Kupotea taratibu kwa alama ya Kanisa Katoliki katika kupinga dhuluma

...Tunakumbuka kwamba matokeo mojawapo ni kutimuliwa kwa Katibu Mkuu wa TEC wakati huo, Raymond Sabas, na kutangazwa siyo raia.
Alitimuliwa na nani, na kanisa au serikali?
 
Alitimuliwa na nani, na kanisa au serikali?
Serikali, ila naamini Pengo alimtoa kafara. Sikusikia Kanisa likihangaika juu yake. Wala Askofu NiweMugizi hakupata utetezi wowote. Ni pale Magu alipogundua kwamba kama anafariki, atazikwa na NiweMugizi. Hapo ndio akaachia paspoti yake, siku za mwisho
 
Kumbuka wanashule na hospital sikuizi hawatoi huduma wanafanya biashara
 
Hakuna anayelitaka Kanisa Katoliki libebe majukumu ya mtu mmoja mmoja, taasisi za kiraia za kupigania haki au vyama vya siasa. Lakini kutowajibika kwa mtu mmoja mmoja au vyama vya siasa au taasisi nyingine, hakuhalalishi kwa Kanisa Katoliki kutofanya yaliyo sehemu ya wajibu wake kwa kuzingatia nafasi yake kwa sisi waumini wake, hata kama ingekiwa ni nchi ya chama kimoja au nchi isiyo na chama chochote cha siasa.
 
Jamani wanasiasa pambaneni tu kwa nguvu za wanasiasa,tatizo siasa inausaliti mkubwa sana,viongozi wa dini wanaweza kusimama lakini mwisho wa siku haohao ambao wanaoneka kuonewa,wakipata madaraka wanasau au kubadirika kabisa.
 
Haya malalamiko yenu nimekuja kugundua wale wote wa aina yako mnakiri ukuu wa Kanisa Katoliki ndio maana wote bila kujali madhehebu au dini zenu hamuishi kulipelekea lawama, ni kama vile inavyokuwa kwa baba na watoto nyumbani.

Kule juu nimekusoma unakiri mahali ulikuwa huujui au hujawahi kuuona waraka wa Kanisa Katoliki wa Kwaresma uliotolewa enzi za mwendazake na kuzua sintofahamu mpaka baadhi ya mapadri wakaitwa sio watanzania, lakini pamoja na hayo, bado unalia tu unataka zaidi, sasa nikuulize, kabla hujapewa hiyo zaidi wewe na wenzio mmechangia nini kuondoa hali iliyopo?
 
Yawezekana mchango wangu ukawa mdogo, lakini kwa nafasi yangu kama mtu mmoja na siyo taasisi, naridhika kuwa nimetimiza wajibu wangu;

1) Sijawahi kuuza utu wangu, licha ya vishawishi vingi vya kupewa cheo, na nitasimama hivyo daima.

2) Sijawahi kukosa kuwa mkweki wa nafsi yangu katika mambo ninayoyaamini ni sahihi au siyo sahihi.

3) Mara kadhaa nimetoa kile nilicho nacho kuwagharamia wale wanaoteswa na watawala pasipo haki.

4) Sijawahi kuunga mkono ugandamizaji wa aina yoyote dhidi ya yeyote kwa kauli au matendo.

Zaidi ya hapo, unahitaji nguvu za taasisi, vinginevyo utapotezwa na wala isijulikane kama ulikuwa ukitetea chochote.

Kanisa Katoliki ni taasisi kubwa, imara na yenye nguvu Duniani. Ni kweli kuna waraka uliwahi kutolewa dhidi ya utawala kuhusiana na uonezi. Lakini hata kauli ile ilikosa nguvu kutokana na mgawanyiko miongoni mwa viongozi wa Kanisa. Hata wale mapadre na Askofu walioanza kuandamwa na dola kulitokana na mgawanyiko ndani ya Kanisa lenyewe lakini Kanisa Katoliki lisingeweza kupuuzwa kama kusingekuwa na mgawanyiko, na wala wale mapadre na Askofu wasingeweza kuzongwa na Serikali kama ilivyotokea.

Kuna dalili ya taasisi hii kukosa mwelekeo thabiti. Kanisa Katoliki linalojulikana kwa nidhamu, inawezekanaje baada ya kauli ya TEC, Askofu Mkuu mmoja anatoka na kusema, mimi siyo sehemu ya hiyo kauli ya Kanisa???
 
Hakuna kanisa siku hizi. Kila mtu anaangalia Tumbo lake tu.
 
