Kupita bila kupingwa, Kuna wenzenu hawana aibu kabisa

Kupita bila kupingwa, Kuna wenzenu hawana aibu kabisa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Kuna mtu hawazi Wala kufikiria watu watasema nini mtoto na mwanawe kupita bila kupingwa katikati ya watanzania 65,000,000.

Hata kama unasema hujui lakini hii inaweza kukulazimisha kujua.

Baada ya baba wa taifa kufa, nani amebakia kutuambia acheni kufanya hivi?
 
Pia ni AIBU kwa First Lady kugombea Ubunge badala ya kuwa na NGO ya kutoa ushauri au misaada kwa kijamii
 
Hivi hawana aibu? Na aliependekeza hili litokee kama hivi ni mtu wa kuaminika huyu ndani ya jamii?
 
Pambaneni na hali zenu mkiambiwa NRNE mnaikataa Sasa mchawi kabaki kwenu.
 
Pambaneni na hali zenu mkiambiwa NRNE mnaikataa Sasa mchawi kabaki kwenu.
Ukitaka ukweli wa Mungu, mwasisi wa figisu za kupita bila kupingwa kwenye uteuzi ndani ya chama alikuwa Mwl. Nyerere. Alijifanyia hivyo yeye mwenyewe kwa miaka yake yote 23 ya kutawala na alimfanyia hivyo Mzee Ali Hassan Mwinyi. Tofauti ya Mwl Nyerere na Hawa wa Sasa ni kwamba, Mwl hakuwahi kushawishi ndugu yake apite bila kupingwa kwenye ubunge.
 
Kuna mtu hawazi Wala kufikiria watu watasema nini mtoto na mwanawe kupita bila kupingwa katikati ya watanzania 65,000,000.

Hata kama unasema hujui lakini hii inaweza kukulazimisha kujua.

Baada ya baba wa taifa kufa, nani amebakia kutuambia acheni kufanya hivi?
Unajua tuache wivu usiokuwa na maana yoyote ile,muhimu hilo jimbo kuna vyama vya upinzani wakapambane wachukue jimbo
 
Unajua tuache wivu usiokuwa na maana yoyote ile,muhimu hilo jimbo kuna vyama vya upinzani wakapambane wachukue jimbo
Hata wanaCCM wanaotaka maisha (ubunge) wa jimbo ni wengi, wanafamilia wote kupita bila kupingwa haitokei kwa bahati mbaya tu. Hii inachafua murua kabisakabisa. Heri wangewaacha na watu wengine wajitokeze na kupitishwa halafu waende kushindwa kiaina huko mbele ya safari.
 
Kila akiingia bunge kupambania mafao ya wenza wa rais, ina maana anapata posho ya mwenza wa mke wa rais, mshahra wa kibunge.
Na bado anapita bila ya kupingwa haya tafuneni nchi hiii mpk muimalize.
 
Back
Top Bottom