Vijana wanataka nini mkuu, na serikali ifanyeje ili mahitaji hayo yaweze kutolewa?Viongozi wetu wanapaswa kuelewa jambo moja muhimu: kizazi cha sasa cha vijana si kizazi cha kuamrishwa bila kuuliza maswali. Hawa vijana wamefundishwa kuhusu demokrasia, haki za binadamu, uchaguzi huru na wa haki, utawala wa sheria, na uwajibikaji wa serikali. Hivyo wanapoona tofauti kati ya wanachofundishwa na uhalisia wanaouona, huzalisha hasira, kutokuamini mfumo, na msuguano mkubwa wa kisiasa.
Matukio ya tarehe 29 Oktoba yalipaswa kuwa somo kwa taifa, si jambo la kufunikwa kimya. Kukandamiza maoni ya vijana kwa nguvu hakumalizi tatizo; mara nyingi huahirisha mlipuko wa baadaye. Historia ya dunia inaonyesha kuwa jamii inapofika hatua ambayo vijana wengi wanaamini mfumo hauwasikilizi, huanza kutafuta njia nyingine za kujieleza na hapo ndipo utulivu wa taifa huingia hatarini.
Ni muhimu viongozi wakatambua kuwa hawa vijana si wajinga. Wanasoma dunia kupitia mitandao, elimu, teknolojia, na uzoefu wa mataifa mengine. Wanajua maana ya uchaguzi wa haki, uhuru wa kutoa maoni, na haki za kiraia. Ukiwafundisha misingi hiyo halafu ukionekana kuiheshimu kwa maneno lakini si kwa vitendo, unazalisha kizazi chenye hasira ya kimfumo.
Pia kuna jambo la kutafakari kwa kina: taifa linaendelea kuwapeleka vijana katika mafunzo ya kijeshi na uzalendo kupitia JKT. Hilo si tatizo lenyewe. Tatizo linaanza pale ambapo vijana wenye hasira, waliopoteza imani na mfumo, wanaendelea kupata nidhamu ya kijeshi, mtandao wa kijamii, na uwezo wa kujipanga. Taifa lolote makini linapaswa kuona hatari ya muda mrefu ya kuchanganya ukosefu wa matumaini, ukandamizaji wa kisiasa, na kizazi kikubwa cha vijana waliokatishwa tamaa.
Suluhisho si vitisho. Suluhisho ni kusikiliza, kufanya mageuzi, kujenga taasisi zinazoaminika, na kuruhusu vijana wajisikie kuwa sehemu ya taifa badala ya maadui wa mfumo. Taifa lolote lisiposikiliza sauti ya vijana mapema, hulazimika kuisikia kwa nguvu baadaye.
Gentleman, hoja yangu si kuhalalisha vurugu wala uharibifu wa mali. Hakuna jamii yenye ustaarabu inayopaswa kufurahia kuchoma vituo, kuharibu miundombinu au kushambulia watu. Lakini pia taifa makini haliwezi kujadili matokeo bila kujadili chanzo cha hasira za kizazi kipya.Gentleman,
ni nani kawafundisha hao vijana mambo hayo unayoyaeleza ya demokrasia, haki za binadamu, uwajibikaji, utawala wa sheria na utawala bora, na akina nani hawajafundishwa masuala hayo?
na kutukana na kuporomosha matusi nani kawafundisha?
hivi kufanya uharibifu mathalani kulipua vituo vya mafuta, kuchoma vituo vya polisi, kuchoma makazi ya watu na ofisi za umma, kupiga watu walioenda kutumia haki zao za kupiga kura na kuwakata vidole, kuharibu miundombinu na matukio nonsense kama hayo yanaweza kufichika na kufunikwa kimya kweli gentleman?
Nani kawafundisha vijana hao kwamba hii ndio njia ya kudai haki zao ambazo ambazo wengine hawana?
