Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nakubaliana na wewe.maggid,
..wa-Znz wanaposema wanataka mamlaka kamili, wanamaanisha wanataka mamlaka kamili, siyo "mamlaka kamili."
..ndiyo maana wengine tangu zamani sana tulisema kwamba serikali 3 hazitakidhi madai ya wa-Znz wa leo.
..njia sahihi ya kujibu madai ya wa-Znz ni kukubali muungano huu uvunjike, na tushirikiane kupitia EAC.
..pia ili kuepusha uhasama na usumbufu, wa-Znz wote walioko Tanganyika wapewe status ya ukaazi wa kudumu mpaka watakapoamua uraia wanaoutaka.
cc: GHIBUU, takashi, Nguruvi3, Nonda, Kibunango, Kobello
Ndugu Ndoa,
Profesa Shivji ametoa maoni yake. Tuamini hivyo na tuheshimu fikra zake hata kama kuna kutofautiana kimitazamo. Ndio demokrasia.
Maggid,
Iringa.
Kwa maneno yako haya unakosea.....Shivji huwa hapelekeshwi na huongea kile anachoamini yeye na haya ni mawazo yake siku zote...
Fuatilia kongamano la Kwanza akitoa hotuba kuhusu Katiba mpya na kwa nini katiba mpya.....maoni yake kuhusu muungano yalikuwa ni hayo hayo....
Tunaweza kumpinga sio kosa....ila kuwa na serikali tatu ni ngumu kiutendaji kwa serikali ya muungano!
Skiliza mzalendo.
Kwani shivji yeye kama nani hapa ? Kwani nchi yake ? Hakuna mtu yoyote anae weza kuwasemea wananchi zaidi ya wananchi wenyewe, sio warioba wala kikwete wala shein wala mpumbavu yyote, suala la muungano nani alie pendekeza serikali tatu ? Kwanza tuangalie maoni, ccm wamependekeza serikali mbili, jamuhuri ya muungano na zanzibar, ccm wa zanzibar wamependekeza hivyo hivyo ila zanzibar yenye mamlaka kamili, cuf imependekeza mkataba kwa upande wa zanzibar, kwa bara siwezi kujua, ukija kwa wananchi wa zanzibar walio wengi wengi walipendekeza muuungano wa mkataba zanzibar yenye mamlaka kamili, walio pendekeza mfumo huu uliopo ila zanzibar yenye mamlaka kamili asilimia kama 13, asilimia 66 mkataba, ni wazi kwamba wananchi ni ndio wanao guswa na muungano hakuna mwengine.
Sasa hizi serikali tatu kazitoa wapi ? Kwa chadema ? Kama kwa chadema basi ccm imekufa, inamana chadema inakauli kuliko ccm ?
Sisi wanzanizbari tunataka mkataba , au tuvunje kabisaa, hatutaki kusemewa tunataka maoni yetu yatekelzwe
Ndugu Ndoa,
Profesa Shivji ametoa maoni yake. Tuamini hivyo na tuheshimu fikra zake hata kama kuna kutofautiana kimitazamo. Ndio demokrasia.
Maggid,
Iringa.
njia sahihi yani ama kuwa na serikali moja au kuvunja muungano kila bajeti watu wanalalamika pesa za maendeleo kidogo,kodi imepanda serikali ina wizara nyingi hizo gharama za serikali kuendesha serikali tatu nani abebe kama sio mwananchi wa kawaida kama tumeona hatuna haja ya muungano ni bora tuuvunje kila mtu awe kivyake
Unaposema serikali unamaanisha nini?? Kuna mpaka serikali za mtaa ambazo zina legislature (halmashauri), Executive (mayor) na Judiciary (mahakama za jiji). Hizi nazo ni serikali.
Dola!! .. kutakuwa na dola ngapi? Au nchi ngapi? .. Hapo ndiyo tunapokataa kuwa na nchi mbili zilizoungana, ambapo kila moja ina madaraka kamili.Na serikali ya muungano ambayo madaraka yake kikatiba hayashurutishi nchi shirikishi kuyafuata.\
Yaani ukiangalia mfano, unaweza kuona kuwa Zanzibar ina uwezo wa kufanya gerrymandering na kuanzisha wilaya mpya ishirini, just to balance or to even have more votes thAn Tanganyika.
