Kupinga Serikali Tatu; Natofautiana Na Profesa Issa Shivji...

Labda mkuu tusaidiane wewe/au Shivji una/ana maana gani na hiyo Supremacy of the law inayotakiwa kwa katiba ya Muungano juu ya katiba za nchi washirika? lakini kama anachokitaka ni katiba yenye uwezo wa ku overrule katiba za Washirika hata katika masuala yasiyo ya kimuungano nadhani hapo ameenda mbali na kama anatamani kukiona hicho kitu kwa nini asipendekeze tukawa na na serikali moja tu nadhani hiyo itakuwa tafsiri sahihi ya supremacy ya katiba ya muungano kwa nchi washirika? lakini swali ni kwamba anaweza kuyasema hayo mbele ya wazanzibari wenzake? mimi ilidhani hicho anachokiita udhaifu wa katiba ya muungano katika masuala kadhaa ndiyo matakwa halisi ya wazanzibar ambao wanataka mamlaka kamili, au tuseme kinachomtisha Shivji ni Watanganyika(sleeping giants) kupata mamlaka kamili ya kufanya self determination? kama itakavyokuwa kwa Zanzibar, Kwa Shivji anataka kutengeneza/kuimarisha ukuta ambao utawazuia watanganyika kuamua hatima ya muungano kwa kushauri uwepo wa vipengele zuizi vya kikatiba. vitakavyoendelea kuwanyima uhuru watanganyika kuamua hatima yao ndani au nje ya muungano! Huyu jamaa anadhani shule kaenda peke yake na waliobaki ni mazumbukuku wa kupelekeshwa kama anavyotaka ati!!
 
serikali tatu ni sahihi kabisa katika tanzania ya leo,taitizo langu ni moja tu,9 decembernchi mbili ziliungana na kuzaa nchi mpya ambayo haikuwepo awali nayo ni TANZANIA,nchi wanachama wa muungano huo ni TANGANYIKA na ZANZIBAR lakini leo mbona katiba inaitaja Tanzania bara hii ni nchi ya tatu katika huu muungano?mbona kuna kigugumizi kuitaja Tanganyika katika katiba hii mpya,mimi ni mtanganyika halisi naipenda Tanganyika na pia naidai iwepo au kuna nini?
 
napenda serikali moja tu. Either Muungano wa serikali moja na zanzibar iwe jimbo au mkoa (maana hata wakazi wa sengerema au geita ni wengi kuliko raia wote wa unguja na pemba) au muungano usiwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…