Nimepitia hoja zote kwenye huu uzi. hoja zenu zote ni nzuri na kila mtu kachangia kwa experience yake. Nimejifunza pia kuna vitu nilikuwa sijui. Pia nimeona watu wakichanganya kati ya Bond Fund ya UTT na Treasury Bond ya Serikali
Ni vyema kujua kuwa hivi vitu viwili ni tofauti.
Nimeona pia watu wakisema Treasury Bond (T-Bonds) ni biashara kichaa, hoja zao kuu ni mbili. Ya kwanza, mfumuko wa bei (inflation rate) na ya pili kuwa faida yake ndogo (low return).
Kwa hoja hizo mbili pekee wapo sahihi ila hawapo sahihi kwasababu ya hoja zifuatazo (nitazesema huku chini).
Nimeona pia baadhi ya watu wameringanisha (compare) kati ya T-Bonds na Real estate. Na kwa hoja nyingi zilipo humu wengi wamechagua Real estate over Bonds. Si jambo baya pia.
Wengine pia wamefanya comparison ya Mifuko ya UTT pamoja Hisa. Hapa kulikuwa na ukinzani, pande moja ilikubali UTT kuwa bora zaidi pande nyengine ikasema heri uwekeze tu mwenyewe kwenye hisa.
Kwanza kabla sijaendelea lazima tujue kuwa kuna utofauti kati ya Biashara na Uwekezaji. Ni kama jambo moja hivi kwasababu vyote vinahitaji pesa na lengo kuu ni kuleta faida lakini utofauti upo.
SWALI: Utofauti uko wapi? Nitakujibu
Watu wanatakiwa kujifunza sana Elimu ya uwekezaji. Elimu ya biashara imeonekana kwenye hoja nyingi sana humu ila elimu ya uwekezaji kwakweli ni kwa kiasi kidogo sana.
"Tatizo hilo"
Blah blah blah nimeongea sana sasa na mimi nitoe hoja zangu. Ngoja nifungue friji nitoe chochote kitu, nawarudia
View attachment 2372047
UTOFAUTI KATI YA BOND FUND NA TREASURY BOND (T-BONDS)
Bond fund ni mfuko wa pamoja unaotolewa na UTT AMIS, lengo lake kuu ni kukuza mtaji pamoja na kutoa gawio kwa wawekezaji wake. Gawio linatolewa kwa kila mwezi au kila baada ya miezi 6 inategemea na kiasi ulichowekeza.
Ukiwekeza kuanzia elfu 50 utakuwa kwenye mpango wa kukuza mtaji (hautopata gawio labda riba ya mwisho wa mwaka). Ukiwekeza 5M utapata gawio kila baada ya mieizi 6. Ukiwekeza 10M utapata gawio kila mwezi.
Mpango wa gawio la kila mwezi hauna kikomo cha uwekezaji unaweza kuwekeza hata Billioni
Sasa gawio linatolewaje? Gawio ni 1% ya uwekezaji wako. Tuchukulie umewekeza 200M. Ina maana utakuwa kwenye mpango wa kupata gawio kila mwezi. Kwa pesa hiyo gawio lako ni 2M kila mwezi. Yaan utapata 2M kila mwezi na pesa yako 200M itabaki kama mtaji, tena tarajia kuongezeka kwa mtaji kulingana na thamani ya vipande kukua (ila tarajia kushuka pia kwa mtaji kwasababu thamani ya vipande pia hushuka).
?????
Em Chill kiasi, pata kinywaji piga fundo moja
View attachment 2372048
Haya tuendelee sasa....
Hakuna namna unaweza kuingiza pesa bila ya kuwa na risks. Hata T-Bonds zina risks zake, moja wapo ni serikali ikifirisika na kushindwa kulipa madeni yake. Ushawahi waza nini kitatokea? Em jiulize alafu tafuta habari kuhusu Bonds za Ugiriki na Hispania nini kiliwapata wawekezaji wake.
Cha muhimu ni kupima je risks ni kubwa kiasi gani.? Risk inaendana na faida inayotarajiwa kupatikana? Mifuko ya UTT-AMIS, pamoja na T-Bonds kwakweli ni vitu venye risk ndogo sana. Risk yaje inaendana na faida tarajiwa, hivyo ondoa shaka.
Hii Bomd Fund ya UTT-AMIS haina kikomo cha muda unlike T-Bonds ambayo lazima mkubaliane na Serikali pesa yako itawekezwa kwa muda gani.
