Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

Kupinga wagombea huru, ni uamuzi wa "Kipumbavu"

Wanajua kabisa kuwa Mwaka huu itashindikana na mambo haya huwa wanayaleta kila baada ya muda wa uchaguzi uanze, Babu la msingi hapa ni kuandika katiba upya na kuruhusu mgombea binafsi
 
Waziri ameniacha hoi anaposema ati wanafanya kazi za serikali? Kazi gani za serikali kama sio ujambazi na wizi ambao unatokea kila siku? Je, utekelezaji wa hukumu ya mahakama sio kazi mojawapo? Mijitu mijizi hata siku moja haiwezi kuacha. Vile vile ameshindwa kujibu swala la utekelezaji wa hukumu iliyotolewa mwaka 2006. Hii ni serikali ya kitapeli sasa kwa nini wanakataa mgombea binafsi ni kwa sababu wanafahamu siku zao zinahesabika.

BRAVO MM Mwanakijiji.
 
MM tunashukuru kwa interview..duhh!! yaani umewavua nguo..ni watupu kabisa hawa watawala ktk karne hii ya 21.
 
Mkuu MM,

Bravo na hongera sana. Quality ya sound is excellent. Sishangazwi sana na majibu ya Mh. Marmo; ni wale wale tu!!!

Hivi naomba kujuzwa hapa; wakati mahakama inatoa hukumu ya 2006 hakukuwa na deadline ya rufaa? Why have they taken loong time to submit?
 
Mzee MM shukrani kwa kutuunganisha na waziri.

Ombi kwa nn usifanye hivi kwa niaba ya JF kuwahoji,kuwashauri ,kuwapa madukuku na maoni ya wananchi mawaziri wote kwa style kama hii ya mahojiano .

Otherwise agenda kuu amabyo Mh Marmo anatakiwa kujua ni katiba mpya ni bora kuliko katiba yenye viraka.
 
Good Job MMJJ,

Bahati mbaya majibu ya waziri yanasikitisha na inaonekana wazi kuwa ilikuwa ni vigumu kumshurutisha/ kum-bana kutoa majibu ya uhakika kwa vile alikuwa na uwezo wa kukata simu wakati wowote na ukawa ndio mwisho wa maongezi. Nilichoelewa toka kwake ni kuwa;
  1. Serikali ya JK hawayathamini, hawayaogopi na wala hawayaheshimu maamuzi ya Mahakama
  2. Watafanya uchaguzi kwa jinsi wanavyotaka wao
  3. Marmo ana kiburi na pengine dharau. Majibu mengi aliyotoa ni ya dharau kama vile MMJJ/wasikilizaji wake hawana uwezo wa kumfanya lolote kwa atakayosema.
  4. Serikali ya JK inaelekea hawajui nini cha kufanya juu ya hili jambo japokuwa wao wenyewe hawalitaki. Inaonekana wazi kuwa wakishikinizwa na waTZ, wafadhili n.k., wanaweza wakaruhusu kwa shingo upande, lakini late in the game.
 
MM, nimependa mahojiano yako na mheshimiwa Marmo, umemuuliza maswali magumu japokuwa alikuwa anatoa majibu mepesi kwa maswali magumu. Tunahitaji watu wa aina yako, maana nilikuwa natatizika wakati mheshimiwa rais akiwa anaongea na waandishi, hayo maswali wanayouliza huwa naamua kuzima tv.
 
NI muhimu kujua kuwa Marmo anatetea serikali na msimamo wa serikali; amejaribu kufunua fikra zilizoko nyuma ya uamuzi wao ambazo naweza kusema ni "delay tactics".

a. Wanaweza wakaamua kuahirisha uchaguzi (ili watawale kwa siku kadhaa zaidi)
b. Wanaweza kuweka masharti magumu kweli kwa wagombea binafsi ili kufanya uwepo wao kuwa mgumu kweli.
 
NI muhimu kujua kuwa Marmo anatetea serikali na msimamo wa serikali; amejaribu kufunua fikra zilizoko nyuma ya uamuzi wao ambazo naweza kusema ni "delay tactics".

a. Wanaweza wakaamua kuahirisha uchaguzi (ili watawale kwa siku kadhaa zaidi)
b. Wanaweza kuweka masharti magumu kweli kwa wagombea binafsi ili kufanya uwepo wao kuwa mgumu kweli.[/QUOTE
Ni kweli kabisa.Na katika A wanaweza kuahirisha uchaguzi ili wajipange vizuri na kuwaumiza upinzani kwani watakuwa wamejiandaa kulinagana na ratiba iliyopo sasa.
 
sawa huo uchaguzi na upelekwe mbele, lakini mahamuzi ya mahakama ni lazima yafuatwe, mtu anapohukumiwa kifungu,hawezi amua ni lini ataanza tumikia hicho kifungo.
 