Ni muhimu sana kuwalea vijana wetu katika misingi imara ya kimaadili badala ya kusingizia mabadiliko ya teknilojia ya mawasiliono inawafanya kujifunza mambo kutoka mataifa mengine na kuyaaply kwenye taifa lao.
hakuna haja ya kuchochea vijana kufanya mambo useless yanayoweza kupelekea wakaathirika zaidi na hatua zao nonsense za eti kudai haki.
Wawajibike katika kufanya kazi kwa bidii mashambani, viwandani, maofisini na walipe kodi stahiki, ili hatimae wawe na haki au sababu ya kudai haki mahususi mathalani huduma bora za afya, maji, umeme, elimu, miundombinu n.k.
haipo sauti ya kijana wa Tanzania, kote ulimwenguni itapuuzwa 🐒
Mungu Ibariki Tanzania
Vijana wengi wa Tanzania hawataki vita wala machafuko. Wanataka vitu vya msingi ambavyo taifa lolote lenye mfumo wa kisasa linapaswa kuwapa wananchi wake: kusikilizwa, kuheshimiwa, kupata fursa, na kuona sheria zinatumika kwa wote bila upendeleo.Vijana wanataka nini mkuu, na serikali ifanyeje ili mahitaji hayo yaweze kutolewa?
Gentleman,Gentleman, hoja yangu si kuhalalisha vurugu wala uharibifu wa mali. Hakuna jamii yenye ustaarabu inayopaswa kufurahia kuchoma vituo, kuharibu miundombinu au kushambulia watu. Lakini pia taifa makini haliwezi kujadili matokeo bila kujadili chanzo cha hasira za kizazi kipya.
Unauliza nani kawafundisha vijana kuhusu demokrasia, haki za binadamu, utawala bora, na uchaguzi huru na wa haki? Mfumo wenyewe wa elimu wa Tanzania ndio uliowafundisha. Civic and Moral Education darasa la nne kuna mada ya haki za binadamu. Sekondari wanafundishwa demokrasia, katiba, utawala wa sheria, uwajibikaji, pamoja na free and fair elections. Hivyo tusishangae vijana wanapoanza kupima uhalisia wa nchi yao kwa yale yale waliyojifunza darasani.
Tofauti ya kizazi hiki na vya nyuma ni kwamba hawaishi tena kwenye zama za taarifa moja kutoka TBC pekee. Kupitia mitandao ya kijamii wanaona namna mataifa mengine yanavyojadili siasa zao, wanaona vijana wa Kenya wakitetea katiba yao, wanaona namna upinzani unavyokandamizwa, wanaona mijadala ya utekaji, wanajiuliza maswali kuhusu watu kama Ben Saanane au Mdude Nyagali. Unaweza usikubaliane na hitimisho lao, lakini huwezi kuwazuia kuona na kuuliza.
Hatari zaidi ni pale vijana wanaposikia lugha za dharau kutoka kwa viongozi huku wakiona mfumo ukiwalinda wenye nguvu kupitia vyombo vya dola. Hapo ndipo kizazi kinaanza kupoteza imani si kwa chama pekee, bali kwa taasisi nzima za taifa.
Kuwaambia vijana wafanye kazi na walipe kodi ni sawa. Lakini kizazi kinacholipa kodi pia hutaka kuuliza maswali. Historia ya dunia inaonyesha kuwa maendeleo ya kiuchumi pekee hayawezi kuzima hitaji la haki, uwazi, na ushiriki wa kisiasa.
Tusijidanganye kwamba vijana hawaoni yanayotokea. Wanaona. Wanasikia. Wanajadili. Na katika dunia ya leo, taarifa haziwezi tena kufungwa ndani ya mipaka ya taifa.
