Kupuuza maoni ya Wananchi Mtandaoni: Hatua ndogo inayoweza kuigharimu Taifa kubwa

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyochapishwa Julai 2025 inaonyesha kuwa idadi ya watumiaji wa intaneti nchini imefikia milioni 54 kufikia robo ya nne ya Mwaka wa Fedha 2024/2025, hilo ni ongezeko kubwa kutoka milioni 29, Mwaka 2020.

Katika kipindi cha miaka minne hiyo, Tanzania imeendelea kushuhudia ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti, unaochochewa na upanuzi wa huduma za mtandao kupitia simu za mkononi, kupungua kwa bei ya vifaa vya mawasiliano kama simu janja, pamoja na ongezeko la uelewa wa fursa za kidijitali miongoni mwa wananchi.

Kwa sasa, zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia huduma za intaneti — hatua inayoiweka nchi kwenye mkondo wa kujenga uchumi wa kisasa wa kidijitali na shindani, sambamba na kukuza sekta nyingine muhimu za maendeleo.

Huduma za intaneti zimekuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya sekta mbalimbali kama biashara, elimu, afya, fedha, kilimo, na utawala bora. Majukwaa ya kidijitali yameibuka kuwa njia rahisi na za haraka za kufanya biashara, kuwasiliana, kujifunza, na kupata huduma muhimu kwa ufanisi zaidi.

Wimbi la Kupuuzia Maoni ya Wananchi Mtandaoni
Pamoja na mafanikio haya, bado kumekuwapo na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa taasisi za umma kupuuzia watumiaji wa mitandao ya kijamii — hasa pale wananchi wanapotumia majukwaa hayo kutoa hoja za kisiasa au kiutawala kwa mlengo wa kukosoa.

Baadhi ya viongozi wamekuwa wakisikika wakitaka jamii na mamlaka kupuuzia hoja zinazoibuliwa mtandaoni, huku wengine wakidai kwamba wachangiaji wanaokosoa au kupinga ni watu wasio raia wa Tanzania, au waliokimbilia ughaibuni. Swali ni, je, hoja hizi zina mantiki kweli?

Wimbi la Taasisi, Viongozi wa Umma Kufunga Sehemu za Maoni (Comment Section)
Propaganda hii imewafanya baadhi ya viongozi na taasisi za umma kufunga sehemu ya maoni wanapochapisha taarifa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii. Matokeo yake, wananchi wanashindwa kutoa maoni hata katika masuala ya kawaida yasiyo na mivutano ya kisiasa.

Hali hii inaibua wasiwasi kuhusu namna viongozi wanavyoyapokea mabadiliko ya kidijitali Duniani, wakati ambapo shughuli nyingi sasa zinategemea intaneti. Kabla ya kuwalaumu wananchi ambao ndio walaji na wachangiaji wakuu wa maudhui tunapaswa kujiuliza: Je, viongozi wetu wanaelewa vema nafasi ya intaneti katika jamii ya leo? Wengi wao wanaonekana kutaka kuitumia mitandao kwa ajili ya kutuma taarifa pekee , siyo kupokea mrejesho au maoni.

Aliyewahi kuwa Balozi wa Cuba na Msemaji wa CCM, Humphrey Polepole aliwahi kukemea tabia ya viongozi wanaopuuza ujumbe katika majukwaa ya mawasiliano kama WhatsApp, akifananisha tabia hiyo na "uhuni" kwa kiongozi wa umma. Alikosoa vikali mtindo wa Viongozi kuondoa kipengele cha 'blue tick" kwenye WhatsApp zao wanapotumiwa ujumbe na wananchi.

Tuliharakisha Kutunga Sheria Kali, Tukasahau Kujielimisha
Kadiri Ulimwengu wa Kidijitali ulivyokuwa ukikua na kuonekana kama tishio kwa watawala katika mataifa makubwa, mamlaka zetu zilikimbilia kutunga Sheria na Kanuni kali kuhusu matumizi ya intaneti, tukiamini huo ndio njia bora ya kujilinda.

Hata hivyo, katika harakati hizo tulisahau kujielimisha na kuelimishana kuhusu matumizi sahihi na rafiki ya mtandao. Ilitarajiwa kwamba shule zingekuwa na vilabu vya uelewa wa matumizi salama ya intaneti, lakini hadi leo bado tumejikita zaidi kwenye sheria na udhibiti, badala ya elimu na uhamasishaji.

TCRA ipo bize kuthibiti, lakini unajiuliza ni tija zipi zimepatikana baada ya kuundwa kwa Wizara ya Teknolojia ya habari? nadhani hii ni Wizara muhimu sana kwa Serikali katika kuratibu suala la uelewa kwa viongozi umma pamoja na wananchi.

Ni muhimu kutambua kuwa kwa sasa, mtandao wa intaneti ndio uwanja uliosalia kwa watu kupashana habari na kujadili mambo ya kijamii. Matumizi ya redio na magazeti yanapungua kila siku, hivyo kupuuzia mitandao ni sawa na kujipotosha au kujikaanga wenyewe.

Nguvu ya Mtandao Haiwezi Kupuzwa
Tumeshuhudia nyakati ambazo Polepole, Gwajima au baadhi ya Watu wengine wanapozungumza masuala ambayo wananchi wamekuwa wakiyapigia kelele walipotoa matamko, wananchi walijaa mtandaoni kufuatilia mubashara kujadili. Itashangaza kama hata hilo halikutoa picha ya kwamba jamii inakui ya jambo fulani badala yake ikaaminika kuwa hao ni "roboti".