Good Job MMJJ,

Bahati mbaya majibu ya waziri yanasikitisha na inaonekana wazi kuwa ilikuwa ni vigumu kumshurutisha/ kum-bana kutoa majibu ya uhakika kwa vile alikuwa na uwezo wa kukata simu wakati wowote na ukawa ndio mwisho wa maongezi. Nilichoelewa toka kwake ni kuwa;
  1. Serikali ya JK hawayathamini, hawayaogopi na wala hawayaheshimu maamuzi ya Mahakama
pamoja na kumuita Nyerere dikteta na haambiliki, Nyerere mara zote aliheshimu mahakama, alikuwa na uwezo wa kuingilia mahakama lakini mara zote alijizuia hilo. Ni hadi alipoingia kwanza Mwinyi, halafu Mkapa na sasa Kikwete wanaona mahakama ziko chini yao. Yaani, ni kama zinawasumbua tu.

  1. Watafanya uchaguzi kwa jinsi wanavyotaka wao
Hili nadhani ndio wanataka kufanya; kwamba wao ni serikali na watafanya wanalopenda.

  1. Marmo ana kiburi na pengine dharau. Majibu mengi aliyotoa ni ya dharau kama vile MMJJ/wasikilizaji wake hawana uwezo wa kumfanya lolote kwa atakayosema.
wakati mwingine nafikiri ni kile kinachoitwa kiburi cha madaraka.

  1. Serikali ya JK inaelekea hawajui nini cha kufanya juu ya hili jambo japokuwa wao wenyewe hawalitaki. Inaonekana wazi kuwa wakishikinizwa na waTZ, wafadhili n.k., wanaweza wakaruhusu kwa shingo upande, lakini late in the game.
Nafikiri wanajua lakini hawako tayari kuface reality.. wangependa kweli wagombea binafsi wasije chini ya ngwe hii ya pili ya JK kwani inamtishia JK zaidi.
 
sawa huo uchaguzi na upelekwe mbele, lakini mahamuzi ya mahakama ni lazima yafuatwe, mtu anapohukumiwa kifungu,hawezi amua ni lini ataanza tumikia hicho kifungo.

serikali inaoonekana inaweza kufanya hivyo.. kumbuka katika kukata rufaa kwao hawakutaka mahakama ya rufaa isitishe utekelezaji wa hukumu ile ya awali; ndio maana jaji mkuu aliwaambia hukumu ya awali bado inasimama.
 
thanx mzee heshima yako its me new future aka conquest,lakini hawa wajamaa wa ccm watakubali hilo kwani mie naona wanajiaandaa kutoa bomu 2010 pia hawawezi kuachia ngazi kirahisi wakale wapi na hapo ndio wamefika huyo marmo nae yumo hukohuko mzee umasikini ni wetu till the end of time.
conquest.
 
mzee kuna hili wenzetu wachina hata mzee qunfuu yumo,vijana ndio usiseme, hali kadhalika na hao wengine wenye maendeleo sie kwetu ni wizi na uchawi tuu angalia mzee wasomi wote wanenda kusfanya kazi nje ya nchi vijana matejaa wa unga wazee wachawi na uganga wasichana ukahaba hivi jamani kutakuwa na mabadiliko tufanyeje hapo ingekuwa memory card is just to format what about watz
i seek and tied of this tz
conquest
 
serikali inaoonekana inaweza kufanya hivyo.. kumbuka katika kukata rufaa kwao hawakutaka mahakama ya rufaa isitishe utekelezaji wa hukumu ile ya awali; ndio maana jaji mkuu aliwaambia hukumu ya awali bado inasimama.

serikali yetu mara nyingi inafeli kwa kukosa mipango mbadala, wao walijuwa tunakata rufaa na tutashinda, kama ingelikuwepo hiyo plan b nadhani hizi dana dana zote zisingekuwepo.
 
serikali inaoonekana inaweza kufanya hivyo.. kumbuka katika kukata rufaa kwao hawakutaka mahakama ya rufaa isitishe utekelezaji wa hukumu ile ya awali; ndio maana jaji mkuu aliwaambia hukumu ya awali bado inasimama.
.
Hili suala la mgombea binafsi linanisikitisha na kunihuzunisha, kwa maoni yangu, sio tuu serikali inaidharau mahakama, bali mahakama yenyewe inajidharaulisha na kupelekea kudharauliwa.

