Kupotea taratibu kwa alama ya Kanisa Katoliki katika kupinga dhuluma

Pengo aliharibu sn RC
Pengo hayupo madarakani, na hata alipokuwapo alikuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo la dar es Salaam. Sasa aliliharibu vipi wakati hajawahi hata kuwa Rais wa TEC? Wakati mwingine watu hamjui muundo wa Kanisa, mmekariri tu yule mnayemtaka kumshambulia
 
Sasa kama anayetawaliwa kwa dhulma anaona sawa,kanisa lifanyeje sasa ndugu yangu? Wanaopaswa kusimama kwa dhati haswa ni wananchi
Inahitaji akili kubwa sana kukuelewa.
 
Kwa ufupi umekosea sana kuanzisha uzi kwa mfumo wa taarifa wakati haukufanya juhudi za kutafuta nyaraka za kanisa za hivi karibuni. Matokeo yake ni kwamba umegundua hilo lakini umeshawalisha watu hayo mawazo na hawataki kusoma link za nyaraka, wanataka waendeleze ulichoanzisha. Ni vyema tukaanzisha uzi kwa mfumo wa kuuliza, kama hatuna uhakika, kuliko kutumia mfumo wa taarifa

Kuhusu kufikisha ujumbe kwa waumini, Katiba ya Halmashauri ya Walei ni moja ya katiba nzuri kabisa. imefafanua jinsi mtiririko wa maagizo ya Hierakia kwenda kwa Walei ulivyo, na wajibu wa kila kiongozi katika viongozi watano, na inataja majukumu yao. Kuhusu kufikisha ujumbe unaohusu mambo ya kijamii/malimwengu, hii hapa chini ni sehemu ya katiba inapoitaja Kamati ya Haki na Amani:

 
Pengo hayupo madarakani, na hata alipokuwapo alikuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo la dar es Salaam. Sasa aliliharibu vipi wakati hajawahi hata kuwa Rais wa TEC? Wakati mwingine watu hamjui muundo wa Kanisa, mmekariri tu yule mnayemtaka kumshambulia
Yeye ndiyo alikuwa kiongozi Tz
 
Pengo hayupo madarakani, na hata alipokuwapo alikuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo la dar es Salaam. Sasa aliliharibu vipi wakati hajawahi hata kuwa Rais wa TEC? Wakati mwingine watu hamjui muundo wa Kanisa, mmekariri tu yule mnayemtaka kumshambulia
Yeye ndiyo alikuwa kiongozi Tz
 
Yeye ndiyo alikuwa kiongozi Tz
Sasa ndio unadhihirisha wazi kwamba wewe sio Mkatoliki, na kama ni Mkatoliki basi ni wale wasioshirikiana pamoja na wenzao jumuiyani, wanaosubiri Jumapili moja moja waende kanisani tena wakijisikia, wanaolalamika mitandaoni huku kumbe hawajui muundo wa Kanisa lao, wala hawajui majina ya viongozi wa kanisa lao, wala hawajui vyeo vyao, wala hawajui mipaka ya vyeo vya viongozi wao, isitoshe hawajui hata mipaka ya kimamlaka ya Familia, Jumuiya, Parokia, Jimbo na Taifa! Kazi yao ni kulalamika tu na kuwapakazia wenzao!
 
Mkuu pole kama una undugu na Pengo lakini ukweli lazima usemwe
 
Mkuu pole kama una undugu na Pengo lakini ukweli lazima usemwe
Labda nikuulize, Pengo ni nani kabla na baada ya kustaafu? nakuuliza kwa nia ya kukusaidia muundo ulivyo
 
Siamini kama nimekosea sana kama unavyodai.

Kuunena ukweli, kukemea maovu, kulinda haki, kupeleka ujumbe wa haki na amani, ni jukumu la kanisa la wakati wote katika jamii yenye dhuluma, tena inatakiwa kusemwa bila kukoma maana ni sehemu ya ibada.

Kutoa tu waraka, mara moja kwa mwaka au mara moja kwa miaka 5, tena bila ya kuwa na mkakati wenye kuleta matokea, ni mapungufu.

Unaamini kuwa waraka mmoja katikati ya dhuluma nyingi, tena waraka ambao hauna mkakati wa kuwafikia waumini wote, unatosha kutimiza wajibu wa kanisa katika kupeleka ujumbe wa kuiishi haki kwenye jamii yenye madhulumu mengi?

Katiba, miongozi na taratibu zinaweza kuwepo, lakini jambo la muhimu zaidi, ni kujiuliza kama hayo yote yanatimiza kilichokusudiwa? Ujumbe wa kupinga dhuluma ni lazima uwafikie wanaodhulumiwa, wanaodhulumu na wanaoshuhudia dhuluma hata kama wao hawadhulumiwi au hawadhulumu.
 
AMINA KUBWA mkuu
 
99.99999999999999999999999999999999999999999999999999999999999% ni zero kichwani
 
Kisa ana
Kanisa halifanyi kazi utakavyo wewe
Ila linataka sadaka nichumayo Mimi.
 
Kanisa Katoliki lina taratibu zake. Nyaraka huwa zinatolewa kwa kalenda au kwa tukio mahususi. Waraka wa Kwaresma hutolewa kila mwaka na hubeba ujumbe wa Kanisa ulimwenguni na kuhusisha na matukio ya Kanisa mahalia. Lakini pia kuna wakati hutolewa waraka kwa jambo mahususi bila kujali kalenda, kama vile maelekezo kuhusu tahadhari dhidi ya Covd19 ambapo nyaraka kadhaa zilishatolewa

Kwa hiyo si sahihi kusema waraka unatolewa mara moja kwa miaka 5, maana kwaresma ipo kila mwaka na ujumbe wake kwa mfumo wa waraka hutolewa pia kila mwaka. Watu ni wavivu kufuatilia na kusoma

Lakini pia si busara kutoa nyaraka za jambo hilo hilo kila mara, sasa RC itakuwa kama Gwajima anayeongelea chanjo kila mara katika mahubiri, maana hiyo sasa itatafsiriwa na kupokelewa kwa mtazamo tofauti
 
Kuonya kivipi maana sio sisiemu pekee ndio wachafu?

Nafikiri Ukiyasikiliza vizuri mahubiri ni maonyo tosha sasa zaidi ya hapo itakuwa kiongozi wa dini umeingia kwenye siasa moja kwa moja ....
Ila kusifia watawala siyo kuingia kwenye siasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…