Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka

Kupigwa risasi kwa Tundu Lissu: Kampuni ya simu ya Tigo yadaiwa ilivujisha mawasiliano yake kwa mamlaka

Katika mashauri yaliyosikika katika mahakama ya ajira ya London, Uingereza, imeibuka taarifa kwamba kampuni ya mawasiliano ya Tigo ilihusika katika kutoa taarifa za simu za mwanasiasa maarufu wa Tanzania, Tundu Lissu, kwa mamlaka za serikali kabla ya jaribio la mauaji dhidi yake mwaka 2017.

Taarifa hizo zinadai kuwa Tigo ilitoa taarifa za eneo na mawasiliano ya simu ya Lissu kwa serikali ya Tanzania kuanzia tarehe 22 Agosti 2017, wiki chache kabla ya shambulio hilo kutokea. Taarifa hizi zilifuatiliwa kwa saa 24 kila siku, hadi siku ya tukio.

Shambulio la Risasi Dhidi ya Tundu Lissu

Lissu, ambaye ni mwanasheria na mwanasiasa wa upinzani, alishambuliwa kwa risasi nyingi tarehe 7 Septemba 2017 nje ya makazi yake ya bunge mjini Dodoma. Alipigwa risasi akiwa kwenye gari lake na kujeruhiwa vibaya, lakini alinusurika kifo. Mpaka sasa, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na shambulio hilo.

Mfanyakazi wa Tigo Afutwa Kazi kwa Kuwasilisha Malalamiko

Katika kesi hiyo, Michael Clifford, afisa wa zamani wa Tigo na mpelelezi wa zamani wa polisi, alidai kuwa alifutwa kazi kwa sababu ya kufichua taarifa kuhusu mpango wa utoaji wa taarifa za simu za Lissu kwa serikali ya Tanzania. Clifford alidai kwamba baada ya kuhudhuria mkutano uliohusu utoaji wa taarifa hizo, alianzisha uchunguzi wa ndani na kugundua kwamba Tigo ilikuwa ikitoa taarifa za simu ya Lissu kwa serikali bila idhini yake.

Kwa mujibu wa Clifford, alifukuzwa kazi baada ya kupeleka malalamiko kwa viongozi wake kuhusu suala hilo, akieleza kwamba alihisi alikuwa akifanya hivyo kwa maslahi ya umma. Clifford aliongeza kuwa taarifa zilianza kutolewa mara tu Lissu alipoanza kushutumu serikali hadharani.

Athari za Kesi Hii

Kesi hii imeibua maswali makubwa kuhusu usalama wa taarifa binafsi za wananchi na jinsi zinavyoweza kutumiwa vibaya na makampuni ya mawasiliano kwa kushirikiana na serikali. Pia, inaleta changamoto za kisheria kuhusu haki za wafanyakazi wanaojaribu kufichua maovu yanayofanyika ndani ya taasisi walizozifanyia kazi.

Kwa sasa, bado hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi ya Tigo au watu waliotajwa kuhusika katika tukio hili, lakini kesi inaendelea kusikilizwa kwenye mahakama za Uingereza.
View attachment 3105596

Chanzo: The Guardian
Ingekuwa ni Tanzania Ile sheria ya usalama wa Taifa inayohusu kutunza Siri za Nchi tena kwa.kuapisha ingemtia huyo Afisa kifungoni kwa.miaka 20 achilia mbali kufutwa kazi.

Tanzania tuna sheria za hatari
 
Mbona Kabendera alifungulia Voda kesi ha kuvujisha Mawasiliano lakini wakaitupilia mbali?

..kabendera alishtaki Tanzania.

..pia Kabendera hakuwa ndani ya kampuni ya Voda.

Mazingira hayo yanaweza kuwa yalimkwamisha Kabendera asiwe na ushahidi wa kutosha dhidi ya Voda.

..anayetoa madai dhidi ya Tigo ni mtumishi wao ambaye anadai alihusika ktk suala hilo.
 
Lakini ni mazingira hayo hayo isipokuwa tuu amekosekana wa ndani kutoa ushahidi
 
Kwani ilikuwa siri, mbona yule roporopo aliyekuwepo (Magufuli) alikuwa anasema wazi tunadukua mawasiliano ya Lissu na kusikiliza jinsi anavyojaribu kufanya sabotage kwenye re-negotiations za madini na ACCACIA.