Kwa mjibu wa taratibu zetu hukumu ikishatolewa utekelezaji wa hukumu hiyo huanza mara moja, hata kama kumekatwa rufaa, na utekelezaji huo utasitishwa na mahakama pale tuu inapothibitishwa utekelezaji wa hukumu husika una adverse effect endapo rufani itashindwa.

Baada ya hukumu ile mwaka 2006, serikali ingepata adverse effects gani kama ingeanza maandalizi ya mgombea binafsi?. Kumbe rufani siku hizi ndio stay order ya kuzuia utekelezaji wahukumu?. Yote haya mahakama imeyaona na imekubali kuchezewa.

Nina imani na Jaji Mkuu, atairudishia hadhi mahakama, japo serikali itakuja na hoja za muda uliobakia hautoshi!.

Uamuzi ni mwezi ujao, muda wa maandalizi kwa first track unatosha, uchaguzi hausogezwi hata siku moja na mgombea binafsi yupo.
 
Nafikiri wanajua lakini hawako tayari kuface reality.. wangependa kweli wagombea binafsi wasije chini ya ngwe hii ya pili ya JK kwani inamtishia JK zaidi.
Nafikiri you are right kuwa sirikali ya JK wangependa kikombe hiki kiwapite maana kwao ni sumu.

But I could as well feel some fear from them. Inaelekea hawataki liwe jambo kubwa kabla ya uchaguzi ili wenye nguvu (wafadhili) wasije wakawapa summons wajieleze. JK anaogopa sana kufananishwa na akina M7, Mugabe n.k. katika kuibinya demokrasia. Sura ya matendo ya serikali yake ni muhimu sana kwa u-vasco dagama wake.

Tatizo ni kuwa it is very unlikely kuwa waTZ watakuwa organised kulipinga hili suala na ku-draw attention ya international community kabla ya uchaguzi.
 
Tatizo ni kuwa it is very unlikely kuwa waTZ watakuwa organised kulipinga hili suala na ku-draw attention ya international community kabla ya uchaguzi.

Watanzania ni wa tiifu wa nidhamu ya wanakondoo, hatuna utamaduni kugoma/kuipinga serikali yao ndio maana kila baada ya miaka 5 tunaichagua kwa kishindo, sisi ni yes man, bendera fuata upepo na kanyaga twende!

Unless otherwise newtons laws of motion ziapply kwenye 'a body in motion'
where will that other force come from?. Dr. Slaa mwenyewe na Mwanakijiji peke yao hawawezi, hao wengine wakowapi?.
 
Nafikiri you are right kuwa sirikali ya JK wangependa kikombe hiki kiwapite maana kwao ni sumu.

Nimependa hiyo; ni kweli kwa sababu ukiangalia sana utaona kuwa wagombea binafsi wanaitishia CCM sasa hivi kwa sababu iko at its weakest point na kama wahenga wasemavyo "kamba hukatika pembamba". Kuruhusu wagombea huru sasa hivi ni kujaribu kuivuta kamba iliyokwisha anza kukatika. Na fikiria kuwa JK akisimama na mgombea huru hana uwezo wa kushinda.

But I could as well feel some fear from them. Inaelekea hawataki liwe jambo kubwa kabla ya uchaguzi ili wenye nguvu (wafadhili) wasije wakawapa summons wajieleze. JK anaogopa sana kufananishwa na akina M7, Mugabe n.k. katika kuibinya demokrasia. Sura ya matendo ya serikali yake ni muhimu sana kwa u-vasco dagama wake.

Strategy ya JK iko hivi: watengenezee wengine mazingira bora ya kiutawala wewe mwenyewe endelea hivyo hivyo. Ndio maana ya kuja na hizi sheria za kusema "ati tukiondoka tuache mazingira bora ya utawala" kama alivyosema pale Mwanza kwa TAKUKURU. Yaani mazingira bora ya utawala yaje baada ya yeye kuondoka kutawala!

Tatizo ni kuwa it is very unlikely kuwa waTZ watakuwa organised kulipinga hili suala na ku-draw attention ya international community kabla ya uchaguzi.

Ukisoma hukumu ya awali ya kina Lugakingira kwa mara ya kwanza Mahakama ililaani waziwazi uamuzi wa serikali kubypass maamuzi ya mahakama na kwenda kubadili katiba wakati suala bado liko mahakamani. Na hili utaliona likirudiwa kwenye hukumu ya Mahakama ya Rufani muda si mrefu ujao.
 
Back
Top Bottom