Kupotea kwa Humphrey Polepole kumefanya hata walio CCM wajione wao sio lolote wala chochote. Ni onyo ma kitisho

Kupotea kwa Humphrey Polepole kumefanya hata walio CCM wajione wao sio lolote wala chochote. Ni onyo ma kitisho

Hakika Tumekuwa wapumbavu sana
"Mwalimu Nyerere alituonya sana kwa Katiba Hii inamruhusu Rais kuwa Dikteta"

Kakikudi kadogo mno kametutawala watu wote kwa Kukosa Umoja na Usaliti tulionao.

HAKUNA ALIYE SALAMA WOTE TUMETEKWA BADO KUPOTEZWA TU.
 
Kupotea kwa Polepole naweza kusema ndo kumechangia kwa 90% yale ya October 29 naweza kusema ndo yananchochea 7//7 mpasuko uliopo ndani ya CCM sio wa mchezo level aliyokua amefeikia Polepole na kupotea hakuwezi kuacha chama Salama Kama unazani Yale maandamano ya October 29 yaliratibiwa na wananchi pole sana
Kama unazani Yale maandamano ya October 29 yaliratibiwa na wananchi pole sana
 
Ni mtazamo na mawazo yako lakini suala la kupotea kwa Polepole lilichangia kwa asilimia 90 October 29

Nipe hoja kwa namna ipi?

Ninavyojua, Polepole asingekamatwa, MO29 ingekuwa zaidi ya ilivyokuwa.

Kupotea kwake kulishusha morali ya wafuasi wake, iliwapa hofu viongozi ambao walikuwa na mpango au agenda za siri.

Kimedani lile lilikuwa pigo kwa timu ya MO29.

Sasa nipe hoja ili nione kwa namna ipi kupotea kwa Polepole kulichangia 90% ya MO29. Maana kimedani inakataa kwa upande wangu
 
Kwamba lilikuwa tukio la kutengeneza?

1. Kwamba Dola inahusika na kutengeneza tukio hilo?

2. Kwamba Walionyuma ya Polepole walitengeneza tukio hilo ili kumuondoa Polepole kwenye scripts na kuondoa au kupunguza tension ya yeye kutafutwa?
... muda wote alipokuwa anastream video mitandaoni alikuwa mafichoni, ... na akapotelea mafichoni ambako hatujui:
1) ... yupo hai na huru!
2) ... yupo hai mikononi mwa watekaji!
3) ... ameuwawa?
NI VIGUMU KUJUA!
 
.
Wanaogopa Ukweli kama ulivyosema. Ila hawamuogopi Warioba.
Warioba hajaanza kuongea leo. Warioba ameshazeeka haongei vitu kujijenga au kujikuza kisiasa.
Hii ni tofauti na waliochini yake
Hujajibu kwanini Warioba walimweka under house arrest after MO29 ikiwa hawamuogopi?
Kwanini anatishiwa maisha kila tu akitema cheche kwenye press ikiwa hawamuogopi?
 
Week iliyopita Nimechukua Video zote za Polepole You tube zaidi ya video 15 nimejaribu Kumfuatilia kila Sentensi yake.

Mtu amekuwa Balozi wa CUBA.
mtu amekuwa Mbunge.
Amekuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM

Amevamiwa.
Ametekwa.
Amepotea.
SISIEMU MAPUMBAVU YOTE NA MANAFIKI YAMESHINDWA KUMTAFUTA MWENZAO.

HAKUNA ALIYE SALAMA HII NCHI.
Ukisisikiliza zile video zote hakuna hata moja alipowahi kumtaja rafiki yake waliyekua karibu nae bega kwa bega kwa kile walichoita kukinyoosha chama kimaadili na kurudisha miiko ya CCM hapa namzungumzia Bashiru Ali.

Ulijiuliza kwa nini?
 
Hamjambo!

Moja ya athari za kupotea kwa Humphrey Polepole ni kuwadogodesha hata wale waliowahi kufikiri ni wakubwa ndani ya CCM iwe kwa nafasi walizowahi kuzishika au wanazozishika hivi sasa.

Ni wanaccm wachache sana waliowahi na watakaowahi kufika level ya kisiasa aliyofika Humphrey Polepole. Wachache sana.

