Hamjambo!
Moja ya athari za kupotea kwa Humphrey Polepole ni kuwadogodesha hata wale waliowahi kufikiri ni wakubwa ndani ya CCM iwe kwa nafasi walizowahi kuzishika au wanazozishika hivi sasa.
Ni wanaccm wachache sana waliowahi na watakaowahi kufika level ya kisiasa aliyofika Humphrey Polepole. Wachache sana.
Hata wale wanaojifikiria kwamba wanalolote sasa wana mashaka. Wanakaa kitaalamu.
Ile unanijua mimi ni nani haina nguvu tena.
Kwa sababu asilimia 90% ya wanaoweza kusema unanijua mimi ni nani hawatakuja wafike level ya Humphrey Polepole.
Kupotea kwake haiathiri upinzani. Lakini inaathiri waliondani ya CCM yenyewe kwamba.
Wewe huna lolote. Sio chochote sio lolote.
Unaweza ukapotea au kupotezwa leo hii na nchi ikaendelea bila tabu yoyote.
Hii imetoa nafasi kwa pekee kwa walioccm kuwa na hofu na kujua mipaka yao. Kwamba hawapo huru kwa kiwango wanachofikiri wanacho.
Na sio wakubwa kama wanavyojidanganya ni Wakubwa
Ukubwa wa mtu haupo kwenye chama alichopo, au cheo alichonacho.
Ukubwa wa mtu upo kwenye imani aliyonayo, msimamo, na uadilifu.
Wahalifu na waovu kisaikolojia hawatambui ukubwa wa cheo au chama au pesa ulizonazo.
Wahalifu au watenda ubaya wanaheshimu zaidi watu waadilifu, wenye imani ya utu na haki, na wenye msimamo.
Wahalifu na watenda mabaya hawatamuogopa mtu kwa cheo chake, fedha zake, au chama alichopo. Wahuni saikolojia yao haifanyi kazi hivyo.
Wahuni wanahofu pale wanapogundua kwamba wanaenda kumfanyia ubaya mtu mwadilifu. Hii huwaumiza sana. Na hata wakifanya huwapa mgogoro wa kinafsi.
Kwa sababu wahuni hata kama ni wabaya lakini mioyoni pia wanaule moyo wa utu.
Na siku zote UTU hauwaweki watu kwa madaraja ya cheo, utajiri na vyama. Bali huwaweka watu katika Wema na ubaya.
Siku zote wahuni hawalipwi na hawagharamiki kulipa pale wanapotendea ubaya watu wasiowaadilifu. Ila hulipwa mabaya wanapotendea watu Wema na waadilifu ubaya
Nimemaliza
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam