FALSAFA ZA OLIGARCHY:
MY 2 CENTS:
Kiufupi, Nipo kwenye uwekezaji zaidi ya miaka Kumi,
Wakuu nimesoma comments nyingi sana, mara real estate mara UTT mara Hatifungani, Concept ni nyingi lakini naomba nitoe njia yangu iliyonipa mafanikio kwa kiwango cha compounding.
Tujikumbushe:
Tajiri wa kwanza duniani Elon Musk, ni co founder wa makampuni mengi makubwa duniani including TESLA, SPPACE X, The Boring company. Pamoja na Utajiri wake wote Huu Hisa zake asilimia 50% zimekuwa PLEDGED kama COLLATERAL ya LOAN.
MO DEWJI KUNUNUA HISA ZA SIMBA
Mwaka 2016 Mo dewji aliwasilisha pendekezo lake la kwanza kuinunua simba, Fuatilia uzi Huu
BILIONEA MO DEWJI AWASILISHA RASMI BARUA YA KUINUNUA KLABU YA SIMBA | Rundugai Blog , Lakini zoezi la kuilipa simba halikufanyika.
Tukiangalia Hapo chini , tunaona cheki imelipwa kwenda Kwa Simba sports club Endowment Fund.
Dhumuni la hii sio kuongelea simba bali ni kuwafundisha Financial Decision making na Utofauti kati ya Watu wenye fedha na watu wasio na elimu ya fedha.
MY 2 CENTS:
Financial Assets classes zinazotoa yield
PIA zinatumika kuhedge maamuzi ya biashara yanayofanYika , Elon musk alitaka kuimiliki twitter, ili kufanya maamuzi yake kwenye playbook ile ilibidi akope kupitia hisa za kampuni anazomiliki ili anunue Twitter (
Musk says he has secured $46.5 bln in funding for Twitter bid) . Hii inaonesha hajatumia pesa yake kumiliki kampuni ya twitter kwa term nyingine tunasema amemiliki Twitter kupitia Other peoples Money (OPM). Funzo: Ukitaka kununua vitu itengenezee asset Hisa au Hatifungani ambayo itakuwa kama Backup yake
Mfano:
Nina Tsh 200,000,000 nataka ninunue Gari/Nyumba ya kuishi (Liability) ya Millioni 100, Way forward is Buy a Treasury Bond then ikopee utapigwa haircut 70% roughtly 140M lakini wewe chukua 100M nunua unachotaka kufanya may be a car (liability) au nyumba then Mkopo uliochukuliwa utajilipa na Coupon za hatifungani, after 6-8 years utakuwa na vyote Gari/Nyumba uliyonunua Plus Bond ya 200M plus Coupon ya kila semi annual
Insteas ya ungenunua kile kitu then value ingepotea.
Je unadhani Mo dewji alishindwa kulipa Mil 200 cash kuinunua simba? Hapana sio kweli kwenye ulimwengu wa kifedha kama angetoa pesa ile cash ni upuuzi wa hali ya juu. from 2016-2021 ni 5 years, kama angewekeza hzo hela kwenye Hatifungani maana yake angepata coupon za Estimated 80% value (15.95% estimates x5) so kuweka hyo hela kwenye asset classes ingemaanisha ameipata simba + ameretain value ya hela yake.
Maana ya Endowment Fund:
Huu ni mfuko wa uwekezaji ambao unasimamiwa na fund manager, hela zinawekwa halafu wanainvest kwenye both Traditional na Altenative Investments. Kwenye kila returns za kila mwaka ,kuna kuwa na withdrawal policy ila nyingi hela zinakuwa utilized nyingine zinarudishwa mfano:
Bil 20 za dewji wakanunua 25 years Bond 12.56% per annum maana yake kila mwaka watapata coupon za (12.56%*20) =2.5 Billion , ambapo 1 billion anaweza akairudisha kuinvest , so next year mfuko utakuwa na 21B instead of 20 halafu 1.5B ikatumika kwa kazi nyignine za simba.
Tafakari why endowment Fund? if you buy a share where does the money Go. (discussion for another time)
So Quick Killer points:
1. Kuna utofauti baina ya uwekezaji na Biashara, msichanganjye hizi mambo
2. Ukiwa na mtaji unaweza ukauwekeza ili kuulinda halafu ukaukopea baada ya hapo ndo ukafanya Biashara unayoitaka, Jiwe moja ndege mia
JIULIZE HALAFU FANYA MAAMUZI:
Una Milioni 200 ni bora ujenge nyumba ya kupangisha hela yote then kazi iishe? kumbuka return ya real estate kwa mwaka ni Single Digit
au
Kuwa Mjanja , chukua Milioni 200 Nunua Bond ikopee pata 140M , Jenga nyumba ya 140M pangisha
Mapato ya kupangisha mengine rudisha kununua bond,afetr 8 years Rudia njia ile ile. (Exponential Growth ndo kila kitu)
Soma: THE RICHEST MAN IN BABYLON , POOR DAD RICH DAD,
Jifunze: Utofauti wa asset na liabilities, Kusoma na kutengeneza Financial Statement (Personal).
NTASHUSHA ANDIKO SOON : THE BANK & OPM STRATEGIES (OTHER PEOPLES MONIEEEEEE)
- Kama makampuni yana Financial statement pia katika individual lvel lazima uwe na financial statement na Auditor wako ni mke wako
😉😉😉😉
-kama kwenye financial world watu wanahedge Liability, at individual level pia u can hedge your liabilities (Eti nyumba ya kuishi ni Liability au asset? Na nyumba ya kupangisha je ? liability au asset?
🙄🙄🙄
- Interest Rate Arbitrage * Ngoma hapa ntaongelea namna ya kupiga hesabu zilizomfanya simba kuwa Mfalme wa pori na kumwacha mdomo wazi Tembo mwenye mwili mkubwa! eti ukienda mbuga za wanyama unataka umwone Simba au Tembo?
- OPM vs Geo investment Opportunities- Vuka border hujazaliwa Tanzania umezaliwa duniani
Nimeongea Kimafumbo vitu vingine ila natumaini umepata kauelewa kidogo.
OLIGARCHY, CFA
(Tanzania hatufiki 10 Accredited CFA Holders) "
Nina uhaya ndani yangu, relax kabla hamjaanza kunipiga nyundo"