Kupitia UTT, Ninahitaji milioni 2 kila mwezi

Watu wenye mahela mengi sijui kwanini huwa akili zao hazina akili,sijui kwakweli.

Mil 200 nisubiri faida ya 2m kwa mwezi,mweeeh Bana eeh hela sio zangu mimi inanikereketa nini kama sio kiherehere tuu...

The same to me .sijui kwanini watu wanakuwa waogo .mimi i love adventures

Naupenda sana ujasiriamali hata nikifeli nainjoi the lessons ambazo nimejifunza .Nashangaa sana mtu anayetafuta security.


Kitu ninachojifunza vijana tujifunze kutake risk wakati tukiwa bado wadogo ili tuwe guru kwenye biashara uzeeni.

Ukizoea ku take risk inafika point ambayo hakuna kitu kinakutisha kwenye biashara kwa sababu unajua hata nikianguka nitainuka tena.

Kama mwaka nimepiga Tsh mil 100+ kutoka kwenye mtaji wa mil 7 na Mwakani natarajia kukunja mil 200+.

Ndo mtu aniambie niwekeze kwenye bond[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16].

“Uoga wako wakupoteza ,utakukosesha hela nyingi sana”-Fred Vunjabei
 
Biashara/hela nzuri ni ile ambayo hata ukiipoteza yote na ukachukuliwa ukaenda kutupwa katikati ya burundi ,unaitengeneza tena ndani ya 2-3 years.


Ile process ya kubuild something from scratch is what i love .

Unakuwa umeinuka na kuanguka mara nyingi .
 
You nailed it mkuu,hii post imemalizwa na hii comment.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]
 
UTT wanaalika members zao kwenye annual meetings pia. Hii PDF file niliyoambatanisha ni report moja wapo baada ya annual meeting ya mfuko mmoja wapo UTT. Ungeweza kuingia website ya UTT na kupata documents nyingi sana na zingejibu maswali yako mengi sana. Wapo wengi wanaobeza hapa lakini hawana ufahamu halisi wa mutual funds kama UTT ni kitu gani.

Jukumu la kujifunza unalo mwenyewe kwa kusoma vitabu, tafuta materials kwenye website husika, tembelea ofisi husika na uliza maswali, na mwisho wasiku utapata picha halisi ya kile unachotaka kukijua. Lakini hapa watakuja watu watakuambia mambo mawili matatu lakini kutokana na changamoto ya kwamba kuna watu wengine watakuja na kubeza bila kuwa na uelewa wa kutosha, utajikuta wewe unayumba.

Ningependa kuweka baadhi ya mambo sawa kulingana na nilivyoona comments nyingi humu.

1. Investment sio kitu sawa na biashara

2. Mifuko mingi ya UTT ina kua kwa compound interest rate >12% ambayo ni kubwa kuliko inflation rate ambayo ni kama 4%

3. Watu wengi wana mindset ya kufanya kazi/biashara na kupata income, wanaona kama investment na kutegemea the power of compound interest na kupata passive income ni uzembe.

4. Pesa unayotoa kwenye mfuko wako wa UTT haikatwi kodi, ila kwa baadhi ya mifuko wanakukata 1% as an exit load.

5. Watu wengi hawafikirii long term combined with the power of compound interest. Mfano vipande vya umoja fund mwaka 2005 vilikua TZS 100/kipande wakati saivi kipande ni kama 850 TZS/kipande. Sasa ni miaka 17 imepita. Fikiria mtu angekua amemuwekea TZS 3M (mwaka 2005) mwanae mdogo kwa ajili ya elimu ya juu. Mtoto anafika umri wa kwenda elimu ya juu leo(2022) angekua na kama TZS 24M, ambayo inatosha kumsomesha bila shida. Na bado sioni kama 24M ya leo ni sawa na 3M ya 2005, labda mimi sielewi inflation inavyofanya kazi, nileweshwe.

