Kupotea ghafla kwa Xi Jinping katika Duru za Kisiasa kunatufunza nini?

Xi si Rais wa maisha hakuna mambo za Rais wa maisha
"Rais wa maisha" ni kiongozi ambaye anatawala nchi au taasisi kwa kipindi cha maisha yake yote, bila ukomo wa muda wa uongozi. Mara nyingi, cheo hiki kinachukuliwa au kupewa kiongozi fulani kwa mamlaka makubwa ya kisiasa, na mara nyingine kwa njia zisizo za kidemokrasia.


Sifa kuu za "rais wa maisha":​


  1. Hachaguliwi tena mara kwa mara – anaendelea kuwa madarakani bila uchaguzi wa kumpinga.
  2. Mara nyingi hubadilisha katiba au sheria ili aendelee kutawala.
  3. Uongozi wake hauhitaji ridhaa ya wananchi tena baada ya kupewa mamlaka hayo.
  4. Wakati mwingine, hupewa cheo hicho kwa heshima, lakini katika hali nyingi ni kwa nguvu au ujanja wa kisiasa.

Mifano halisi ya kihistoria:​


  • Jean-Bédel Bokassa wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alijitangaza mfalme baada ya kuwa rais.
  • Kim Il-sung wa Korea Kaskazini alitangazwa kuwa "Rais wa Milele" hata baada ya kufariki.
  • Viongozi wengine kama
======================

Rais Xi Jinping kafuzu hivyo vigezo vya Rais wa maisha
 
Kwahiyo Hu Jintao alitawala mihula miwili sababu alikuwa Rais dhaifu?... kipindi cha Hu Jintao kilienda sambamba na ukuaji mkubwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia huko China
 
Tafsiri ya Rais wa maisha Xi hana kutokana na hii tafsiri uliyoweka hapa.

Siasa za China unafuatilia kwa kiasi gani ? Angalau hili swali litatoa mwangaza kuona kama Xi hana hiyo sifa kuitwa Rais wa maisha
 
Tafsiri ya Rais wa maisha Xi hana kutokana na hii tafsiri uliyoweka hapa.

Siasa za China unafuatilia kwa kiasi gani ? Angalau hili swali litatoa mwangaza kuona kama Xi hana hiyo sifa kuitwa Rais wa maisha
Kama huioni hiyo sifa ni sawa naheshimu maoni yako ila sikubaliana nayo
 
Kwahiyo Hu Jintao alitawala mihula miwili sababu alikuwa Rais dhaifu?... kipindi cha Hu Jintao kilienda sambamba na ukuaji mkubwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiteknolojia huko China
Na ndicho kipindi kilitokea scandal kubwa ya kisiasa katika nchi ya China iliyopita na maafisa wengi wa ranks za juu za siasa za China mfano rahisi ni Bo Xilai na ndio ulizaa big anti-corruption campaign ya Xi ndani ya chama,serikali na jeshi mpaka leo
 
Umesema vyema
 
Acha nikusaidie madaraka ya nguvu katika nchi za kikomunisti yapo ndani ya chama na cheo chenye madaraka makubwa ndani ya chama cha kikomunisti cha China ni cheo cha katibu mkuu na hiki cheo hakina ukomo wa utawala.

Cheo cha urais hakina mamlaka yoyote yale makubwa zaidi ya nembo ya uwakilishi.

Nguvu ya Xi ipo kwenye cheo cha ukatibu wake wa chama na uwenyekiti wa Central Millitary Commission hizi ndio position mbili zenye nguvu katika siasa za kikomunisti na katika nchi ya China maana hapa kuna husisha udhibiti wa chama na jeshi.

Kukusaidia tena katika siasa za kikomunisti unaweza kuwa nguvu kubwa na tishio bila hata kuwa na cheo chochote kikubwa officially katika nchi wala katika chama hata pia katika jeshi ila influence kubwa uliyonayo ya kiushawishi na kukubaliki katika haya maeneo mawili jeshi na chama inaweza kukufanya kuwa paramount leader wa nchi hii ndio nguvu iliyo mrudisha Deng Xiaoping kiutawala katika siasa za China baada kifo cha Mao na kukamatwa kwa gang of 4 na hata baada ya kurudi Deng hakuwa Rais wala katibu mkuu wa chama cha kikomunisti cha China ila ndie aliyekuwa kiongozi mwenye nguvu katika nchi ya China na paramount leader
 
Rais Xijinping kajilimbikizia mno madaraka kuliko Marais waliomtangulia
 
Thread na mleta thread ni wapumbavu promax
 
Acha nikusaidie madaraka ya nguvu katika nchi za kikomunisti yapo ndani ya chama na cheo chenye madaraka makubwa ndani ya chama cha kikomunisti cha China ni cheo cha katibu mkuu na hiki cheo hakina ukomo wa utawala.
Sahihi
 
Rais Xijinping kajilimbikizia mno madaraka kuliko Marais waliomtangulia
Nitajie hayo madaraka aliojilimbikizia kuliko wengine ?

Unajua how powerful Deng Xiaoping alikuwa bila kuhodhi position yoyote katika zile tatu katika siasa za China ? Au unajua how Mao alikuwa powerful kiasi gani ? Au Xi mnamzungumzia zaidi sasa kwa sababu usambaaji wa taarifa ni mkubwa kwa sasa na mtu yoyote anaweza kuandika chochote anacho jisikia hata asicho kifahamu
 
China hawana mambo ya Bible, iwe Xi, Hu or any leader

Lakini wachungaji wetu matapeli wanapiga codes hapo, wakiunganisha na vocals kidogo tu unakuta wanatoa single Madhabahuni
 
Kuna habari zinasema ameanza kufanya ugatuzi wa madaraka naona kaanza kuchoka kwa majukumu mengi aliyojipa huenda pia akaondoka mwaka 2027.

 
Unaokoteza vijarida uchwara unaleta kwenye mambo serious 🤣🤣🤣​
 
Kuzielewe siasa za China inapaswa kutenga muda na kuzifuatilia ila ukitaka kujifunza siasa za China kwa kuokoteza tu habari na vijihabari vinavyo chapishwa lazima utaishi kwa speculations mara Xi hivi mara Xi vile
 
Kiongozi wa china ana madaraka makubwa sana vipi ikitokea akayatumia vibaya au ikatokea akabadilika kama wa kwetu si itakuwa kisanga
 
Unajua kwa nn marekani na washirika wake na wewe mtoa mada mnafeli siku hizi?...watu siku hizi wamebadirika wanasoma makala zenu wanatafakari wanaona ujinga wanaachana na nyinyi Acha ujinga dogo sijui bro!!..kuwa na akili japo kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…