Kupitia kinachoendelea ndani ya CHADEMA ni dhahiri CCM itaendelea kuwa chama dola kwa muda wa miaka mingi ijayo

Kupitia kinachoendelea ndani ya CHADEMA ni dhahiri CCM itaendelea kuwa chama dola kwa muda wa miaka mingi ijayo

Alpaslan Bey

Senior Member
Joined
Nov 4, 2023
Posts
121
Reaction score
163
Ndugu wana JF,

Ni ukweli usiofichika mpaka sasa CHADEMA imeshaingia kwenye mtego wa CCM na kazi nzuri iliyofanywa na watu ambao ni very smart na kwa uangalifu mkubwa ni kama imeshamalizika ikiwa na athari hasi kwa miaka mingi sana ijayo kwa CHADEMA na athari chanya kwa CCM.

Kete muhimu za kuimaliza CHADEMA zilianza mara tu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 na kuendelea mara tu baada ya uchaguzi wa mwaka 2020. Kila uchaguzi ulikuwa na experience yake na yaliyoendelea baada ya hapo yana uzoefu tofauti pia.

Baada ya 2015 wabunge wengi walirudi nyumbani na maneno "kuunga mkono juhudi" yalizaliwa na kushika kasi sana na kazi hii ilimalizika 2020. Baada ya hapo maneno kuunga juhudi yalikufa na kuibuka maneno mapya "kulamba asali" ambayo kutokana na utamu wake wapo wanaoendelea kulamba mpaka sasa.

Kwa nini sasa CCM itaendelea kutawala kwa miaka mingi ijayo???

1. Ukimfahamu muasisi wa propaganda za ukomo wa madaraka ya mwenyekiti na kwa nini sasa amenyamaza na kuunga mkono mtu huyohuyo ambaye awali alipingwa, ndipo utajua kazi imemalizika

2. Mpaka sasa watu wengi wamepoteza imani na kuamua kurudi nyuma kwa kuumizwa na yanayoendelea ndani ya CHADEMA. Wengine hapa hapa JF walikuwa wanachama, wakereketwa, washauri na wachangiaji wazuri wa michango ya hali na Mali kwenye CHADEMA na sasa wametangaza kuomba msamaha chama dola na kurudi nyumbani hata kama kuna gharama kubwa tumeilipa huko tulikokuwa.

3. Kwa mazingira ya siasa za nchi yetu kuanzisha chama kipya na kukijenga mpaka kisimame kinahitaji miaka mingi sana kitu ambacho kitaifanya CCM iendelee kutamba kwa miaka mingi sana ijayo hivyo hata wakivurugana na baadhi yao kuamua kuanzisha chama kipya ni dhahiri hawataweza kusimama kwa haraka

4. Uamuzi wa Lissu kugombea umeicha CHADEMA uchi mbele ya wafuasi na wanachama wake. Imeonyesha jinsi viongozi wasivyo wamoja na jinsi walivyo wabinafsi linapokuja suala la maslahi yao. Ni dhahiri kwa wanachama wengi imedhihirika ya kwamba malengo hasa ya CHADEMA ni kuendelea kuwa chama cha upinzani na sio vinginevyo.

5. Kwa yanayoendelea ndanibya CHADEMA, itahitaji miaka mingi sana ijayo kwa CHADEMA kurudisha imani yake kwa wanachama na wafuasi wake na pengine isije ikafanikiwa kuwa mahali ilipokuwa imefika kwa siku zake zote ilizobakiza kuishi kama chama cha siasa hapa duniani 😂

USHAURI WANGU kwa wanaJF wenzangu hususani wale tunaopenda siasa.

Taifa letu, wananchi na mifumo yetu yote tuliyonayo haijawahi kuwa tayari kwa utekelezaji wa mfumo wa vyama vingi hivyo nawasihi "Tukubali turudi nyumbani CCM na tukashirikiane na wazalendo wengine wengi walioko huko kulijenga taifa letu mpaka wakati wa Mwenyezi Mungu mwenye taifa lake kuamua vinginevyo ila kwa sasa ni kujidanganya". Ukweli wa jambo hili unachagizwa na matokeo ya tume ya kukusanya maoni kuhusu uanzishwaji wa mfumo wa vyama ving miaka ya tisini ambao kimsingi watanzania asilimia 80 hawakuafiki na walipiga kura ya kuendelea kuwa na mfumo wa chama kimoja dhidi ya asilimia 20 za waliokubali mfumo wa vyama vingi.

Dokezo, "Kipindi cha mfumo wa chama kimoja kulikuwa na upinzani wenye tija sana bungeni na nchi ilinyooka" rejea ya G55 ya kina Njeru Kasaba na wenzie ilikuwa na nguvu kuliko CHADEMA na wapinzani wengine wote"
 
Back
Top Bottom