Kupinga Serikali Tatu; Natofautiana Na Profesa Issa Shivji...

Kupinga Serikali Tatu; Natofautiana Na Profesa Issa Shivji...

Suluhisho la uhai wa huo unaoitwa ETI Muungano basi ni Serikali 3 au na iwe basi nalitote tugawane mbao
 
poleni wanafunzi wa prof shivji...Mimi ningeweza kumuona ningemuuliza jumuiya ya ulaya imeungana au haijaungana...?
 
maggid,

..wa-Znz wanaposema wanataka mamlaka kamili, wanamaanisha wanataka mamlaka kamili, siyo "mamlaka kamili."

..ndiyo maana wengine tangu zamani sana tulisema kwamba serikali 3 hazitakidhi madai ya wa-Znz wa leo.

..njia sahihi ya kujibu madai ya wa-Znz ni kukubali muungano huu uvunjike, na tushirikiane kupitia EAC.

..pia ili kuepusha uhasama na usumbufu, wa-Znz wote walioko Tanganyika wapewe status ya ukaazi wa kudumu mpaka watakapoamua uraia wanaoutaka.

cc: GHIBUU, takashi, Nguruvi3, Nonda, Kibunango, Kobello
 
Last edited by a moderator:
Maggid, nadhani utasikia rai yangu ya wewe kushiriki mijadala na si 'kutupa' kitu na kukimbia.

Kuna utata sana wa serikali 3. Aliyekuwa rais wa znz Aboud Jumbe alijiuzulu kwa sakata hilo.
Wznz waksema ameonewa.

G55 ilikuja na pendekezo hilo kama ilivyokuwa kwa tume ya Nyalali, Kisanga na Warioba(tume ya kwanza).CUF kina sera ya serikali 3. Profesa Shivji amekaririwa mara nyingi akitaka serikali 3.

Inashangaza wale waliokubali serikali 3 ndio hao hao wanaoonyesha mashaka nayo akiwemo Prof Shivji.

Prof Shivji ni mzanzibar na ametoa elimu ya znz katika muungano. Kama raia au msomi anayo haki ya kujiunga na taasisi kama maridhiano au Uamsho bila tatizo au kujificha.

Kisichopendeza ni kujificha nyuma ya uprofesa ili kuendeleza ajenda za akina Uamsho .
Hapa natofautiana naye sana na nabaki kumuheshimu sana.

Ukisoma mapendekezo yake, anasema mambo ya nje na uraia yasiwe ya muungano kama wanavyodai wale wa mkataba wa muungano.

Prof anashangaa kwanini Polisi lisiwe jambo la muungano wakati huo huo akitaka znz huru kama walivyo akina Maalim na Jussa.

Ukiondoa Uraia na uhamiaji hakuna serikali ya shirikisho. Rais wa shririkisho hawezi kuwepo kama hakuna raia na hapo Prof Shivji anaunga mkono hoja ya kuvunja muungano kiufundi.

Profesa anasema mapendekezo yaliyopo yatampa rais wa Tanganyika nguvu kubwa kwasababu ana eneo kubwa.Prof haelezi nguvu ya kiuchumi itakayotokana na mchango wa Tanganyika katika serikali kuu.
Kwamba kuwe na usawa hilo haliwezekani isipokuwa kama znz itakuwa na mchango sawa na Tanganyika.
''with great power comes responsibility''

Prof anasema wznz wengi wanataka mamalaka kamili. Juzi tu kulikuwa na kikao cha kamati ya kushughulikia kero za muungano chini ya Gharibu Bilal na Makamu wa pili wa rais Idd Seif alisema kuna.Ingawa sikubaliani na kamati hizi lakini kuna kitu kinachoonekana hapo.

Kinachoonekana ni kuwa wanaotaka mamlaka kamili ni wapemba ambao nadhani Prof Shivji ana sympathize nao kwa kusema ni wengi.
Lau isingekuwa hivyo akina Gharib na Idd Seif wangeungana na akina Jussa na Maalim kutaka mamlaka kamili.

Hofu ya profesa ni kuvunjika kwa muungano. Hapa amejificha tu katika usomi lakini ukweli ni kuwa hasimamii muungano.Znz imevunja katiba ya muungano mara zaidi ya 10, profesa hakuwahi kuonya kuwa kuna hatari ya kuvunja muungano.