Pamoja na hayo Lissu akaonywa acha, aelewi somo; akipata muda kwenye media ni kuponda uongozi hoo dictator uchwara, akienda bungeni bado anapika sumu yake ya uongo ya kwenda kushitakiwa MIGA.

I mean it’s obvious Lissu has been compromised for a while, kwa nyakati zile na alichokuwa anafanya ni kujitakia tu.

If anything hii kesi inaonyesha Magufuli alikuwa mkweli alipokuwa anasema kutwa Lissu anapogia simu wafanyakazi wa ACCACIA na tume ya madini kutafuta umbea na coaching ili kuiangamiza serikali.

Wafuasi wa CDM mitandaoni ni shida wapo tayari kutetea viongozi wao kwa lolote bila ya kujali national interest.
 
..Wazungu / Mabeberu wanaabudu mahakama na sheria, kuliko wanavyoabudu MUNGU.

..kuna jasusi wa FBI Marekani alijitoa mhanga kumchoma Rais Richard Nixon ktk kashfa ya udukuzi wa campaign HQ za chama cha Democrats.

..kashfa hiyo ilijulikana kama Watergate Scandal. Jasusi wa FBI alikuwa anatoa siri za uhalifu uliofanywa na timu ya kampeni ya Rais Richard Nixon wa Republican kwa waandishi wawili wa habari.

..ukifanya uhalifu na mabeberu suala likifika MAHAKAMANI lazima watakiri kila mlilofanya.
 
Kwani ilikuwa siri, mbona yule roporopo aliyekuwepo (Magufuli) alikuwa anasema wazi tunadukua mawasiliano ya Lissu na kusikiliza jinsi anavyojaribu kufanya sabotage kwenye re-negotiations za madini na ACCACIA.

Pamoja na hayo Lissu akaonywa acha, aelewi somo; akipata muda kwenye media ni kuponda uongozi hoo dictator uchwara, akienda bungeni bado anapika sumu yake ya uongo ya kwenda kushitakiwa MIGA.

I mean it’s obvious Lissu has been compromised for a while, kwa nyakati zile na alichokuwa anafanya ni kujitakia tu.

If anything hii kesi inaonyesha Magufuli alikuwa mkweli alipokuwa anasema kutwa Lissu anapogia simu wafanyakazi wa ACCACIA na tume ya madini kutafuta umbea na coaching ili kuiangamiza serikali.

Wafuasi wa CDM mitandaoni ni shida wapo tayari kutetea viongozi wao kwa lolote bila ya kujali national interest.

..Ilitakiwa apelekwe MAHAKAMANI.

..mbona Nyerere aliwafikisha mahakamani wanajeshi waliopanga kumpindua na kumuua?

..kwanini Magufuli aliamua kumuua Lissu? Yeye angempeleka mahakamani, halafu akasubiri kusaini hukumu ya kifo kama angepelekewa.

..pia suala la Acacia / Barrick imegundulika kwamba Lissu alikuwa mkweli, na Magufuli muongo.

..kwa kifupi Magufuli aliamua kumuua Lissu ili uwanja uwe wazi kuwalaghai wananchi kwamba anatetea rasilimali.
 
Lakini ni mazingira hayo hayo isipokuwa tuu amekosekana wa ndani kutoa ushahidi

..Kabendera alipaswa kuwa na mtu wa ndani ya Voda, au Tiss, ambaye yuko tayari kuwachoma wenzake.

..Pia huwezi jua kama Kabendera hawezi kushtaki nje ya nchi na ikatoka hukumu itakayompa ushindi.

..Kwenye nchi za mabeberu kuna sheria zinazoyakataza makampuni yao kujihusisha na mambo fulani fulani, hata yanapofanya kazi nje ya nchi zao.

..Makampuni ya mabeberu hawaruhusiwi kujihusisha na rushwa ktk mataifa ya nje. Kwa mfano, kampuni kama Boeing ikijulikana kwamba imejihusisha na rushwa hapa Tanzania inaweza kushtakiwa ktk mahakama za Marekani na kuingia ktk matatizo makubwa. Ni mfano tu.
 
