Kupotea ghafla kwa Xi Jinping katika Duru za Kisiasa kunatufunza nini?

Ebu fuatilia ujue Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Kikomonisti Cha China (CCP) chenye wajumbe 24 na chenye mamlaka makubwa ya maamuzi ndani ya chama na ndani ya China kilichofanyika tarehe 30 Juni, 2025 chini ya Rais Xi Jinping kiliamua nini. Baada ya hapo tuletee habari.
 
Mzee labda unaizungumzia china ya tandale.
 
Propaganda tu hizi, Xi Jinping ndio mtu mwenye nguvu zaidi huko China hakuna wakumyumbisha.
 
Uwo ndio mtazamo wako wa ki magharibi

lkn China inatakiwa kukuwa kiuchumi sio kidemokrasia kama watakavyo Wazungu !!

CHINA inatakiwa iwe vile Xi anataka wajamaa tunataka

CHINA moja manake pia ni kauli moja sio midomo mingi ndio Hapana ndio Hapana iyo sio CHINA ilivojegwa tangu mwanzo ktk historia yake. Democratic tumewaachia wenyewe Wazungu.
 
Hakuna mwenye nguvu kumzidi Xijinping huko China kuanzia ndani ya Ccp mpaka jeshini......hivyo wa kumtingisha hayupo.
 
Wewe na akina nani wakati wewe mbongo na kuna Wachina hawamtaki Xi.

Xi hatodumu milele, kwahiyo akiondoka yeye basi China inakufa. Au kabla hajawa Rais China haikuwepo na haikuwa inakua kiuchumi?
 
Unatunga habari na kuconclude! Una shida kwenye kibeba nywele
 
China imerudije nyuma kisiasa?
Xi kachukua term ya tatu kuwa Chairman wa CCP. Jambo ambalo halikufanywa na watangulizi wake wawili Hu Jintao na Jiang Zemin, walishavuka uko utawala usio na kikomo.

Xi ana siasa za consolidation of power na power struggle. Anataka kuwa kama Mao kwenye wakati usio kama wa Mao.
 
Hakuna mwenye nguvu kumzidi Xijinping huko China kuanzia ndani ya Ccp mpaka jeshini
China haijawahi kuwa na Rais asiye na nguvu zaidi kwenye CCP au jeshini.
......hivyo wa kumtingisha hayupo.
Unakosea mkuu. Marais wakorofi wa China ndio walikuwa na wa kuwatingisha. Tafuta Mao Zedong kasalimika mara ngapi, pamoja na ukorofi wake na mkono wa chuma. Hata Deng alikuwa na upinzani. Na hao wawili Xi hawafikii wala kuwakaribia.
Kama hamna wa kumtingisha mbona anabambikia watu kesi na kufanya purges jeshini.

And btw si kwamba naungana na mtoa mada, mchango wangu unajitegemea kabisa. Yeye mambo yake anajua kayatoa wapi.
 
Ukimsikia mtu anakashifu ujamaa jua moja kwa moja mtu huyo uwezo wake kiakili ni mndogo mno ....na ukisikia mtu anakashifu ubepari huyo naye ni punguani ....nilisha eleza hapa kuwa ujamaa una sehemu yake na ubepari una sehemu yake ..kuna mifumo mi 4 tu nayo ni ..
1)SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIJAMAA
2)SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIBEPARI.
3)SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIBEPARI
4)SERIKALI YA KIBEPARI NA UMMA WA KIJAMAA.
Mfumo sahihi ni huo NO 2 Nyerere alijikwamisha kwa kufuata mfumo NO 1 ....Mwinyi yeye alikosea kwa kufuata mfumo NO3 ..Marais waliotumia mfumo NO 3 ni Kikwete Mkapa na sasa Samia, huu mfumo ni mbaya sana kwa sababu unageuza serikali kuwa mali ya kikundi kidogo kwa maslai yao binafsi ...NI MAGUFULI PEKEE ALIYE FUATA MFUMO SAHIHI NAO NI MFUMO NO 2 yaani SERIKALI YA KIJAMAA NA UMMA WA KIBEPARI..huu ndiyo mfumo sahihi sasa mtajua kwanini nimesema wanao kashifu ujamaa au ubepari wote hawana chembe ya akili hata kama ni baba au mama yako jua tu ni (wapumbavu) wacha leo niwa tag hawa mambumbumbu ya masjidi yaje yapate elimu kidogo adriz Malaria 2 Mufti kuku The Infinity FaizaFoxy Bwana Utam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…