Sahihi mkuu,kama zilivyoundwa tume nyingi pia wangeunda tume za kukusanywa vijana na kuhoji kwenye dodoso,Vijana waeleze wanataka serikali iwafanyie kitu Gani na utekelezaji uwepo pia sio kuishia kwenye makaratasi tuu .Viongozi wetu wanapaswa kuelewa jambo moja muhimu: kizazi cha sasa cha vijana si kizazi cha kuamrishwa bila kuuliza maswali. Hawa vijana wamefundishwa kuhusu demokrasia, haki za binadamu, uchaguzi huru na wa haki, utawala wa sheria, na uwajibikaji wa serikali. Hivyo wanapoona tofauti kati ya wanachofundishwa na uhalisia wanaouona, huzalisha hasira, kutokuamini mfumo, na msuguano mkubwa wa kisiasa.
Matukio ya tarehe 29 Oktoba yalipaswa kuwa somo kwa taifa, si jambo la kufunikwa kimya. Kukandamiza maoni ya vijana kwa nguvu hakumalizi tatizo; mara nyingi huahirisha mlipuko wa baadaye. Historia ya dunia inaonyesha kuwa jamii inapofika hatua ambayo vijana wengi wanaamini mfumo hauwasikilizi, huanza kutafuta njia nyingine za kujieleza na hapo ndipo utulivu wa taifa huingia hatarini.
Ni muhimu viongozi wakatambua kuwa hawa vijana si wajinga. Wanasoma dunia kupitia mitandao, elimu, teknolojia, na uzoefu wa mataifa mengine. Wanajua maana ya uchaguzi wa haki, uhuru wa kutoa maoni, na haki za kiraia. Ukiwafundisha misingi hiyo halafu ukionekana kuiheshimu kwa maneno lakini si kwa vitendo, unazalisha kizazi chenye hasira ya kimfumo.
Pia kuna jambo la kutafakari kwa kina: taifa linaendelea kuwapeleka vijana katika mafunzo ya kijeshi na uzalendo kupitia JKT. Hilo si tatizo lenyewe. Tatizo linaanza pale ambapo vijana wenye hasira, waliopoteza imani na mfumo, wanaendelea kupata nidhamu ya kijeshi, mtandao wa kijamii, na uwezo wa kujipanga. Taifa lolote makini linapaswa kuona hatari ya muda mrefu ya kuchanganya ukosefu wa matumaini, ukandamizaji wa kisiasa, na kizazi kikubwa cha vijana waliokatishwa tamaa.
Suluhisho si vitisho. Suluhisho ni kusikiliza, kufanya mageuzi, kujenga taasisi zinazoaminika, na kuruhusu vijana wajisikie kuwa sehemu ya taifa badala ya maadui wa mfumo. Taifa lolote lisiposikiliza sauti ya vijana mapema, hulazimika kuisikia kwa nguvu baadaye.
Gentleman, hakuna anayepaswa kuhalalisha ugaidi, vurugu, au uharibifu wa taifa. Lakini pia hakuna taifa linaloweza kujenga amani ya kudumu kwa kukataa kujiuliza kwanini kizazi chake kina hasira kubwa kiasi hicho.Gentleman,
ikiwa ni mfumo wa elimu ya Tanzania ndio umewafundisha hayo masuala ya demokrasia, haki za binadamu, uwajibikaji utawala bora n.k, maana yake, Tanzania ina nia njema na wananchi wake, inataka kila mtu afahamu wajibu wake na anachostahili, right?
Sasa kulikoni waache kutumia demokrasia waliyofunzwa kufanya mabadiliko kadiri ya matamanio yao, na badala yake wakubali kubebwa ufala wa kifikra na wanjanja, mathalani baadhi ya AZAKI, na kisha wapewe mafunzo ya kigaidi, wafadhiliwe kwenda kufanya uharibifu na kusababisha maafa kwa ndugu, jamaa na marafiki zao?
Hayo ndio waliyofundishwa?
huoni kwamba hiyo ni changamoto ya hayo unayosema wanajifunza kwa wenzao wa sijui kutoka wapi na wapi huko kupitia mitandao na teknilojia ya mawasiliono? Yaani kwa vile unaweza kupata taarifa kupitia nje ya TBC, basi hiyo inakua fursa ya wewe kujitumbukiza kwenye hatari ya kujiangamiza mwenyewe, right?