Haya turudi kwenye T-Bonds.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Leo nawahangaisha ee? Mara twende huku mara turudu huku. Lakini ndo maisha cha msingi kufahamishana
T-Bonds yenyewe unaikopesha serikali kwa muda maalumu na kwa riba maalumu. Riba haipandi wala haishuki kwa muda wote mliokubaliana. Kwa Tanzania, T-Bonds zipo za miaka 2, 5, 7, 10, 15, 20, na 25. Zote hizi zina riba tofauti tofauti. Kama ifuatavyo
View attachment 2372053
Miaka 2 riba 7.9312%
Miaka 5 riba 9.0775%
Miaka 7 riba 9.4633%
Miaka 10 riba 10.4547%
Miaka 15 riba 11.4060%
Miaka 20 riba 12.0307%
Miaka 25 riba 12.4308%
UTOFAUTI KATI YA BIASHARA NA UWEKEZAJI.
Hizi ni vitu viwili tofauti, kwa haraka haraka unaweza usikubaliane na mimi lakini ndo ukweli. Biashara inahitaji sana uwe active, uhusike moja kwa moja kwenye operation zake. Ikiwemo kutafuta wateja, masoko, kupiga mahesabu ya kila siku na mambo mengine mengi
(kabla hujaendelea kusoma, em niandikie hapo, mambo gani mengine kwenye biashara inakupaswa kufanya).
Kama wewe ni mfanyabiashara utakubaliana na mimi. Uwekezaji hauhitaji mambo yote hayo, unakuwa passive earner wewe unakuwa observer. Una oversee kipi kimeenda vyema kipi hakiko sawa. Muwekezaji ni mfanyaji maamuzi lakini sio mtendaji. Yeye huangalia biashara ipi inafanya vizuri aweke pesa zake zimletee faida.
Mfano:-
Umenunua hisa za TCC, kwenye Annual General Meeting (AGM) wanahisa mtakutana kujadili mambo kadhaa kuhusu kampuni yenu, mtatoa mapendekezo labda tuongeze uzalishaji katika product fulani (tuseme labda embassy). Hakuna mwanahisa atahusika moja kwa moja kwenye kuongeza uzalishaji wa embassy labda kama ni muajiriwa wa TCC.
Ni rahisi kwa muwekezaji kuwekeza sehemu tofauti Tofauti hata 10 na zote zikamletea faida kuliko mfanyabiashara kufanya biashara 10 na zote zimletee faida. Kumbuka biashara inahitaji muda wako.
Tofauti nyengine ni kiwango cha faida kinachotengenezwa kwenye biashara kwa mwezi ni tofauti na kwenye uwekezaji. Ila hapa kuna mushkeri kidogo.
Mara nyingi mfanyabiashara hutengeza pesa nyingi sana (kwa %) kwenye biashara yake tofauti na muwekezaji.
NOTE TO TAKE
Kumbuka nimesema mara nyingi sio mara zote. Usijichanganye ukanywa tui la nazi ukidhani ni maziwa, kama ni sumu itakuua.
View attachment 2372054
Mfanyabiashara anaweza kutengeneza faida ya hadi 40% ya mtaji wake kwa mwezi, kuna biashara zengine hata 100%. Ila hizi business za 100% hizi [emoji23][emoji23][emoji23] sio za kuziamini mara nyingi huwa za msimu au magendo (illegal)
Muwekezaji hawezi kupata faida hii kwa mwezi, na kama upo huo uwekezaji em tuambiane. Kumbuka lengo ni kufahamishana.
Em jiulize maswali yafuatayo alafu nipe jibu
SWALI LA 1:- Je? Mtu akianza biashara ikakua na kufikia hatua haimuhitaji yeye awepo ndo apate faida, yaani biashara ikianza kujiendesha yenyewe. Hiyo tutaendelea kuita biashara au uwekezaji?
SWALI LA 2:- Watu kama akina Mo Dewji, Bakhresa, au GSM. Ni wafanyabiashara au wawekezaji?
MAMBO NI MENGI SANA KUHUSU HATIFUNGANI. FAIDA NI NYINGI SANA SIWEZI KUZIANDIKA ZOTE HAPA. UNAWEZA KUTEMBELEA WEBSITE YA B.O.T KWAAJILI YA KUJIFUNZA ZAIDI
AU
Unaweza kununua nakala ya kitabu changu "IJUE HATIFUNGANI" humo nimeelezea mambo mengi sana. Faida na hasara zake, hatifungani vs instruments zengine za uwekezaji. Namna bora ya kunufaiki kupitia hatifungani na mambo mengine meeeengi
Soft Copy 10,000/=
Hard Copy 20,000/=
Nicheki PM
Kwa maelekezo zaidi