Leo ujio wa Tanganyika anaona hatari hiyo! Ukimsoma vizuri profesa, anaunga hoja ya muungano wa mkataba lakini nafsi inamsuta

Ndugu yangu Kobelo, federation haiwezekani kwasababu znz inataka iwe znz kwa maana kuwa haitaki kutoa kuwa sehemu ya federation. Haikubali kupoteza utambulisho kama ilivyofanya Tanganyika.

Na mwisho wale wanaosema hawataki muungano wa serikali 3 inabidi waende mbali na kusema wanataka ipi?Wakisema mbili, je watawatendea haki Watanganyika.Wakisema moja je znz wapo tayari kutoa sehemu ya uhuru na mamlaka yao?

cc.JokaKuu, Jasusi, Mwanakjiji, Kichuguu, Mchambuzi
 
maggid,

..wa-Znz wanaposema wanataka mamlaka kamili, wanamaanisha wanataka mamlaka kamili, siyo "mamlaka kamili."

..ndiyo maana wengine tangu zamani sana tulisema kwamba serikali 3 hazitakidhi madai ya wa-Znz wa leo.

..njia sahihi ya kujibu madai ya wa-Znz ni kukubali muungano huu uvunjike, na tushirikiane kupitia EAC.

..pia ili kuepusha uhasama na usumbufu, wa-Znz wote walioko Tanganyika wapewe status ya ukaazi wa kudumu mpaka watakapoamua uraia wanaoutaka.

cc: GHIBUU, takashi, Nguruvi3, Nonda, Kibunango, Kobello
Nakubaliana na wewe.
Nguruvi3, nakuelewa vizuri sana unaposema Zanzibar hawapo tayari au hawataridhia kuwepo kwa Federation. Hii ndiyo njia nzuri ya kuwa na serikali tatu, au kuwe na majimbo (kama CDM wanavyopendekeza) kitu ambacho sidhani kama wazanzibari watakikubali. Binafsi sikubaliani na majimbo.

Watanganyika hatujali tena, hasa kizazi hiki. Na hatuogopi wala hatuna soni tukiwa tunawataka wazanzibari wakubali uwepo wa Tanganyika kama dola ya kipekee au shirikishi. Na kwa vyovyote vile, ni lazima Tanganyika itakuwa na sauti kubwa kwenye muungano, as long as it exist (Tanganyika).

It's up to Zanzibaris, nchi moja au mbili, ikli mradi Tanganyika iwepo. other than that, hatutawatendea haki wanetu.
 
Maggid umempinga shivji kwasababu amepinga serikali tatizo tu bila kuangalia udhaifu wa rasimu.
Embu msome hapa
' Alibainisha rasimu hiyo imekosa maelezo ya
wazi na thabiti kuhusu ukuu wa Katiba ya
Muungano juu ya katiba nyingine za washirika
wa Muungano, hali itakayosababisha
migongano na kutoelewana kati ya mamlaka za
washirika wa Muungano na mamlaka ya
Jamhuri ya Muungano.
Alisema kuwa Ibara ya nane ya rasimu hiyo
inayozungumzia ukuu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano inayopendekezwa ina kasoro kubwa
kwani imeeleza kuwa ukuu wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano utakuwa katika mambo
ya Muungano tu na si vinginevyo.
“Ukisoma rasimu hii ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano katika Ibara ya 8(1) inasema na
hapa nitanukuu: “Bila ya kuathiri masharti ya
katiba za washirika wa Muungano kwa mambo
yasiyo ya Muungano, Katiba hii itakuwa sheria
kuu katika Jamhuri ya Muungano,” mwisho wa
kunukuu. Kwa hiyo Ibara hii inaeleza wazi
kabisa kuwa katiba inayopendekezwa haitakuwa
na nguvu za kisheria juu ya katiba za washirika
wa Muungano,” alisema Shivji.
Alifafanua kuwa katiba zote za nchi zinazofuata
muundo wa shirikisho kama unaopendekezwa
na Tume ya Warioba zikiwemo Katiba za
Marekani na Australia, zina vipengele
vinavyoeleza wazi kuwa katiba ya shirikisho ni
sheria kuu juu ya katiba za washirika, hali
aliyosema imeondoa mianya ya kuibuka kwa
migongano kati ya mamlaka za shirikisho na
washirika wao.
Kwa msingi huo, Profesa Shivji alisema kuwa
muundo wa Muungano unaopendekezwa ndani
ya rasimu ya Warioba ni tegemezi na dhaifu
kwasababu haujawekewa nguvu ya kikatiba ya
kuulinda na kuupa mamlaka thabiti.
 
mawenge,

..kama Prof amesema hayo uliyaandika basi atakuwa analinganisha apples and oranges.