Suala la kudanganyana hakuna tena, ni kisingizio tu cha kujaribu kuhalalisha uharibifu au uhalifu fulani. Udanganywe ili iweje na kwa faida ya nani. Tanzania mambo yote yanafanyika hadharani labda kwingineko ndiko wanaweza kudanganyana.
Tanzania tukisema barabara zimejenga unaziona zikijengwa, hospitali, mashule, mabwawa n.k vyote vinafanyika mchana kweupe, kwahiyo hakuna kudanganyana hata kidogo.
hayo mengine sijui ya utekaji n.k,
nadhani ni michezo ya kisiasa tu ambayo imezoeleka nyakati hizi, karibu duniani kote. Na michezo hiyo haiwezi kua kisingizio cha kuharibu amani, umoja na utulivu wa taifa letu, au kuchochea watu kujiangamiza wenyewe kwa wenyewe.🐒
Katika historia ya mataifa, kuna jambo moja linalojirudia kama mzunguko usioepukika: watawala karibu wote hufahamu mahitaji ya wananchi wao, lakini wachache huchagua kuyasikia kwa wakati.Sahihi mkuu,kama zilivyoundwa tume nyingi pia wangeunda tume za kukusanywa vijana na kuhoji kwenye dodoso,Vijana waeleze wanataka serikali iwafanyie kitu Gani na utekelezaji uwepo pia sio kuishia kwenye makaratasi tuu .
Magufuri alipo ingia madarakani alijaribu kuwapa vijana nafasi za maamuzi nchini kwa kuwapa madaraka mbalimbali lakini mwisho wa siku ndo tulishuhudia mambo ya hovyo kutoka kwa hao vijana walio kuwa na ushamba wa madaraka mfano akina Sabaya ,Makonda na Ali Hapi nkVijana wengi wa Tanzania hawataki vita wala machafuko. Wanataka vitu vya msingi ambavyo taifa lolote lenye mfumo wa kisasa linapaswa kuwapa wananchi wake: kusikilizwa, kuheshimiwa, kupata fursa, na kuona sheria zinatumika kwa wote bila upendeleo.
Wanataka uchaguzi unaoaminika. Wanataka uhuru wa kusema bila kuogopa kutekwa au kuitwa maadui wa taifa. Wanataka taasisi zinazowajibika. Wanataka kuona bunge likisimamia serikali badala ya kusifia kila kitu. Wanataka kuona mfumo unaowapa nafasi ya kushiriki kwenye maamuzi ya taifa ambalo wao ndio wataliendesha kesho.
Tatizo ni kwamba mara nyingi mfumo wetu unawachukulia vijana kama watu wa kuhamasishwa wakati wa uchaguzi pekee, si washirika wa maamuzi ya kitaifa. Hilo ni kosa kubwa la kimkakati.
Mfano mzuri ni baada ya matukio ya 29 Oktoba. Kama kweli taifa lilitaka kujua nini kiliharibika, ingewekwa tume yenye uwakilishi mpana wa kizazi cha vijana, wanazuoni, wanasaikolojia wa jamii, wanaharakati, na wataalamu huru. Lakini vijana wenyewe ambao ndio walikuwa katikati ya hasira na malalamiko walibaki pembeni. Wengi waliopewa nafasi ni wazee, viongozi wa kisiasa, au watu wa mfumo ule ule uliokuwa unalalamikiwa. Hapo vijana wengi waliona kuwa mfumo unajichunguza wenyewe.
Ukiondoa vijana kwenye maamuzi muhimu ya taifa huku wao ndio nguvu kazi, walipa kodi wa kesho, na kundi kubwa zaidi kijamii, unajenga tatizo la muda mrefu. Hiyo si siasa tena; ni suala la uthabiti wa taifa.
Historia inaonyesha mataifa mengi hayakuingia kwenye migogoro kwa sababu watu hawakuwa na chakula pekee, bali kwa sababu kizazi kipya kilihisi hakina sauti ndani ya mfumo wake wenyewe.