..Ilitakiwa apelekwe MAHAKAMANI.

..mbona Nyerere aliwafikisha mahakamani wanajeshi waliopanga kumuua na kumpindua?

..kwanini Magufuli aliamua kumuua Lissu? Yeye angempeleka mahakamani, halafu akasubiri kusaini hakumu ya kifo kama angepelekewa.

..pia suala la Acacia / Barrick imegundulika kwamba Lissu alikuwa mkweli, na Magufuli muongo.
Wafuasi wa CDM hata siku viongozi wenu wakitoa bunduki hadharani na kuuwa, mbele ya umati. Mtasemq nyinyi ndio mliiona vizuri ilikuwa bahati mbaya tu jua lilikuwa usoni kwake akuona kashika nini kabla ya kufyatua.

Ni kama sakata la Mnyika mtu anaitwa kwa mahojiano na polisi wito ambao uwezi kukataa kisheria, ataki kwenda. Mkitoka hapo ohoo Mnyika asiende kuwasaidia polisi kwenye mahojiano. Halafu akikamtwa anaonewa.

Sitogusia ya nani sahihi kwenye mambo ya mikataba kwa sababu najua Lissu hajui na wewe ndio kabisa, so huko tutakuwa tunapoteza muda tu.

Acheni hii mambo ya blind support, if it’s wrong it’s wrong. Msipende kutetea makosa ya wazi ya viongozi wenu.
 
Katika mashauri yaliyosikilizwa katika Mahakama ya ajira ya London, Uingereza, imeibuka taarifa kwamba kampuni ya mawasiliano ya Tigo ilihusika katika kutoa taarifa za simu za mwanasiasa maarufu wa Tanzania, Tundu Lissu, kwa mamlaka za serikali kabla ya jaribio la mauaji dhidi yake mwaka 2017.

Taarifa hizo zinadai kuwa Tigo ilitoa taarifa za eneo na mawasiliano ya simu ya Lissu kwa serikali ya Tanzania kuanzia tarehe 22 Agosti 2017, wiki chache kabla ya shambulio hilo kutokea. Taarifa hizi zilifuatiliwa kwa saa 24 kila siku, hadi siku ya tukio.

Shambulio la Risasi Dhidi ya Tundu Lissu

Lissu, ambaye ni mwanasheria na mwanasiasa wa upinzani, alishambuliwa kwa risasi 36 tarehe 7 Septemba 2017 nje ya makazi yake ya bunge mjini Dodoma. Alipigwa risasi akiwa kwenye gari lake na kujeruhiwa vibaya, lakini alinusurika kifo. Mpaka sasa, hakuna aliyekamatwa kuhusiana na shambulio hilo.

Mfanyakazi wa Tigo Afutwa Kazi kwa Kuwasilisha Malalamiko

Katika kesi hiyo, Michael Clifford, afisa wa zamani wa Tigo na mpelelezi wa zamani wa polisi, alidai kuwa alifutwa kazi kwa sababu ya kufichua taarifa kuhusu mpango wa utoaji wa taarifa za simu za Lissu kwa serikali ya Tanzania.

Clifford alidai kwamba baada ya kuhudhuria mkutano uliohusu utoaji wa taarifa hizo, alianzisha uchunguzi wa ndani na kugundua kwamba Tigo ilikuwa ikitoa taarifa za simu ya Lissu kwa serikali bila idhini yake.

Firm disclosed phone data of shot Tanzanian politician, UK tribunal hears

Tigo's former investigator claims he was unfairly dismissed for raising concerns over 2017 attack on Tundu Lissu

David Pegg
Tue 24 Sep 2024 15.58 BST

Gunmen tried to assassinate a Tanzanian opposition politician after a telecoms company secretly passed his mobile phone data to the government, according to evidence heard in a London tribunal.

The mobile phone company Tigo provided 24/7 phone call and location data belonging to Tundu Lissu to Tanzanian authorities in the weeks before the attempt on his life in September 2017.

The arrangement, which Tigo does not deny, was revealed in a claim by a former internal investigator for the company that was heard at the Central London employment tribunal this month.