..sidhani kama tunapaswa kulinganisha Tanzania[Tanganyika + Zanzibar] na Marekani au Australia.
 
Last edited by a moderator:
Huwa najiuliza kwanini hatuchukii hatua hizi?
Kura ya maoni kwa wznz
(Puerto rico, Quebec, Timor, Iereland, Sudan n.k) hawa wote wamefanya kura za maoni kwa matokeo tofauti.

Endapo znz wanataka muungano wanapaswa waulizwe ni wata sacrifice na kipi hawatatoa.
-Wakikubali mchakato uendelee
-Wakikataa basi tukutane EAC

Ningefurahi sana kama prof Shivji angesimamia hoja hii amabyo amekuwa anaieleza huko znz miaka mingi.
Prof husema wananchi hawakuulizwa kuhusu muungano na znz iliburuzwa. Sasa anatakiwa aungane na akina Maalim Seif, Jussa, Himid Mansour, Sheikh Farid kudai kura ya maoni. Mimi ninawaunga mkono kwa hilo.
 
Ninathubutu kusema kuwa baadhi yetu humu hatukumwelewa Prof. Shivji. Na kama tulimwelewa, tunapindisha alichokisema kutokana na kuathiriwa na mambo tunayoyaamini.

Pamoja na kutoa mawazo yake kuhusu muundo wa muungano, la msingi alilolisema Shivji ni makosa kuzungumzia muungano kwa jicho la idadi ya serikali. Alisema, muungano ni suala la demokrasia. Si suala la idadi ya serikali peke yake. Watu wa pande mbili wanakubali kuungana na kufanya mambo yao kwa utaratibu wanaouchagua.

Shivji pia alieleza kwa ufasaha kuwa rasimu ya katiba ilivyo sasa itadhoofisha muungano. Hii ni kutokana na ukweli kuwa katiba itakayotokana na rasimu hii itakosa ukuu (Supremacy of the Law). Yaani katiba ya muungano inashauri badala ya kushurutisha nchi washirika. Hivyo, washirika wana hiari na si wajibu kufanya mambo yaliyopo kwenye katiba ya muungano. Sasa, kama Katiba ya Muungano haibani nchi washirika, ni dhahiri kuwa muungano utadhoofishwa. Na ili kueleweka vema, hapa Prof Shivji alitumia mifano ya Mashirikisho mengine duniani kama Marekani na Australia (mchangiaji mmoja hapa anasema kwa makosa hii ni kufananisha chungwa na apple). Shivji pia alieleza kuwa mambo kama vyombo vya usalama, benki kuu, mipaka ya nchi washirika yalivyo kwenye rasimu ya katiba yanaweza kudhoofisha muungano.

Shivji pia alieleza kuwa rasimu ya katiba kwenye suala la muungano ni matokeo ya compromise na si consensus baina ya wajumbe wa tume. Hivyo, bado kuna manung'uniko katika kila upande: ule unaotaka muungano wa mkataba na ule unaotaka muungano wa serikali moja. Manung'uniko hupelekea migogoro.

Mhadhara wa Prof Shivji upo online sasa. Ninashauri Bw. Maggid na wengine tuusome tena tukiwa sober. Shivji is making strong arguments.
 
Ndugu Ndoa,

Profesa Shivji ametoa maoni yake. Tuamini hivyo na tuheshimu fikra zake hata kama kuna kutofautiana kimitazamo. Ndio demokrasia.
Maggid,
Iringa.

Nilivyomuelewa Shivji ni kuwa muungano wa serikali tatu unaotokana na serikali mbili ambazo ni UNEQUAL hauwezi kudumu. Na mimi nasimamia hapa.
 
