Kupotea kwa Humphrey Polepole kumefanya hata walio CCM wajione wao sio lolote wala chochote. Ni onyo ma kitisho

Kupotea kwa Humphrey Polepole kumefanya hata walio CCM wajione wao sio lolote wala chochote. Ni onyo ma kitisho

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
Hamjambo!

Moja ya athari za kupotea kwa Humphrey Polepole ni kuwadogodesha hata wale waliowahi kufikiri ni wakubwa ndani ya CCM iwe kwa nafasi walizowahi kuzishika au wanazozishika hivi sasa.

Ni wanaccm wachache sana waliowahi na watakaowahi kufika level ya kisiasa aliyofika Humphrey Polepole. Wachache sana.

Hata wale wanaojifikiria kwamba wanalolote sasa wana mashaka. Wanakaa kitaalamu.
Ile unanijua mimi ni nani haina nguvu tena.

Kwa sababu asilimia 90% ya wanaoweza kusema unanijua mimi ni nani hawatakuja wafike level ya Humphrey Polepole.

Kupotea kwake haiathiri upinzani. Lakini inaathiri waliondani ya CCM yenyewe kwamba.
Wewe huna lolote. Sio chochote sio lolote.

Unaweza ukapotea au kupotezwa leo hii na nchi ikaendelea bila tabu yoyote.

Hii imetoa nafasi kwa pekee kwa walioccm kuwa na hofu na kujua mipaka yao. Kwamba hawapo huru kwa kiwango wanachofikiri wanacho.
Na sio wakubwa kama wanavyojidanganya ni Wakubwa

Ukubwa wa mtu haupo kwenye chama alichopo, au cheo alichonacho.
Ukubwa wa mtu upo kwenye imani aliyonayo, msimamo, na uadilifu.

Wahalifu na waovu kisaikolojia hawatambui ukubwa wa cheo au chama au pesa ulizonazo.
Wahalifu au watenda ubaya wanaheshimu zaidi watu waadilifu, wenye imani ya utu na haki, na wenye msimamo.

Wahalifu na watenda mabaya hawatamuogopa mtu kwa cheo chake, fedha zake, au chama alichopo. Wahuni saikolojia yao haifanyi kazi hivyo.

Wahuni wanahofu pale wanapogundua kwamba wanaenda kumfanyia ubaya mtu mwadilifu. Hii huwaumiza sana. Na hata wakifanya huwapa mgogoro wa kinafsi.

Kwa sababu wahuni hata kama ni wabaya lakini mioyoni pia wanaule moyo wa utu.
Na siku zote UTU hauwaweki watu kwa madaraja ya cheo, utajiri na vyama. Bali huwaweka watu katika Wema na ubaya.

Siku zote wahuni hawalipwi na hawagharamiki kulipa pale wanapotendea ubaya watu wasiowaadilifu. Ila hulipwa mabaya wanapotendea watu Wema na waadilifu ubaya

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Week iliyopita Nimechukua Video zote za Polepole You tube zaidi ya video 15 nimejaribu Kumfuatilia kila Sentensi yake.

Mtu amekuwa Balozi wa CUBA.
mtu amekuwa Mbunge.
Amekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

Amevamiwa.
Ametekwa.
Amepotea.
SISIEMU MAPUMBAVU YOTE NA MANAFIKI YAMESHINDWA KUMTAFUTA MWENZAO.

HAKUNA ALIYE SALAMA HII NCHI.
 
Kupotea kwa Polepole naweza kusema ndo kumechangia kwa 90% yale ya October 29 naweza kusema ndo yananchochea 7//7 mpasuko uliopo ndani ya CCM sio wa mchezo level aliyokua amefeikia Polepole na kupotea hakuwezi kuacha chama Salama Kama unazani Yale maandamano ya October 29 yaliratibiwa na wananchi pole sana
 
Kile kilikuwa ni kitisho Mkuu.
Hakuna CCM ambaye angethubutu kuvaa kidete kujua alipo Polepole ilhali anajua ataonekana mshirika.