Kuwasikiliza vijana si udhaifu wa serikali. Ni uwekezaji wa amani ya muda mrefu.
Tukirejelea historia, unajua bhn hoja hii imejitokeza mara nyingi kwa nyakati tofauti: “Tatizo si mfumo, ni watu.”Magufuri alipo ingia madarakani alijaribu kuwapa vijana nafasi za maamuzi nchini kwa kuwapa madaraka mbalimbali lakini mwisho wa siku ndo tulishuhudia mambo ya hovyo kutoka kwa hao vijana walio kuwa na ushamba wa madaraka mfano akina Sabaya ,Makonda na Ali Hapi nk
Katika kitu ambacho waafrika tunakosea ni kudhani kuwa matatizo yetu yana sababishwa na kundi fulani tu lakini sio kweli,matatizo ya waafrika yanasababishwa na huruka yetu ya ubinafisi na tabia ya kutowajibika kama jamii kwa ujumla na tabia hii haipo kwa wana siasa tu bali hili lipo kwenye jamii yote ya waafirika si kwa wazee,vijana,wafanyakazi ,wasomi,wasio na kazi,wakulima ,ambao hawajasoma.
Ukitaka kulijua hilo ebu angalia maisha yetu ya kila siku yamejaa ulaghai mtupu ,kuibiana na kurudishana nyuma kufanyiana fitina kiufupi kitu kinacho itwa uadilifu na uaminifu kwa muafirika ni kitu ghali sana kwake.
Mfano sasa hivi kafungue duka la milion 5 alafu umtafute kijana mojawapo muhitimu wa chuo anaye hangaika kutafuta ajira kwa miaka 5 ukisha muajili, fikira zake hazitakuwa ni namna gani ya kukuza duka lako bali fikira zake zitakuwa ni namna gani ya kukuibia ili apate hela za kuhonga mademu zake na kunywa pombe au kununua simu ya maana.
Au ww tafuta fundi umuajili kujenga,
fikira zake hazitakuwa kufanya kazi yako kwa ubora ili na kesho umuitie kazi nyingine, bali fikira zake ni huyu jamaa atatoka saa ngapi nipate nafasi ya kumchomoa mifuko miwili ya simenti
hizi ndo akili za waafirika walio wengi.
Hata leo ccm ikitokea ikaondoka madarakani kikaingia chama kingine madarakani hakuna chochote kitakacho badilika ndani ya nchii kwa sababu tatizo sio chama bali taitizo ni watu ,hizo porojo za wanasiasa majukwaani ni za kutafutia madaraka tu lakini wakisha yapata mtaamini macho yenu.
Kuna msemo mmoja unasema kuwa Watz wengi hatuchukii ufisadi bali tunachukia ni kwanini nafasi ya kufanya ufisadi aipate fulani na sio mimi.
Mkuu huwezi kujenga mifumo ya kiwajibikaji kutoka kwenye jamii isiyo ya kiwajibikaji ,huwezi kujenga mifumo ya uaminifu kutoka kwenye jamii usio thamini uaminifu kwa sababu hiyo mfumo haitajiendesha kama robot bali hiyo mifumo itatakiwa kusimamiwa na watu kutoka kwenye jamii husika.Tukirejelea historia, unajua bhn hoja hii imejitokeza mara nyingi kwa nyakati tofauti: “Tatizo si mfumo, ni watu.”
Ni kauli yenye ukweli nusu na hatari nusu nyingine.
Ndiyo, Afrika imepata maumivu makubwa kutoka kwenye rushwa, ubinafsi, na udhaifu wa maadili ya kijamii. Lakini historia pia inatufundisha jambo ambalo mara nyingi hupuuzwa: mifumo huumba tabia, na tabia huimarishwa na mifumo.
