mara nyingi tumeionya serikali na viongozi wake kuanzia Rais hadi chini kuwa HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA lakini kwa sababu ni wajinga, wapumbavu kwa sababu ya kulewa madaraka chakari, wakati wa kulipia ujinga na upumbavu wao umeshafika....
Serikali ilikuwa na fursa nzuri kufuata taratibu za kisheria kumtia hatiani Tundu Lissu kama kweli alikuwa na nyendo zilizokuwa zinahatarisha usalama wa nchi....
Lakini kwa ujinga na upumbavu wa John Pombe Magufuli na watu wake wakauvaa ushetani wa kuvunja sheria kwa kuchukua njia ya mkato ya kutaka kumuua huyu mwamba bila hata kujua kuwa jamaa ni immortal...
Na huu utekaji na mauaji yanayoendelea sasa hapa nchini yana sura hii hii na mtindo na style ni hii hii....
Haya Makampuni ya mawasiliano ya simu ususani Vodacom na Tigo ni washiriki wa unyama kwa namna ya kuwauza wateja wao kwa baadhi ya viongozi wa serikali ya CCM, majambazi na magaidi kinyume kabisa cha sheria ili wauwawe....
Hii haikubaliki hata kidogo.....
Kampuni za simu zinapaswa kujiweka kwenye safe side pale mamlaka fulani za kiserikali mf. Polisi, TISS au kiongozi yeyote limbukeni anapoitaka kampuni ku - disclose taarifa za mawasiliano ya mteja wao fulani, waambie wafuate utaratibu wa kisheria kwa kwenda mahakamani wamshitaki kwanza huyo mtu kisha mahakama ikiona kuna hoja itatoa kibali kwa kampuni ya mawasiliano ya simu ku - disclose information za mteja wao zinazotakiwa....
Lakini hii ya kutenda kijinga tu, hakika kuna siku kampuni fulani itafirisiwa na kufa kabisa kibiashara....!!
Tundu Lissu huu ni wakati wako wa kampuni ya Millicon//Tigo kukutajirisha sasa...!