Alafu kingine,
Ukishakuwa mtu wa imani kali, msimamo na muadilifu sana ni ngumu sana hao CCM kukutilia maanani sana.
Swali linakuja ni wangapi huko CCM ni waadilifu kwa kiwango cha kuweza kujitoa mhanga ili wahuni waone mzungumzaji ana moral authority ya kuzungumza
 
Yale maandamano yalianza kuratibiwa kabla hata ya kupotea Polepole. So kusema MO29 imechangiwa kwa asilimia 90% na kupotea kwa Polepole kimahesabu hainipi majibu.

Kwanza kitendo cha kupotea kwake kabla ya hiyo tarehe kulihafifisha kwa kiasi fulani vuguvugu la MO29.
Hata kama alikuwa na washirika ndani ya ccm baada ya yeye kupotea lazima wangerudi nyuma na wangeghairi mpango wa kujitokeza.

Kimsingi, kimedani kupotea kwa Polepole iliwapa nguvu zaidi upandw wa pili na ni kitisho kwa waliondani ya ccm kwamba wasithubutu
 
Jana Nimeandika Sehemu nikasema Watanganyika wote Tumetekwa Nyara na Wahuni wachache Ndani ya CCM. WOTE

Kilichobaki ni Kupotezwa na Kuuwawa.

HAKUNA ALIYE SALAMA TENA KWENYE TAIFA ALILILOLIPAMBANIA MWALIMU JK NYERERE.

Watu wasiojihusisha na siasa wala kuzifikiria wao mara nyingi hujiona wapo Safezone
 
Kile kilikuwa ni kitisho Mkuu.
Hakuna CCM ambaye angethubutu kuvaa kidete kujua alipo Polepole ilhali anajua ataonekana mshirika.

Alafu kingine,
Ukishakuwa mtu wa imani kali, msimamo na muadilifu sana ni ngumu sana hao CCM kukutilia maanani sana.
Swali linakuja ni wangapi huko CCM ni waadilifu kwa kiwango cha kuweza kujitoa mhanga ili wahuni waone mzungumzaji ana moral authority ya kuzungumza
Joseph Sinde Warioba
 
Wahalifu wabobezi huwa hawana dhamira ya kuwawezesha kutofautisha mtu mwema na mtu mwadilifu. Kwa kifupi mhalifu halisi hana utu.

Sio hawana dhamira, ila wanapuuza ile dhamira ya kujua huyu ni mwema au mbaya.

Unafikiri wanajeshi wa Marekani au Israel wakipiga Palestina hawajui kwamba wanachofanya ni halali au haramu?

Binadamu sio Robots wanajua kabisa.
 
Yale maandamano yalianza kuratibiwa kabla hata ya kupotea Polepole. So kusema MO29 imechangiwa kwa asilimia 90% na kupotea kwa Polepole kimahesabu hainipi majibu.

Kwanza kitendo cha kupotea kwake kabla ya hiyo tarehe kulihafifisha kwa kiasi fulani vuguvugu la MO29.
Hata kama alikuwa na washirika ndani ya ccm baada ya yeye kupotea lazima wangerudi nyuma na wangeghairi mpango wa kujitokeza.

Kimsingi, kimedani kupotea kwa Polepole iliwapa nguvu zaidi upandw wa pili na ni kitisho kwa waliondani ya ccm kwamba wasithubutu
Ni mtazamo na mawazo yako lakini suala la kupotea kwa Polepole lilichangia kwa asilimia 90 October 29
 
Kwanini walimweka under house arrest?
CCM wanaogopa UKWELI na UWAZI bila kujali nani anasema.
Sasa kwa mtu mwenye NYADHIFA ya Warioba akiongea madudu ya CCM, hawaogopi? You know the answer!
.
Wanaogopa Ukweli kama ulivyosema. Ila hawamuogopi Warioba.
Warioba hajaanza kuongea leo. Warioba ameshazeeka haongei vitu kujijenga au kujikuza kisiasa.
Hii ni tofauti na waliochini yake
 
Back
Top Bottom