6. In a short term (one year, two years, few months) thamani ya vipande inaweza kuonekana imeshuka but in a long term, the graph is almost certainly going up!!
View attachment ANNUAL REPORT FOR LIQUID FUND- YEAR 2021_0.pdf
 
Kwahiyo pesa ya mkopo unakuwa umeokota, siyo?
Mfano chukua mkopo bank wa milion 32 kwa miaka 7 uwe unarudisha 582,142....hapa baada ya miaka saba utakuwa umewalipa bank jumla ya Tsh 48,899,928.
Lakini hiyo milion 32 tulifanye uliweka UTT ikawa inakuingizia 320,000 kila mwezi....kwa miaka saba hiyo hela itakuwa imekuzalishia 26,880,000.....sasa hii faida jumlisha na milioni 32 uliyowekeza jumla baada ya miaka 7 utakuwa na 58,880,000.
Naomba unielemishe kama nitakuwa nimebugi.
 
Ahsante sana. Ila hiyo document kwangu haifunguki msaada tafadhali
 
UTT kuna compound interest. Ukiwekeza 200m inaweza kufika 400m baada y miaka 5 au 6. Jambo jingine si Kila mtu anaweza kufanya biashara ndio maana ya kuwekeza kwenye bonds au mutual funds kama UTT
compound interest ni nini? mfano nimeweka 10 million kwenye mfuko wa ukwasi,hiyo compound interest naipataje au naionaje?
 
compound interest ni nini? mfano nimeweka 10 million kwenye mfuko wa ukwasi,hiyo compound interest naipataje au naionaje?
Compound interest: mfano capital ni 10million na interest ni 14% kwa mwaka umeweka bond Fund au liquid Fund utapata 140,000/= mwaka wa kwanza kwa hiyo capital plus interest itakuwa 11,400,000/=
Mwaka wa pili capital yako itakuwa 11,400,000/= interest 14% ......... endelea ku calculate hapo
Mwaka wa tatu nakuendelea.
 
Ooh nimekuelewa,Kwahiyo compound interest kwa lugha rahisi ni Interest on interest,sasa mimi nikijua interest unapata kulingana na idadi ya vipande uko navyo,je huo mwaka wa pili utapataje compound interest ikiwa idadi ya vipande hujaongeza?
 
Ooh nimekuelewa,Kwahiyo compound interest kwa lugha rahisi ni Interest on interest,sasa mimi nikijua interest unapata kulingana na idadi ya vipande uko navyo,je huo mwaka wa pili utapataje compound interest ikiwa idadi ya vipande hujaongeza?
Hata usipoongeza vipande, interest inakuwa calculated on accumulated interest over time as well as on your original principal yaani original investment plus the income earned from investment ( can grow together/ zinakuwa pamoja). Jambo la muhimu wekeza then forget na uendelee na michakato mingine.
 
UTT...nili nunua hisa nikiwa Form Six. Nika poteza cheti. Nilipo maliza chuo, nili fuatilia ili nijue Hisa zangu, niongeze hisa na niweze kuomba cheti kipya. Ila sikuweza kusaidiwa.
Nimepoteza Hisa zangu.
 
Weka namba yako ya M-PESA tukuchangie
 
Kwanini uhesabie thamani na bilioni 10 pekee na huesabii coupon rate unayopewa kila mwaka kwa 25 yrs?

Kwa case ya Tz;

Unatoa 10bn sometimes at a discount.

Coupon rate ni 12.56% kwa mwaka. Unalipwa kwa miaka 25.

Baada ya miaka 25 unarudishiwa 10bn yako wakati hapo kati umekula zaidi ya 31.4bn ya interest payements.

Yani 10bn yako baada ya miaka 25 unakuwa umeshapata zaidi ya 41.4bn.

Kama ulinunua kwa discount unaongeza capital gain.

Ni taahira pekee anaesema bond zinashuka thamani.
 
Mlinunua kisiasa.

Zile hisa zilikuwa overvalued na isitoshe, telecom sector ni oligopoly. Easy to be manipulated
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…