Mimi katika habari hii sijaridhika kabisa kulinganishwa Zanzibar na Sudan ya Kusini. Pengine sisi ambao si wasomi tunashindwa kuelewa wakati wasomi wakiilinganisha Zanzibar na Sudan ya Kusini huwa wanakusudia vipi. Kwa ufahamu wangu, pengine mfinyu, hizi ni kesi mbili zenye maumbile na historia tofauti. Zanzibar iliungana na Tanganyika na kila moja ikiwa nchi kamili yenye mamlaka kamili. Sifikirii kuwa Sudan ya Kusini ilikuwa kama hivyo Zanzibar. Na sikumbuki kama Tanganyika iliiambia Zanzibar kuwa ni lazima ibakie katika Muungano mpaka kiama. Sasa leo upande mmoja kama unataka marekebisho ya sura ya Muungano kwa nini iwe kizazaa chote hichi. Je pale ikiwa Zanzibar itasema sisi ndiyo basi tena na Muungano huu, mambo yatakuwaje? Nafikiria kwa mitazamo kama hii itakuwa ndiyo kiama cha Zanzibar!! Subhanallah. Kwa maoni yangu, wasomi wanahitaji kuuelimisha umma hasa Watanganyika kuwa kila upande una haki ya kuendelea au kuukataa Muungano. Na hilo si kosa la uhaini wala la jinai. Na kipengele hichi nafikiria inabidi kiwemo katika vifungu vya katiba ya Muungano. Katiba imetungwa kama vile Muungano ni mfumo takatifu uliotoka mbinguni, kwa hivyo hauwezi kuvunjika kabisa. Na hii nafikiria si sahihi kabisa. Pamoja na kuheshimu sana wataalamu wetu, lakini wakati mwengine wasomi wetu wanajikomba mno kwa wanasiasa kiasi cha kushindwa kuitetea haki au ukweli.
 
Kwa maneno yako haya unakosea.....Shivji huwa hapelekeshwi na huongea kile anachoamini yeye na haya ni mawazo yake siku zote...
Fuatilia kongamano la Kwanza akitoa hotuba kuhusu Katiba mpya na kwa nini katiba mpya.....maoni yake kuhusu muungano yalikuwa ni hayo hayo....
Tunaweza kumpinga sio kosa....ila kuwa na serikali tatu ni ngumu kiutendaji kwa serikali ya muungano!


Unajuwa nini kigoda ndugu yangu? Ni kikalio hivyo shivji yuko kwa manufaa ya Nyerere. Iwapo huyu Bwana angekuwa na hoja na suluhisho bora la Muungano kwanini bado ametuacha hadi tumefikia kuuona muungano kuwa na upungufu ki8asi cha kuwa haukarabatiki kwa muundo huu anaoutaka?
 
Skiliza mzalendo.

Kwani shivji yeye kama nani hapa ? Kwani nchi yake ? Hakuna mtu yoyote anae weza kuwasemea wananchi zaidi ya wananchi wenyewe, sio warioba wala kikwete wala shein wala mpumbavu yyote, suala la muungano nani alie pendekeza serikali tatu ? Kwanza tuangalie maoni, ccm wamependekeza serikali mbili, jamuhuri ya muungano na zanzibar, ccm wa zanzibar wamependekeza hivyo hivyo ila zanzibar yenye mamlaka kamili, cuf imependekeza mkataba kwa upande wa zanzibar, kwa bara siwezi kujua, ukija kwa wananchi wa zanzibar walio wengi wengi walipendekeza muuungano wa mkataba zanzibar yenye mamlaka kamili, walio pendekeza mfumo huu uliopo ila zanzibar yenye mamlaka kamili asilimia kama 13, asilimia 66 mkataba, ni wazi kwamba wananchi ni ndio wanao guswa na muungano hakuna mwengine.

Sasa hizi serikali tatu kazitoa wapi ? Kwa chadema ? Kama kwa chadema basi ccm imekufa, inamana chadema inakauli kuliko ccm ?

Sisi wanzanizbari tunataka mkataba , au tuvunje kabisaa, hatutaki kusemewa tunataka maoni yetu yatekelzwe

Ndugu yangu nini maana ya mkataba? Ni makubaliano hivyo serikali hata ziwe 10 mradi tutatiliana sahihi wahusika chini ya document ya kisharia basi tutakuwa kwenye mkataba. Sasa huo muungano wa mkataba si itabidi kuwe na nchi huru kama kawaida yaani tanganyika na zanzibarna baadae tufanye hiyo serikali ya mkataba? Jumla ngapi zitakuwaunakumbuka ya Nyerere na Ramadhani Haji (Waziri Kiongozi wa mwanzo)?
 
Ndugu Ndoa,

Profesa Shivji ametoa maoni yake. Tuamini hivyo na tuheshimu fikra zake hata kama kuna kutofautiana kimitazamo. Ndio demokrasia.
Maggid,
Iringa.