Roma ya mwisho haikuanguka kwa sababu Waroma wote walikuwa wabaya, bali kwa sababu taasisi zake zilianza kuzoea upendeleo, ukimya wa wasomi, na ulinzi wa tabaka la madaraka. Urusi ya kifalme haikuanguka kwa sababu kila raia alikuwa fisadi, bali kwa sababu mfumo ulifunga njia za uwajibikaji hadi uhalisia ukalipuka kwa nguvu.
Hivyo kusema “ni watu tu” pekee ni kurahisisha historia kupita kiasi.
Kuhusu hoja ya vijana kushindwa kupewa nafasi: historia ina mifano miwili. Kuna vijana waliopata madaraka ndani ya mifumo isiyo na uwajibikaji wakageuka kuwa Sabaya, Makonda, au mifano mingine ya matumizi mabaya ya mamlaka. Lakini hilo halikanushi hoja kuu linaonyesha tatizo la pili: mfumo usio na vizuizi imara vya uwajibikaji.
Madaraka bila uwazi hayabadilishi tabia huyapanua.
Na kuhusu kauli kwamba “Mtu akiajiri kijana ataiba,” hiyo si sheria ya jamii, bali ni dalili ya jamii iliyopoteza imani kati ya pande zake mbili. Historia inaonyesha pale ambapo mwajiri na mwajiriwa wanapoingia katika uhusiano wa kutoaminiana, uchumi wenyewe huanza kuoza taratibu si kwa sababu ya tabia ya kundi moja, bali kwa sababu mfumo wa usimamizi na haki umedhoofika.
Tatizo kubwa zaidi katika mataifa mengi si ukosefu wa maadili binafsi pekee, bali ni ukosefu wa mifumo inayolazimisha maadili hayo kuwa na gharama pale yanapovunjwa.
Na mwisho, kauli kwamba “hakuna kitakachobadilika hata chama kikibadilika” ni mtazamo wa historia iliyokwama. Mabadiliko ya mataifa makubwa hayakuja kwa kubadili watu tu, bali kwa kubadili sheria za mchezo namna mamlaka inavyotumika, inavyodhibitiwa, na inavyowajibishwa.
Historia haipingi tabia ya watu. Lakini pia haijawahi kusamehe mifumo inayodhani watu hawawezi kubadilika.
Mkuu, hapa ndipo historia ya mataifa inapokuwa ngumu kuliko tunavyodhani. Ni kweli huwezi kupata mfumo mkamilifu ndani ya jamii yenye mapungufu ya kibinadamu lakini pia ni kweli huwezi kusubiri jamii iwe malaika ndipo ujenge taasisi imara. Mataifa yote yaliyofanikiwa yalijenga mifumo yao katikati ya ubinafsi wa binadamu, si baada ya ubinafsi kuisha.Mkuu huwezi kujenga mifumo ya kiwajibikaji kutoka kwenye jamii isiyo ya kiwajibikaji ,huwezi kujenga mifumo ya uaminifu kutoka kwenye jamii usio thamini uaminifu kwa sababu hiyo mfumo haitajiendesha kama robot bali hiyo mifumo itatakiwa kusimamiwa na watu kutoka kwenye jamii husika.
Mfano katiba kwa kuisoma ina mambo mengi mazuri tu ambayo yakisimamiwa kiwajibikaji matatizo mengi ya nchi hii yatatuliwa lakini kwa sababu iko kwenye jamii isiyo kuwa ta kiwajibikaji hakuna chochote inacho tufaa.
Umetolea mfano mataifa makubwa ya kizungu jinsi yalivyo leta mabadiliko kwa kubadalisha mifumo yao lakini hujatolea mfano wa Zambia,ghana,senegal ambao kwa mara kadhaa wamejaribu kubadilisha vyama lakini mambo ni yale yale.
Unaongea vitu vya kufikirika na vigumu kupimika nje ya uga wa kisiasa.Vijana wengi wa Tanzania hawataki vita wala machafuko. Wanataka vitu vya msingi ambavyo taifa lolote lenye mfumo wa kisasa linapaswa kuwapa wananchi wake: kusikilizwa, kuheshimiwa, kupata fursa, na kuona sheria zinatumika kwa wote bila upendeleo.
