Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Waziri Mkuu aunda Tume ya watu maalumu 21 - Nov 22, 2024

Ifike kipindi serikali iachane na kununua ma-LC 300 series ya zaidi ya Bilioni 500 kwa mwaka.

Nawashauri serikali ianzishe kitengo kinachojitegemea kabisa kama walivyoanzisha DMDP pale magomeni ,basi waanzishe kietengo kinachojitegemea na maafa(Zima moto na uokozi liendelee na majukumu yake kama kawaida).

Kitengo cha maafa kiwe na vifaa vyote vya uokoaji wa uharaka ,hiki kitahusu maafa yenye large impact.

Jengo limedondoka tangia asubuhi around mbili mpaka tatu na kuna baadhi ya victims wapo kwenye vifusi hawajaokolewa ila nasikia wamepeleka oxygeni ya kuwasaidia.

Serikali inabidi iwekeze kwenye elimu ,iende ikawafundishe watu mbinu za kukabiliana na majanga na hao waliofuzu waje kuwafundisha wengine huku ,niliona clip ya jamaa(layman) tu alitoa ushauri wa kufanya kwa mamlaka jinsi ya kuwaokoa walionasa chini lakini wenye mamlaka waliyatupilia mbali ushauri/maoni yake ila akapiga moyo konde akatekeleza hivyo hivyo na ilisaidi kuwanasua waathirika.
 
reyzzap 😪😪😪 upumzike salama, kariakoo imepoteza winga machachari, angalau na sisi tupumue,
Ulikua unakabia juu sana.

Si yupo aggrey yule? Halafu nasikia analalaga dukani..
Kama alikua hapo Kwa urefu ule itakua ndio wa kwanza tofari kumuangukia..

Jamaa kaondoka na ndoto zake..

View attachment 3153973
Daaa, jamaa👆 umetutoka mapema sana,
Acheni uchawi kuku nyie, Akili zenu ni sawa na hao wabomoa nguzo...
Yaani unatoboa Meli ngo! ngo! ngo! eti "ngoja tuizamishe" halafu na wewe upo ndani.
 
Yani mkuu nikiwaza japo mara chache sana napita kule kwenye basement mana mimi sio muumini sana wa kuingia madukani ila nmewaza tu kitu kinashuka mko basement aisee!!! Mungu tuepushe na tunavyojazamaga vile
Nmewaza hivyo pia maana mwenyewe napitaga sana humo chini, haya majengo itabidi yafanyiwe ukaguzi wa kutosha na litakalobainika lipo chini ya viwango libomolewe ila rushwa haitoruhusu hayo yafanyike.
 
Nmewaza hivyo pia maana mwenyewe napitaga sana humo chini, haya majengo itabidi yafanyiwe ukaguzi wa kutosha na litakalobainika lipo chini ya viwango libomolewe ila rushwa haitoruhusu hayo yafanyike.
Hamna wa kuchunguza hapa tuishi tu kama digi digi
Inaogopesha sana na sielewi waliofunikwa na kifusi Mungu kawaisaidia kwa namna gani mana ukiwa open space si umekwisha
 
Hamna wa kuchunguza hapa tuishi tu kama digi digi
Inaogopesha sana na sielewi waliofunikwa na kifusi Mungu kawaisaidia kwa namna gani mana ukiwa open space si umekwisha
Dah hatari sana watu wanajali maslahi yao tu bila kujali uhai wa watu wengine, kwa takwimu za uokoaji hadi jana usiku, watu waliookolewa naona ni wachache sana kulingana na wingi wa watu wanaokuwa ndani ya majengo. Sijui kwa sasa hali ya uokoaji inaendeleaje.
 
Taarifa ni kwamba mwenye jengo aliona kuta zinazuia kuongeza wateja wale wanaotandaza chini hivyo aliagiza wabomoe kuta ili iwe km godauni chini wkt hizo kuta ndio zimeshikilia jengo ndio sababu njengo kushuka. chanzo mwananchi
Fundi ana ambiwa abomoe na yeye ana fanya kweli utakuta na wenyewe wamefukiwa huko chini
 
Ni hatari sana.

Tatizo kubwa zaidi lililopo Tanzania ni kwamba Hakuna mamlaka madhubuti za kudhibiti viwango na ubora wa Majengo pamoja na ubora wa bidhaa zingine mbalimbali.
Watanzania tunaishi kwa nguvu ya Mungu tu peke yake.
Mfano ajali zikitokea barabarani daily utazungumza namna hii vile vile,
Kimsingi hatujawahi kuwa seriously hata kwenye jambo moja linalohusu usalama na afya ya mtu.
Ni nani anayethibitisha usalama wa vyakula sokoni kama vinafaa?nyama ,samaki mboga mboga n.k
Ni nani asimamie ajali kupungua za barabarani?
Bidhaa feki,
Utapeli na ulaghai/dhuluma.


Tuna matatizo mengi sana,ukikoswa kwenye ghorofa unaweza kuwa mganga wa ajali barabarani.juzi juzi alikufa rafiki yangu,ninamfahamu ni kijana tuu.
 
Back
Top Bottom