Ndugu zangu,
Mimi naamini, kuwa Mfumo wa Serikali Tatu hautavunja Muungano, yumkini utauimarisha. Kama kweli tuna dhamira ya dhati ya kutoka kwenye tope la kero za Muungano tulilonasa, basi, Serikali Tatu haziepukiki.
Juzi hapa Profesa Issa Shivji, mbali ya mambo mengine yaliyomo kwenye rasimu ya Katiba, ameonyesha wasiwasi wake kuwa Serikali Tatu zitapelekea kuuvunja Muungano.
Naheshimu sana mawazo ya Profesa Shivji, lakini, katika hili la Serikali Tatu nahofia ametanguliza hofu isiyo lazima.
Uhalisia tulio nao sasa ni kuwa hali ya Muungano wetu inadhohofika kila kukicha. Wengi walio upande wa visiwani wanataka mamlaka kamili ya kidola. Na sauti za wabara wenye kuhoji muungano zinaongezeka kila kukicha. Hivyo, kero za Muungano zingalipo na zitaongezeka. Ili walau tuwe na nafasi ya kuunusuru Muungano, mimi naikubali kwa dhati kabisa ' Njia ya Jaji Warioba'.
Naamini pia, kuwa Serikali Tatu zinaweza pia kupelekea wananchi wa nchi husika kufanya kazi zaidi kwa ajili ya nchi zao. Hivyo basi, kuongeza zaidi bidii ya kuzalisha na kugharamia Serikali ya Muungano bila matatizo makubwa. Serikali Tatu zitaongeza pia hali ya kujitambua na kuheshimiana kama ndugu. Demokrasia ina gharama. Hivyo basi, hatuwezi kuchagua mfumo dhaifu kwa kuogopa gharama za demokrasia.
Na Mwanadiplomasia mahiri wa Kitanzania alipata kuliweka hili vizuri kabisa. Ni Balozi Augustine Mahiga. Alisema, kuwa ingawa Serikali Tatu zina gharama zake, lakini, kisiasa ina manufaa yake kutokana na mijadala ya muda mrefu kuhusiana na muundo wa Muungano.
Balozi Mahiga anazidi kunukuliwa akisema, kuwa iwapo Rasimu hiyo itapitishwa na Watanzania, ni wazi kwamba Tanzania itakuwa imerekebisha kasoro za Muungano unaotimiza miaka 50 mwakani, kwa njia ya mazungumzo. ( Mwananchi, Jumapili, Juni 9, 2013, Uk 2)
Ndugu zangu,
MUUNGANO wa nchi MBILI unapaswa uzae nchi MOJA. Hivyo, Serikali MOJA pia. Tanzania ni muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hata hivyo, Zanzibar kuna Serikali ya Mapinduzi tangu mwaka 1964. Tanganyika hakuna, na jina pia halitumiki.
Tuukubali ukweli, kuwa katika kilichoanishwa hapo juu, ni vigumu kuzungumzia Muungano wa Serikali MBILI badala ya MOJA au TATU.
Naam, umefika wakati wa kuukubali ukweli, kuwa kwa muundo huu wa Muungano tulio nao sasa, siku zote kutakuwa na manung'uniko. Kuukataa ukweli huu ni sawa na kufagilia takataka chini ya jamvi. Iko siku jamvi lazima liinuliwe, na uchafu huo utaonekana tu.
Maggid Mjengwa,
Iringa.
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio