Mpinzire
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 7,503
- 13,463
Jana nilikuwa Club House usiku mpaka saa 00:58 huko! Nilikutana na taarifa ya Mwenyekiti wa umoja wa vijana NCCR Mageuzi kupetea katika mazingira yakutatanisha huko kwake Buguruni tangia tarehe January 24, 2023 usiku.
Kijana huyu ni mmoja wa wafuasi wa karibu wa Mh James Mbatia ambapo wameenguliwa pamoja na James Mbatia katika nafasi zao kwa mabavu ya Serikali kwa kushirikiana na wanachama wasio waaminifu ndani ya NCCR Mageuzi.
Kilichonishangaza ni ukimya wetu sie wananchi, vyombo vya habari, Social Media! Hakuna kitu wote tumemute togauti kabisa na mambo yalivyokawa katika awamu 5 ya Jiwe mtu usipomuona tu inakuwa issue!
Je! Ni kweli kuna uhuru wa habari na kujieleza kama tunavyoaminishwa? Au kwakuwa kwasasa wanatendewa wasio na sauti na ndiyo maana tumekuwa kimya? Au kwasasa kwakuwa tumepewa nafasi yakukaa meza kuu?
Edward Simbeye Mkuu wa Idara ya mawasiliano NCCR jana alieleza kwa mapana kuwa wamewasiliana na vyombo vya habari karibu vyote kuwapa hiyo taarifa, wameongea na wavyama vingine kama Chadema etc lakini kwakweli kinachoendelea mpaka sasa watu wako kimya!
Watanzania hatujaguswa na suala hili? Kwanini limepigiwa kimya kama lilivyopigiwa kimya kung'olewa kwa Mwenyekiti wao? Yangekuwa mambo haya yanafanyika katika chama chochote kipindi cha jiwe mngekaa kimya kama sasa? Tuamini kweli kuwa nyinyi ni wapigania haki za watu au wapigania maslahi yenu?