Wanataka uchaguzi unaoaminika. Wanataka uhuru wa kusema bila kuogopa kutekwa au kuitwa maadui wa taifa. Wanataka taasisi zinazowajibika. Wanataka kuona bunge likisimamia serikali badala ya kusifia kila kitu. Wanataka kuona mfumo unaowapa nafasi ya kushiriki kwenye maamuzi ya taifa ambalo wao ndio wataliendesha kesho.
Tatizo ni kwamba mara nyingi mfumo wetu unawachukulia vijana kama watu wa kuhamasishwa wakati wa uchaguzi pekee, si washirika wa maamuzi ya kitaifa. Hilo ni kosa kubwa la kimkakati.
Mfano mzuri ni baada ya matukio ya 29 Oktoba. Kama kweli taifa lilitaka kujua nini kiliharibika, ingewekwa tume yenye uwakilishi mpana wa kizazi cha vijana, wanazuoni, wanasaikolojia wa jamii, wanaharakati, na wataalamu huru. Lakini vijana wenyewe ambao ndio walikuwa katikati ya hasira na malalamiko walibaki pembeni. Wengi waliopewa nafasi ni wazee, viongozi wa kisiasa, au watu wa mfumo ule ule uliokuwa unalalamikiwa. Hapo vijana wengi waliona kuwa mfumo unajichunguza wenyewe.
Ukiondoa vijana kwenye maamuzi muhimu ya taifa huku wao ndio nguvu kazi, walipa kodi wa kesho, na kundi kubwa zaidi kijamii, unajenga tatizo la muda mrefu. Hiyo si siasa tena; ni suala la uthabiti wa taifa.
Historia inaonyesha mataifa mengi hayakuingia kwenye migogoro kwa sababu watu hawakuwa na chakula pekee, bali kwa sababu kizazi kipya kilihisi hakina sauti ndani ya mfumo wake wenyewe.
Kuwasikiliza vijana si udhaifu wa serikali. Ni uwekezaji wa amani ya muda mrefu.
We ngoja tu hawa CCM watajutia.Viongozi wetu wanapaswa kuelewa jambo moja muhimu: kizazi cha sasa cha vijana si kizazi cha kuamrishwa bila kuuliza maswali. Hawa vijana wamefundishwa kuhusu demokrasia, haki za binadamu, uchaguzi huru na wa haki, utawala wa sheria, na uwajibikaji wa serikali. Hivyo wanapoona tofauti kati ya wanachofundishwa na uhalisia wanaouona, huzalisha hasira, kutokuamini mfumo, na msuguano mkubwa wa kisiasa.
Matukio ya tarehe 29 Oktoba yalipaswa kuwa somo kwa taifa, si jambo la kufunikwa kimya. Kukandamiza maoni ya vijana kwa nguvu hakumalizi tatizo; mara nyingi huahirisha mlipuko wa baadaye. Historia ya dunia inaonyesha kuwa jamii inapofika hatua ambayo vijana wengi wanaamini mfumo hauwasikilizi, huanza kutafuta njia nyingine za kujieleza na hapo ndipo utulivu wa taifa huingia hatarini.
Ni muhimu viongozi wakatambua kuwa hawa vijana si wajinga. Wanasoma dunia kupitia mitandao, elimu, teknolojia, na uzoefu wa mataifa mengine. Wanajua maana ya uchaguzi wa haki, uhuru wa kutoa maoni, na haki za kiraia. Ukiwafundisha misingi hiyo halafu ukionekana kuiheshimu kwa maneno lakini si kwa vitendo, unazalisha kizazi chenye hasira ya kimfumo.