Hozi kauli za watu mmoja mmoja ndio chachu ya mtafaruku katika taifa hili ambalo watu hawana wakati wa kufikiri nafsi zao bali fulani kasema nini! Ona wewe mwenyewe kwanini kapewa wasaa wa kusema nawe huwezi kuupata wasaa kama huo?
 
njia sahihi yani ama kuwa na serikali moja au kuvunja muungano kila bajeti watu wanalalamika pesa za maendeleo kidogo,kodi imepanda serikali ina wizara nyingi hizo gharama za serikali kuendesha serikali tatu nani abebe kama sio mwananchi wa kawaida kama tumeona hatuna haja ya muungano ni bora tuuvunje kila mtu awe kivyake

Rodrick Alexander, gharama gani za zaidi? Kwani hizo shughuli zilizopendekezwa ziwe za muungano hivi sasa hazigharamiwi hata iwe gharama mpya? Halafu unaposema serikali tatu kwani hujuwi kuwa kule zanzibar wanajihudumia serikali yao? Hili watu wengi hawalioni wanachoona kuwa Watanganyika sasa watalazimika kujigharimia kwenye serikali yao. hivyo Serikali ya watanganyika wenyewe hawako tayari kuigharamia?
 
Unaposema serikali unamaanisha nini?? Kuna mpaka serikali za mtaa ambazo zina legislature (halmashauri), Executive (mayor) na Judiciary (mahakama za jiji). Hizi nazo ni serikali.

Dola!! .. kutakuwa na dola ngapi? Au nchi ngapi? .. Hapo ndiyo tunapokataa kuwa na nchi mbili zilizoungana, ambapo kila moja ina madaraka kamili.Na serikali ya muungano ambayo madaraka yake kikatiba hayashurutishi nchi shirikishi kuyafuata.\

Yaani ukiangalia mfano, unaweza kuona kuwa Zanzibar ina uwezo wa kufanya gerrymandering na kuanzisha wilaya mpya ishirini, just to balance or to even have more votes thAn Tanganyika.

Ni bora kuwe na federation ya Tanzania ambapo Tanganyika na Zanzibar ni states. Na federal legislature pamoja na Judiciary ziwe independent and above the laws of the states. The legislature needs to be bicameral with the senate evenly distributed among the member states.

Ila hii serikali ya Muungano waliyopendekeza hawa jamaa is Bogus to say the least.

Hatuwezi kusema ni Bogus bali ni kuwa labda sisi wenyewe ndio mabogus! kwani rasimu si iko kwetu ili tuiweke sawa?
 
Ndugu Maggid na Wengine, Mawazo na Maoni ni jambo moja na uzito wa uchambuzi ni jambo jingine. Mapenzi na matamanio ya kutaka au kutotaka Muungano kwa upande mmoja, na matamanio ya serikali tatu, mbili, moja au sufuri nijambo jingine. Suala la msingi ni kuisoma kwa utulivu hoja ya Prof. shivji na kujua msingi wake ni nini. Mathalani Maggidi anataka na kutamani Serikali Tatu na sababu yake ni kuwa itakuwa imetatua kerro za Muungano. Udhaifu wa hoja ya Maggidi ni kutosema kero hizo ni nini, za nani na zinachukua sura gani? Na pili asili ya kiini cha kero hizo ni nini na namna gani Serikali Tatu zinajibu kero hizo. Mfano, Wazanzibari wengi mafukara (ambao ndio wengi) wanaaminishwa kwamba Zanzibar nje ya Muungano itakuwa na neema na ufukara wao utakoma, kwamba ufukara wao unatokana na Muungano. Je, ni sawa kiini cha ufukra ni Mungano na kwamba siku Zanibar itakapopeperusha Bendera yake UN ndio matatizo ya Wazanzibari yamekwisha? Je, Lakini pia haisemwi ni kwa namna gani Nje ya Muungano ama Serikali Tatu zinavyoweza kushugulikia hali ya migawanyiko ya kisiasa ndani ya Zanzibar yenyewe. Hili sasa halisemwi, Zanzibar inaonekana ni moja - lakini hili si sahihi sana! MUHIMU zaidi ni HATA kwa wanaopenda Serikali Tatu kama Maggidi, anachosema Prof. Shivji ni kuwa kwa namna Katiba ya Warioba ilivyo inaweka misingi na masharti dhaifu (Ya Kikatiba) ya kuulinda Muungano. Sasa mimi ningedhani Maggidi na wengine mungesoma kwa Makini na Utulivu - na sio kwa Kutumia Mioyo Yenu - Bali akili na tafakari huru - kuitazama Hoja na mantiki, ushahidi na uchambuzi wa Prof. Shivji juu ya mengi, lakini hata kwa hilo Mnalilipenda na kutamani!