Michael Clifford, a former Metropolitan police officer, claims that Millicom, the owner of the Tigo brand, sacked him for raising concerns about the affair.

“Mr Clifford’s case is that he was treated to his detriment, frozen out by [Millicom] and automatically unfairly dismissed because he made protected disclosures, or ‘blew the whistle’, in respect of matters of the utmost seriousness and public interest importance,” Clifford’s lawyers said in written submissions.

Lissu was attacked in his car in the parking bay of his parliamentary residence in Dodoma on 7 September 2017. The car was sprayed with bullets and he received severe injuries. Nobody has been prosecuted for his attempted murder.

Five days later, Clifford began investigating after hearing on a conference call that Millicom had been providing Lissu’s mobile phone data to the Tanzanian government. He later handed a summary of his findings to his superiors, his lawyers said.

The report concluded that “information had been provided to the Tanzanian government since 22 August 2017”, the lawyers said. “From 29 August 2017, the intensity of the tracking increased and [Millicom] used its human and electronic resources to live-track 24/7 the location of two of Mr Lissu’s mobile phones.”

The data was passed to the government via WhatsApp messages, which Millicom was later asked to delete. No formal legal request for the data appeared to have been filed.

“In the claimant’s reasonable belief, this information tended to show that [Millicom] was involved in an attempted political assassination and an act of terrorism,” Clifford’s lawyers said.

Get in touch
Do you have information about this story? Email david.pegg@theguardian.com, or (using a non-work phone) use Signal or WhatsApp to message +44 772 8715874. For the most secure communications, use SecureDrop or see our guide.

Clifford claims that after escalating his concerns, his relationship with his managers began to break down and they began to marginalise him within the company, before making him redundant in the autumn of 2019. Millicom disputes Clifford’s claim.

The company provides telecoms services to emerging markets in Latin America and also operated in parts of Africa during the period Clifford was employed. Its position is that at the time Clifford was dismissed, it was in the process of winding down a substantial proportion of its activities in Africa.

Tanzania remains a dangerous country in which to be a member of the political opposition, despite a change of president in 2021. On Monday, police arrested Lissu and at least a dozen others before planned protests against killings and the

Chanzo. The Guardian UKView attachment 3105588
Mambo yanazisidi Kusanuka.
 
Wafuasi wa CDM hata siku viongozi wenu wakitoa bunduki hadharani na kuuwa, mbele ya umati. Mtasemq nyinyi ndio mliiona vizuri ilikuwa bahati mbaya tu jua lilikuwa usoni kwake akuona kashika nini kabla ya kufyatua.

Ni kama sakata la Mnyika mtu anaitwa kwa mahojiano na polisi wito ambao uwezi kukataa kisheria, ataki kwenda. Mkitoka hapo ohoo Mnyika asiende kuwasaidia polisi kwenye mahojiano. Halafu akikamtwa anaonewa.

Sitogusia ya nani sahihi kwenye mambo ya mikataba kwa sababu najua Lissu hajui na wewe ndio kabisa, so huko tutakuwa tunapoteza muda tu.

Acheni hii mambo ya blind support, if it’s wrong it’s wrong. Msipende kutetea makosa ya wazi ya viongozi wenu.
Tanzania remains a dangerous country in which to be a member of the political opposition, despite a change of president in 2021.
 
Tanzania remains a dangerous country in which to be a member of the political opposition, despite a change of president in 2021.
Hiyo habari aiwezi kuwa kwenye TV media, aiwezi kuwa front page ya guardian.

Ni one sided (bias) hakuna upande wa TiGO the objective of the article is clear it’s a sponsored yenye lengo la kuichafua nchi.
 
..kabendera alishtaki Tanzania.

..pia Kabendera hakuwa ndani ya kampuni ya Voda.

Mazingira hayo yanaweza kuwa yalimkwamisha Kabendera asiwe na ushahidi wa kutosha dhidi ya Voda.

..anayetoa madai dhidi ya Tigo ni mtumishi wao ambaye anadai alihusika ktk suala hilo.
Huyo mtumishi alihusika kwenye uchunguzi wa jambo hilo, na alifanya kazi yake ukweli kweli ... kumbe kuna ambao hawakutaka ukweli kweli
 
Back
Top Bottom