Wakati wa wiki ya uchaguzi, tuliona intaneti ikizimwa katika baadhi ya maeneo. Swali ni, je, hali ingekuwaje kama isingezimwa? majibu ya swali hili yanatosha kuwa ujumbe kwa ambao wanaendelea kushupaza vichwa wakipuuza umuhimu na nafasi ya internet katika Dunia ya leo.

Hitimisho
Ni vyema kujenga utamaduni wa kuchukulia kwa uzito maoni ya wananchi yanayotolewa mtandaoni, kwani huko ndiko kunakosikika sauti za watu wengi kwa uwazi.

Kama taifa, tukikumbatia utamaduni huu, tunaweza kuepusha migogoro, vurugu, na matukio ya kusikitisha kama yale yaliyoshuhudiwa na kusimiliwa katika vipindi vya uchaguzi. Mitandao ya kijamii si adui wa serikali, bali ni kioo cha jamii kinachoonesha hisia, matarajio, na changamoto za wananchi.
 
Ngoja mitandao ya kijamii ije na sera acc ya watu wakubwa iwe ni marufuku kufunga coments section hasa za umma na public figure mbona kitaumana
 
Ripoti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) iliyochapishwa Julai 2025 inaonyesha kuwa idadi ya watumiaji wa intaneti nchini imefikia milioni 54 kufikia robo ya nne ya mwaka wa fedha 2024/2025 , hilo ni ongezeko kubwa kutoka milioni 29 mwaka 2020.

Katika kipindi cha miaka minne hiyo, Tanzania imeendelea kushuhudia ukuaji mkubwa wa matumizi ya intaneti, unaochochewa na upanuzi wa huduma za mtandao kupitia simu za mkononi, kupungua kwa bei ya vifaa vya mawasiliano kama simu janja, pamoja na ongezeko la uelewa wa fursa za kidijitali miongoni mwa wananchi.

Kwa sasa, zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanatumia huduma za intaneti — hatua inayoiweka nchi kwenye mkondo wa kujenga uchumi wa kisasa wa kidijitali na shindani, sambamba na kukuza sekta nyingine muhimu za maendeleo.

Huduma za intaneti zimekuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya sekta mbalimbali kama biashara, elimu, afya, fedha, kilimo, na utawala bora. Majukwaa ya kidijitali yameibuka kuwa njia rahisi na za haraka za kufanya biashara, kuwasiliana, kujifunza, na kupata huduma muhimu kwa ufanisi zaidi.

Wimbi la Kupuuzia Maoni ya Wananchi Mtandaoni
Pamoja na mafanikio haya, bado kumekuwapo na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa taasisi za umma kupuuzia watumiaji wa mitandao ya kijamii — hasa pale wananchi wanapotumia majukwaa hayo kutoa hoja za kisiasa au kiutawala kwa mlengo wa kukosoa.

Baadhi ya viongozi wamekuwa wakisikika wakitaka jamii na mamlaka kupuuzia hoja zinazoibuliwa mtandaoni, huku wengine wakidai kwamba wachangiaji wanaokosoa au kupinga ni watu wasio raia wa Tanzania, au waliokimbilia ughaibuni. Swali ni, je, hoja hizi zina mantiki kweli?

Wimbi la Taasisi, Viongozi wa Umma Kufunga Sehemu za Maoni (Comment Section)
Propaganda hii imewafanya baadhi ya viongozi na taasisi za umma kufunga sehemu ya maoni wanapochapisha taarifa kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii. Matokeo yake, wananchi wanashindwa kutoa maoni hata katika masuala ya kawaida yasiyo na mivutano ya kisiasa.

Hali hii inaibua wasiwasi kuhusu namna viongozi wanavyoyapokea mabadiliko ya kidijitali duniani, wakati ambapo shughuli nyingi sasa zinategemea intaneti. Kabla ya kuwalaumu wananchi ambao ndio walaji na wachangiaji wakuu wa maudhui tunapaswa kujiuliza: je, viongozi wetu wanaelewa vema nafasi ya intaneti katika jamii ya leo? Wengi wao wanaonekana kutaka kuitumia mitandao kwa ajili ya kutuma taarifa pekee , siyo kupokea mrejesho au maoni.

Aliyewahi kuwa Balozi wa Cuba na Msemaji wa CCM, Humphrey Polepole, aliwahi kukemea tabia ya viongozi wanaopuuza ujumbe katika majukwaa ya mawasiliano kama WhatsApp, akifananisha tabia hiyo na "uhuni" kwa kiongozi wa umma. Alikosoa vikali mtindo wa Viongozi kuondoa kipengele cha 'blue tick" kwenye WhatsApp zao wanapotumiwa ujumbe na wananchi.

Tuliharakisha Kutunga Sheria Kali, Tukasahau Kujielimisha
Kadiri ulimwengu wa kidijitali ulivyokuwa ukikua na kuonekana kama tishio kwa watawala katika mataifa makubwa, mamlaka zetu zilikimbilia kutunga sheria na kanuni kali kuhusu matumizi ya intaneti, tukiamini huo ndio njia bora ya kujilinda.

Barikiwa sana ndugu natamani ingekuwa wewe ni mmoja wa washupaza shingo uliyetambua tunapokosea.Wasilisho zuri sana ila watalielewaaa?
 
Mods mnatulazimishia reactions au,mbona zachaguo zina goma ama shida iko kwa wapi?
 
Wanasema keyboard warriors hawana impact...
Wakati wanawazindua kutoka usingizi wa kukoroma?Ila kwa kuwa walishajiita viziwi wanahidai wamepoteza uwezo wa kusikia.Je vipi na kuonanapo wamepoteza uwezo au viburi na dharau tuu?
 
Noma sana
 
Back
Top Bottom