Hata wale wanaojifikiria kwamba wanalolote sasa wana mashaka. Wanakaa kitaalamu.
Ile unanijua mimi ni nani haina nguvu tena.

Kwa sababu asilimia 90% ya wanaoweza kusema unanijua mimi ni nani hawatakuja wafike level ya Humphrey Polepole.

Kupotea kwake haiathiri upinzani. Lakini inaathiri waliondani ya CCM yenyewe kwamba.
Wewe huna lolote. Sio chochote sio lolote.

Unaweza ukapotea au kupotezwa leo hii na nchi ikaendelea bila tabu yoyote.

Hii imetoa nafasi kwa pekee kwa walioccm kuwa na hofu na kujua mipaka yao. Kwamba hawapo huru kwa kiwango wanachofikiri wanacho.
Na sio wakubwa kama wanavyojidanganya ni Wakubwa

Ukubwa wa mtu haupo kwenye chama alichopo, au cheo alichonacho.
Ukubwa wa mtu upo kwenye imani aliyonayo, msimamo, na uadilifu.

Wahalifu na waovu kisaikolojia hawatambui ukubwa wa cheo au chama au pesa ulizonazo.
Wahalifu au watenda ubaya wanaheshimu zaidi watu waadilifu, wenye imani ya utu na haki, na wenye msimamo.

Wahalifu na watenda mabaya hawatamuogopa mtu kwa cheo chake, fedha zake, au chama alichopo. Wahuni saikolojia yao haifanyi kazi hivyo.

Wahuni wanahofu pale wanapogundua kwamba wanaenda kumfanyia ubaya mtu mwadilifu. Hii huwaumiza sana. Na hata wakifanya huwapa mgogoro wa kinafsi.

Kwa sababu wahuni hata kama ni wabaya lakini mioyoni pia wanaule moyo wa utu.
Na siku zote UTU hauwaweki watu kwa madaraja ya cheo, utajiri na vyama. Bali huwaweka watu katika Wema na ubaya.

Siku zote wahuni hawalipwi na hawagharamiki kulipa pale wanapotendea ubaya watu wasiowaadilifu. Ila hulipwa mabaya wanapotendea watu Wema na waadilifu ubaya

Nimemaliza

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
kwani gentleman,
huyo muungwana alikua na nin so special hata kue na dhana potofu hizo kuhusu masuala ya siasa, ambayo kifalsafa yana kanuni mbili tu muhimu, yaani kua baridi au joto kali, na ukiwa viguvugu utatapukwa na yeyote yule kwenye medani.

sidhani kama kuna mtu katika siasa za Tanzania anaweza kuthubutu kusema ati huyo muungwana ni role model wake katika siasa. Kwasababu utaulizwa kwa lipi hasa la maana kwa mwanasiasa kigeugeu kama huyo muungwana?🐒
 
Ukisisikiliza zile video zote hakuna hata moja alipowahi kumtaja rafiki yake waliyekua karibu nae bega kwa bega kwa kile walichoita kukinyoosha chama kimaadili na kurudisha miiko ya CCM hapa namzungumzia Bashiru Ali.

Ulijiuliza kwa nini?
Tupe majibu
 
We ni Muhuni Gang?
kwani gentleman,
huyo muungwana alikua na nin so special hata kue na dhana potofu hizo kuhusu masuala ya siasa, ambayo kifalsafa yana kanuni mbili tu muhimu, yaani kua baridi au joto kali, na ukiwa viguvugu utatapukwa na yeyote yule kwenye medani.

sidhani kama kuna mtu katika siasa za Tanzania anaweza kuthubutu kusema ati huyo muungwana ni role model wake katika siasa. Kwasababu utaulizwa kwa lipi hasa la maana kwa mwanasiasa kigeugeu kama huyo muungwana?🐒
 
Kwanini walimweka under house arrest?
CCM wanaogopa UKWELI na UWAZI bila kujali nani anasema.
Sasa kwa mtu mwenye NYADHIFA ya Warioba akiongea madudu ya CCM, hawaogopi? You know the answer!
Ni kweli yuko under house arrest?
 
Back
Top Bottom