Sasa kama anayetawaliwa kwa dhulma anaona sawa,kanisa lifanyeje sasa ndugu yangu? Wanaopaswa kusimama kwa dhati haswa ni wananchi
you nailed it.. ila Inamaana kanisa halijui ujinga wa watawaliwa hata liamue kunyamaza bila kukemea watawala? najua, linajua.
kanisa linajua kuwa watawaliwa wanatatizo la kiakili hivyo lilipaswa kutukingia kifua. si sahihi kanisa kukaa kimya ukulinajua kuwa watawala wanatake advantages kupitia weakness yetu(watawaliwa) kufanya hivyo ni namna ya kubariki udhalimu wa watawala.

the only thing necessary for the triumph of evil is for good men to do nothing
 
Unaposema hujawahi kuuza utu wako licha ya vishawishi vingi vya kupewa cheo huku ukiwa na fake id, hakuna anayekujua, hii kwangu ni kujikweza tu, hebu andika hoja zenye mantiki hapa.

Unaposema hujawahi kuunga mkono ukandamizaji kwa wengine unamaanisha Kanisa Katoliki ndio linaunga mkono? na huo waraka wa Katoliki kukemea utawala uliopita hukuuona? au ndio umeuona ila umeutafutia sababu ya kitoto kisa ulipingwa na Askofu mmoja ndio unaukataa?

Habari ya msimamo wa Kanisa na kutaka kila mmoja aukubali ili wakufurahishe wewe nayo kwangu hata siielewi mantiki yako, naamini Kanisa halifanyii kazi maoni yako binafsi, linafanyia kazi kero zinazoikumba jamii kwa ujumla.

Mwisho, kama mapadri wengi walitoa msimamo wa kuandaa waraka na ukatolewa hiyo kwangu inatosha, inakwenda na dhana ya wengi wape, lakini wewe mwenzangu, unamtumia huyo mmoja alieukataa waraka kama kigezo cha kupinga msimamo wa Kanisa Katoliki ili kuhalalisha madai ya uzi wako, hii judgement yako kwangu naiona ya kitoto.

Huu uzi wako in real sense hauna mantiki, unaulazimisha tu uendelee kuwepo hapa kwa hoja zako za kibinafsi, unatafuta "vijisababu" kupinga mambo ya msingi yanayofanywa na Kanisa Katoliki, nikiamini fika wakati unaanzisha huu uzi, hata Waraka wa Kwaresma wa Kanisa Katoliki ulikuwa hujui kama upo, umeujulia hapa.
 
Waraka wa Kwaresma niliuona na ninaufahamu. Nilidhani kuna mwingine zaidi ya ule ambao mmoja wa maaskofu wakuu aliukataa.

Unaweza kufanya judgement zako kama upendavyo. Unaweza kujiaminisha kuwa hoja nyingine zote ni za kitoto ila za kwako tu ni za kiutuuzima. Amini hivyo ili upate faraja ya moyo.

Lakini ninkosa kuamini hovyo maana yumkini unaweza kuwa unambeza mtu anayekuzidi uelewa wa kinachojadiliwa.

Bado nasisitiza, kwa TEC kumchagua kiongozi wao kwa kuangalia nani ana ukaribu na mtawala, ni kosa kubwa katika haki.

"Kanisa kuanzia sasa lisimame na watu wanaodhulumiwa badala ya kusimama na watawala. Kanisa liwe mdomo wa kuwasemea wasio na uwezo wa kusema", Pope Francis.

Waraka ni kauli njema ya Kanisa. Lakini mahali penye dhuluma, halistahili kuacha kuendelea kukemea kama dhuluma bado inaishi. Labda kama Kanisa limeridhika kuwa sasa dhuluma dhidi ya wasio na sauti imeisha.

Mambo ya fake id, na sijui kujikweza, hayana maana. Hujalazimishwa kuamini. Na kwa vile ni fake ID, na wala huwezi kuamini, basi hukustahili kuuliza maana jibu lolote la yale niliyowahi kufanya, hitaamini. Na kwako itakuwa ni kujikweza au kujidunisha.
 
Jamani wanasiasa pambaneni tu kwa nguvu za wanasiasa,tatizo siasa inausaliti mkubwa sana,viongozi wa dini wanaweza kusimama lakini mwisho wa siku haohao ambao wanaoneka kuonewa,wakipata madaraka wanasau au kubadirika kabisa.
Tunachohitaji ni Katiba ambayo itawezesha serikali iliyoko madarakani iwajibike kwa wananchi, kama sivyo wananchi wawe na uwezo wa kuiondoa madarakani. Katiba Mpya. Kwa hiyo hata CHADEMA wakiingia madarakani, watawajibika kwa Katiba hiyo
 
Muongo mkubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…