Kupotea ghafla kwa Xi Jinping katika Duru za Kisiasa kunatufunza nini?

Kupotea ghafla kwa Xi Jinping katika Duru za Kisiasa kunatufunza nini?

Kiongozi wa china ana madaraka makubwa sana vipi ikitokea akayatumia vibaya au ikatokea akabadilika kama wa kwetu si itakuwa kisanga
Kuyatumia vibaya katika namna gani ? Japo sio rahisi na sio kwamba haiwezekani maana itapaswa awe na uwezo wa kulitawala vile atakavyo jeshi na awe na uwezo wa kukitawala chama vile atakavyo kwa kuanza na wale members 7 wa juu
 
Kuyatumia vibaya katika namna gani ? Japo sio rahisi na sio kwamba haiwezekani maana itapaswa awe na uwezo wa kulitawala vile atakavyo jeshi na awe na uwezo wa kukitawala chama vile atakavyo kwa kuanza na wale members 7 wa juu
Hujui kutumia madaraka vibaya
 
Wachina na Mungu wa wayahudi wapi na wapi, urusi Wakristo wanasali kama kawa, orthodox ndo dhehebu kubwa zaidi la wakristo pia Kuna waislam wengi tu mfano Jimbo la Chechnya . Habari za ufalme wa kusini sijui magharibi sijui hata kama wa wachina wanahangaika nao wao wako bize na uchina wao sisi watu weusi tuko bize na utamaduni na maandiko ya watu wengine, kutwa kucha kutafuta tafsri. Wao wanapiga hatua hawana habari na hivyo vitabu.
 
Karibu Masaki, Chole na Maneromango mkuu
Karibu Msanga -Sokoni, Ngongele, Bembeza na Mianzi Mkuu.Ila mpunga unatoka sana Marui, kihare na Kisangire kwa wasukuma maisha slope sana.Ndio maana Kila thread na comment tu hata kama sielewi 😀😀
 
Kumekuwa na taarifa zinazoendelea kuhusu mvurugano wa Uongozi wa Juu wa Chama cha Kikomunist cha China (CCP) Kiasi kwamba Rais Xi kwa mara ya kwanza ameshindwa kuhudhuria Mkutano wa BRICS huko Brazil. Taarifa zilizopo ni kuwa Xi amezuiliwa kutoka nje ya nchi kwani alikuwa ana mpango wa kutorokea Kazakhstan.

Itakumbukwa kuwa kuelekea ushindi wake kuendelea kuiongoza China Xi ili kujihakikishia anashika hatamu sawa sawa ya madaraka yake aliwaondoa viongozi wote aliowatilia mashaka ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu Li Keqiang. Xi akapanga team yake ya loyalists. Xi akajiaminisha kuwa yes sasa hakuna cha kunitisha.

Ikumbukwe kuwa kwa kumlinganisha Xi na mtangulizi wake Hu Jintao, Xi ni Mkomunisti kindakindaki wakati Hu yeye alikazia zaidi maendeleo ya kiuchumi badala ya ushabiki wa siasa za Kijamaa. Na wakati wa Hu Jintao ndipo China ilipiga maendeleo makubwa kiuchumi. Tujifunze nini na kinachoendelea China:

1. Viongozi chini ya Itikadi za Kijamaa/Kikomunist hujisahau na kufikiri Wao ni miungu watu

2. Mungu ni mwenye Wivu; pale mtu anapojifanya mungu mtu, yeye humuangalia tu (proverbs 14:12) wakati anasema aha sasa niko salama na anguko lake ndipo huja.

3. Nimeisha waambia tena na tena humu JF kuwa Biblia katika Daniel 11 inawatambulisha Wafalme Wawili. Mfalme wa Kusini (ktk zama zetu ni Ushirika wa USA & UK wakiungwa Mkono na washirika wao wa Mataifa ya magharibi) Mfalme wa Kaskazini (ambaye katika zama zetu ni Urusi pamoja na Washirika wake ambao ni China, Iran na N. Korea).

Biblia inamtambulisha USA/UK kuwa ndiyo World Super Power. Mfalme wa Kaskazini na Washirika wake wanataka kuchukua nafasi hiyo. Hata hivyo Biblia inatuhakikishia kuwa hawataweza. Na mbaya zaidi Mfalme wa Kaskazini sera zake zinapingana kabisa na malengo ya Mungu. Mfano Uhuru wa kuabudu. Tunaona Urusi China na N. Korea zinapinga utendaji wa Kikiristo.

Urusi wako na puppet Russian christian orthodox lakini inakandamiza utendaji wa makanisa mengine, mfano imewapiga marufuku kabisa mashahidi wa yehova ikiwatuhumu ati ni magaidi. Iran nayo inakandamiza uhuru wa kuabudu kwa wakristo.

4. Hivyo sitashangaa kuona mataifa haya yakamong'onyoka from within kama vile tuliona kwa SOVIET UNION na the Eastern Communist Block.

5. Tukumbuke tena kuwa MWAKA 2029, DUNIA ITAADHIMISHA MIAKA 2000 toka Yesu ametambulishwa Rasmi kuwa Yeye ndiyo Messiah. Kuelekea mwaka huo tutegemee kuona a lots of upheavals, zitakazotikisa Dunia; lakini hatimaje huenda kukawa na kipindi kifupi cha AMANI (amani ambayo ni fake)
Xi Jinping nilivyoona tu anaanza kukoromeana na United States nikajua huyu mwendo wake haumfikishi mbali. Marekani wanambinu nyingi za kukudhoofisha Moja wapo ni kukuchokesha kwanza.
 
Back
Top Bottom