Jamani jamani muogopeni Mwenyezi Mungu;
Hili suala la uasherati, ushoga ni baya sana na dini zote mbili (uislamu & Ukristo) zinalipiga marufuku,
Rejeeni maandiko hapa chini;
MOSI:
Au, je, hamjui kwamba watu wabaya hawataurithi Utawala wa Mungu? Msijidanganye! Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wafiraji au walawiti, wanyanganyi, wachoyo, walevi, wenye kusengenya, walaghai, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu (1Wakorinto 1:9)
PILI: Twajua kwamba Sheria ni njema, kama ikitumiwa ipasavyo. Lakini tunapaswa kukumbuka kwamba sheria haziwekwi kwa ajili ya watu wema, bali kwa ajili ya wahalifu na wasiotii, wasiomcha Mungu na wenye dhambi, watu wasio na dini na wa kidunia. Watu wanaowaua baba na mama zao, au wauaji wowote wale; sheria imewekwa kwa ajili ya waasherati, wafiraji, wanaowaiba watu, waongo, na wanaoapa uwongo au wanaofanya chochote ambacho ni kinyume cha mafundisho ya kweli. (1 Timoteo 1:8-10).
Msijesema kuwa hamjui kiswahili, hii hapa kwa kiingereza;
8 Now we know that the law is good, if one uses it legitimately. [SUP]9[/SUP]This means understanding that the law is laid down not for the innocent but for the lawless and disobedient, for the godless and sinful, for the unholy and profane, for those who kill their father or mother, for murderers, [SUP]10[/SUP]fornicators, sodomites, slave-traders, liars, perjurers, and whatever else is contrary to the sound teaching.(1 Timothy 1:8-10).
Kila mtu ana jukumu la kukeme hili suala kwa nguvu zote..
@Mr.Toyo, Nakubaliana na wewe kuwa uislam na ukristo unakataza ushoga kwa maana hiyo ni mungu anakataza ushoga. Kama ndivyo vipi wale wasio na dini au hawaamini kama mungu yupo (atheisits) wahukumiwe kwa dini ambazo haziwahusu? Pili, tunaambiwa kuwa kwa mungu kila jambo linawezekana, je ilikuwaje huyu mungu mwenye uwezo wa ajabu akaumba mashoga? uwezo wake ulikuwa likizo wakati mashoga wanazaliwa? Why didn't god stop the recreation process in the first place? Na kama basis ya argument ni maandiko yatokayo kwa mungu tumepata wapi mamlaka ya kuhukumu? (i.e biblia inakataza kuhukumu).
Lakini kuna hili, vitabu vya dini hizi mbili (Uislam &Ukristo) vinonekana kukataza ushoga. Ina maana ushoga umekuwepo tangu miaka hiyo (2000 yrs)? Kama ndivyo Tanzania mbona tunashtuka kama ndio kwanza tumeuskia kumbe ni mambo yako kwa miaka na miaka? Hivi ni kweli hakuna mashoga Tanzania? Na kuna sheria Tanzania inayokataza mtu kuwa ushoga? Ya ndoa ipo (watu wa jinsia tofauti i.e mke mume) lakini ni sheria ipi inayosema mtu haruhusiwi kuwa shoga?
Nimalizie, kuna mahali umenukuu maandiko ya biblia :"Watu wanaoishi maisha ya uasherati, wanaoabudu sanamu, wafiraji au walawiti, wanyanganyi, wachoyo, walevi, wenye kusengenya, walaghai, hao wote hawatashiriki Utawala wa Mungu" Nikiangalia hapa napata maswali mengi. Hivi wale wakwepaji wa EPA, 'walaghai wa Richmond watakuwa na hatia mbele ya mungu kwa kutumia hayo maandiko? Viongozi wetu serikalini (past & present) wanaweza kuwa wametenda/wanatenda moja ya hayo makosa? Sasa inakuwaje viongozi wa dini wanapiga makelele saaana kuhusu ushoga lakini wanapokea pesa za walaghai na wanyang'anyi? Ni mara ngapi tunaona kwenye TV maaskofu, masheikh wanapokea pesa toka kwa watu walioiba/wanaoiba hela za umma? Kuna exemption kwenye haya masharti ya kupata uzima wa milele?
Hivi inakuwaje mtu anayeiba hela zilizokusudiwa kulipia huduma za afya na hivyo kusababisha wagonjwa kulala chini na wengine kufa kwa kukosa dawa ananyamiziwa lakini mtu anayeingia chumbani kwake kwa hiari na kujifurahisha kwa namna atakavyo ndiye anayehukimiwa?double standard?
Mimi naona wanasiasa wanatupoteza kwa kukuza huu mjadala wa ushoga. Badala ya kujibu kwanini miaka 50 ya uhuru nchi yetu bado ni ombaomba wao wanataka wananchi wajadili nani anatumiaje viungo vyake vya mwili wake chumbani kwake!. Na ili ujue wanasiasa wetu ni wasanii, Malaysia ambayo inafuata misingi ya kiislam hawajasema lolote (Malaysia pia ni mwanacham wa jumuiya ya madola). Na Malaysia walipata uhuru toka kwa Waingereza hawa hawa around the same time na sisi. Utagundua hii kauli ya Cameron imewagusa zaidi Matonya kwa sababu wameambiwa kuanzia sasa huduma za vibakuli zitatolewa kwa vigezo na masharti, kama hutaki uko huru kupeleka bakuli lako unakojuwa.