Ni bora kuwe na federation ya Tanzania ambapo Tanganyika na Zanzibar ni states. Na federal legislature pamoja na Judiciary ziwe independent and above the laws of the states. The legislature needs to be bicameral with the senate evenly distributed among the member states.
Ila hii serikali ya Muungano waliyopendekeza hawa jamaa is Bogus to say the least.
Ndugu Maggid na Wengine, Mawazo na Maoni ni jambo moja na uzito wa uchambuzi ni jambo jingine. Mapenzi na matamanio ya kutaka au kutotaka Muungano kwa upande mmoja, na matamanio ya serikali tatu, mbili, moja au sufuri nijambo jingine. Suala la msingi ni kuisoma kwa utulivu hoja ya Prof. shivji na kujua msingi wake ni nini. Mathalani Maggidi anataka na kutamani Serikali Tatu na sababu yake ni kuwa itakuwa imetatua kerro za Muungano. Udhaifu wa hoja ya Maggidi ni kutosema kero hizo ni nini, za nani na zinachukua sura gani? Na pili asili ya kiini cha kero hizo ni nini na namna gani Serikali Tatu zinajibu kero hizo. Mfano, Wazanzibari wengi mafukara (ambao ndio wengi) wanaaminishwa kwamba Zanzibar nje ya Muungano itakuwa na neema na ufukara wao utakoma, kwamba ufukara wao unatokana na Muungano. Je, ni sawa kiini cha ufukra ni Mungano na kwamba siku Zanibar itakapopeperusha Bendera yake UN ndio matatizo ya Wazanzibari yamekwisha? Je, Lakini pia haisemwi ni kwa namna gani Nje ya Muungano ama Serikali Tatu zinavyoweza kushugulikia hali ya migawanyiko ya kisiasa ndani ya Zanzibar yenyewe. Hili sasa halisemwi, Zanzibar inaonekana ni moja - lakini hili si sahihi sana! MUHIMU zaidi ni HATA kwa wanaopenda Serikali Tatu kama Maggidi, anachosema Prof. Shivji ni kuwa kwa namna Katiba ya Warioba ilivyo inaweka misingi na masharti dhaifu (Ya Kikatiba) ya kuulinda Muungano. Sasa mimi ningedhani Maggidi na wengine mungesoma kwa Makini na Utulivu - na sio kwa Kutumia Mioyo Yenu - Bali akili na tafakari huru - kuitazama Hoja na mantiki, ushahidi na uchambuzi wa Prof. Shivji juu ya mengi, lakini hata kwa hilo Mnalilipenda na kutamani!
Na serikali mbili zinazopigiwa upatu na ccm hizo ndio kabisaa zitafunja muungano kwa gharama ndogo kabisa maana zanzibar wamejiapiza wanataka dola kamili hapo chacha.serikali tatu ndio njia bora ya kuvunja muungano bila kelele, wengi tunapenda muungano ufe asubuhi na mapema
maggid,
..wa-Znz wanaposema wanataka mamlaka kamili, wanamaanisha wanataka mamlaka kamili, siyo "mamlaka kamili."
..ndiyo maana wengine tangu zamani sana tulisema kwamba serikali 3 hazitakidhi madai ya wa-Znz wa leo.
..njia sahihi ya kujibu madai ya wa-Znz ni kukubali muungano huu uvunjike, na tushirikiane kupitia EAC.
..pia ili kuepusha uhasama na usumbufu, wa-Znz wote walioko Tanganyika wapewe status ya ukaazi wa kudumu mpaka watakapoamua uraia wanaoutaka.
cc: GHIBUU, takashi, Nguruvi3, Nonda, Kibunango, Kobello
Hata zikawa 10 lakini sisi ni
MAMLAKA KAMILI ZANZIBAR KWANZA SHENGESHA BAADAE!!!!!