Naanza kwa kuangalia nafasi za watu kama hawa(Issa Shivji na wenziwe) katika kutumia maoni yao binafsi kwa nafasi kubwa na ya ushawishi for the sake ya walio wengi. Wao wanatumika vibaya kwa nafasi na vyeo vyao. Pengine kungekuwa na mtu mwenye maoni yaliyo bora zaidi dhidio ya hoja za shivji lakini jiulize atapata wapi nafasi hiyo ya kujibu hoja za huyu bwana aliyepewa ukumbi wa Chuo kikuu, mkuu wa chuo akimpa sifa, redio na TV zote zikimpa nafasi hiyo? Hapa ndipo utumizi mbaya wahoja binafsi unapogharimu jitihada zote za usawa katika kutowa maoni. halafu watu kama hawa wanakuwepo wapi hata Taifa linaingia kwenye matatizo only kukurupuka saa kama hizi kuwatia kiwewe wananchi?
Kuhusu huu mtizamo wako juu ya zanzibar nafikiri mitizamo hii ni finyu sana! Pengine hujuwi kuwa hapo mwanzo kabla ya kufariki Karume zanzibar ilikuwa mbali kimaendeleo kwa hatuwa kadhaa mbele kuliko Tanganyika. Huu muungano ulikuwepo wakatu huo lakini zanzibar ilijitegemea kwa njia zake binafsi. Nyerere alikuwepo na hakukuwa na malalamiko kutoka upande wowotwe wa muungano.Tatizo na malalamiko ya muungano yalianzia pale palipounganishwa vyama vya siasa CCM ikawa supreme kwa serikali zote mbili. Kiama cha Zanzibar kilianza hapo.

Kuhusu hili la migogoro ndani ya Zanzibar unaliona la ajabu kiasi kwamba zanzibar haiwezi kuwa huru? Kwani yanayotokea Tanganyika sasa hivi wewe unayaona ni mshikamano huo ndani ya Taifa?Acha dharau kwanza jiangalie nafsi yako halafu mseme mwenzako!
 
serikali tatu ndio njia bora ya kuvunja muungano bila kelele, wengi tunapenda muungano ufe asubuhi na mapema
Na serikali mbili zinazopigiwa upatu na ccm hizo ndio kabisaa zitafunja muungano kwa gharama ndogo kabisa maana zanzibar wamejiapiza wanataka dola kamili hapo chacha.
 
maggid,

..wa-Znz wanaposema wanataka mamlaka kamili, wanamaanisha wanataka mamlaka kamili, siyo "mamlaka kamili."

..ndiyo maana wengine tangu zamani sana tulisema kwamba serikali 3 hazitakidhi madai ya wa-Znz wa leo.

..njia sahihi ya kujibu madai ya wa-Znz ni kukubali muungano huu uvunjike, na tushirikiane kupitia EAC.

..pia ili kuepusha uhasama na usumbufu, wa-Znz wote walioko Tanganyika wapewe status ya ukaazi wa kudumu mpaka watakapoamua uraia wanaoutaka.

cc: GHIBUU, takashi, Nguruvi3, Nonda, Kibunango, Kobello

Usisahau kuwa wapo wahamiaji kule Zenji wakitoka Tanganyika, sasa status yao iwe vipi?
 
Hata zikawa 10 lakini sisi ni
MAMLAKA KAMILI ZANZIBAR KWANZA SHENGESHA BAADAE!!!!!

Ninaamini kabisa mwamuzi wa mwisho wa ama muungano uendelee na uwe wa aina gani ni WAZANZIBARI pekee. Siyo Issa Shivji kung'angania serikali mbili. Lakini hata hivyo kama ni serikali mbili, basi iwepo serikali ya Tanganika kama nchi huru na Zanzibar kama nchi huru pia. Halafu kuwepo na aina fulani ya shirikisho kama ilivyo Jumuia ya Africa Mashariki, kwa maana kwamba kuwepo na bunge dogo sana la kushughulikia yale mambo saba ya muungano. Wabunge saba kila upande na mawaziri watano tu. Napenda nisilipuuze vilevile wazo la Muungano wa Mkataba unaopendekezwa na wenzetu wa Zanzibar, ili mradi wajitokeze na kuuelezea kwa umakini muundo wake. Hili la Zanzibar kuwa nchi kamili ni takwa muhimu kwa Wazanzibari walio wengi, lisipuuzwe. Kama ndivyo hivyo, Tanganyika nayo ifufuliwe.
 
Back
Top Bottom