Pia kuna jambo la kutafakari kwa kina: taifa linaendelea kuwapeleka vijana katika mafunzo ya kijeshi na uzalendo kupitia JKT. Hilo si tatizo lenyewe. Tatizo linaanza pale ambapo vijana wenye hasira, waliopoteza imani na mfumo, wanaendelea kupata nidhamu ya kijeshi, mtandao wa kijamii, na uwezo wa kujipanga. Taifa lolote makini linapaswa kuona hatari ya muda mrefu ya kuchanganya ukosefu wa matumaini, ukandamizaji wa kisiasa, na kizazi kikubwa cha vijana waliokatishwa tamaa.
Suluhisho si vitisho. Suluhisho ni kusikiliza, kufanya mageuzi, kujenga taasisi zinazoaminika, na kuruhusu vijana wajisikie kuwa sehemu ya taifa badala ya maadui wa mfumo. Taifa lolote lisiposikiliza sauti ya vijana mapema, hulazimika kuisikia kwa nguvu baadaye.
Bili yako ya maji ya mwezi huu nitalipa mimi.Viongozi wetu wanapaswa kuelewa jambo moja muhimu: kizazi cha sasa cha vijana si kizazi cha kuamrishwa bila kuuliza maswali. Hawa vijana wamefundishwa kuhusu demokrasia, haki za binadamu, uchaguzi huru na wa haki, utawala wa sheria, na uwajibikaji wa serikali. Hivyo wanapoona tofauti kati ya wanachofundishwa na uhalisia wanaouona, huzalisha hasira, kutokuamini mfumo, na msuguano mkubwa wa kisiasa.
Matukio ya tarehe 29 Oktoba yalipaswa kuwa somo kwa taifa, si jambo la kufunikwa kimya. Kukandamiza maoni ya vijana kwa nguvu hakumalizi tatizo; mara nyingi huahirisha mlipuko wa baadaye. Historia ya dunia inaonyesha kuwa jamii inapofika hatua ambayo vijana wengi wanaamini mfumo hauwasikilizi, huanza kutafuta njia nyingine za kujieleza na hapo ndipo utulivu wa taifa huingia hatarini.
Ni muhimu viongozi wakatambua kuwa hawa vijana si wajinga. Wanasoma dunia kupitia mitandao, elimu, teknolojia, na uzoefu wa mataifa mengine. Wanajua maana ya uchaguzi wa haki, uhuru wa kutoa maoni, na haki za kiraia. Ukiwafundisha misingi hiyo halafu ukionekana kuiheshimu kwa maneno lakini si kwa vitendo, unazalisha kizazi chenye hasira ya kimfumo.
Pia kuna jambo la kutafakari kwa kina: taifa linaendelea kuwapeleka vijana katika mafunzo ya kijeshi na uzalendo kupitia JKT. Hilo si tatizo lenyewe. Tatizo linaanza pale ambapo vijana wenye hasira, waliopoteza imani na mfumo, wanaendelea kupata nidhamu ya kijeshi, mtandao wa kijamii, na uwezo wa kujipanga. Taifa lolote makini linapaswa kuona hatari ya muda mrefu ya kuchanganya ukosefu wa matumaini, ukandamizaji wa kisiasa, na kizazi kikubwa cha vijana waliokatishwa tamaa.
Suluhisho si vitisho. Suluhisho ni kusikiliza, kufanya mageuzi, kujenga taasisi zinazoaminika, na kuruhusu vijana wajisikie kuwa sehemu ya taifa badala ya maadui wa mfumo. Taifa lolote lisiposikiliza sauti ya vijana mapema, hulazimika kuisikia kwa nguvu baadaye.
Kaka Msaka jr,, hayo ndiyo hasa mambo ambayo vijana wanataka yazungumzwe kwa seriousness badala ya propaganda za kisiasa kila siku.Unaongea vitu vya kufikirika na vigumu kupimika nje ya uga wa kisiasa.
Sema serikali ifanyeje kuongeza fursa za ajira kwa vijana ktk sekta rasmi?
Sema serikali ifanyeje kuongeza mapato ili iache kutegemea wahisani na ipunguze kukopa kwa miradi isiyo ya kibiashara?