Kupuuza Sauti za Vijana leo ni kutengeneza mgogoro wa Taifa Kesho

Kupuuza Sauti za Vijana leo ni kutengeneza mgogoro wa Taifa Kesho

Magufuri alipo ingia madarakani alijaribu kuwapa vijana nafasi za maamuzi nchini kwa kuwapa madaraka mbalimbali lakini mwisho wa siku ndo tulishuhudia mambo ya hovyo kutoka kwa hao vijana walio kuwa na ushamba wa madaraka mfano akina Sabaya ,Makonda na Ali Hapi nk
Katika kitu ambacho waafrika tunakosea ni kudhani kuwa matatizo yetu yana sababishwa na kundi fulani tu lakini sio kweli,matatizo ya waafrika yanasababishwa na huruka yetu ya ubinafisi na tabia ya kutowajibika kama jamii kwa ujumla na tabia hii haipo kwa wana siasa tu bali hili lipo kwenye jamii yote ya waafirika si kwa wazee,vijana,wafanyakazi ,wasomi,wasio na kazi,wakulima ,ambao hawajasoma.
Ukitaka kulijua hilo ebu angalia maisha yetu ya kila siku yamejaa ulaghai mtupu ,kuibiana na kurudishana nyuma kufanyiana fitina kiufupi kitu kinacho itwa uadilifu na uaminifu kwa muafirika ni kitu ghali sana kwake.

Mfano sasa hivi kafungue duka la milion 5 alafu umtafute kijana mojawapo muhitimu wa chuo anaye hangaika kutafuta ajira kwa miaka 5 ukisha muajili, fikira zake hazitakuwa ni namna gani ya kukuza duka lako bali fikira zake zitakuwa ni namna gani ya kukuibia ili apate hela za kuhonga mademu zake na kunywa pombe au kununua simu ya maana.
Au ww tafuta fundi umuajili kujenga,
fikira zake hazitakuwa kufanya kazi yako kwa ubora ili na kesho umuitie kazi nyingine, bali fikira zake ni huyu jamaa atatoka saa ngapi nipate nafasi ya kumchomoa mifuko miwili ya simenti
hizi ndo akili za waafirika walio wengi.

Hata leo ccm ikitokea ikaondoka madarakani kikaingia chama kingine madarakani hakuna chochote kitakacho badilika ndani ya nchii kwa sababu tatizo sio chama bali taitizo ni watu ,hizo porojo za wanasiasa majukwaani ni za kutafutia madaraka tu lakini wakisha yapata mtaamini macho yenu.
Kuna msemo mmoja unasema kuwa Watz wengi hatuchukii ufisadi bali tunachukia ni kwanini nafasi ya kufanya ufisadi aipate fulani na sio mimi.
Kwahiyo hakuna maana ya vijana kusikilizwa au kupewa nafasi?
 
Unaongea vitu vya kufikirika na vigumu kupimika nje ya uga wa kisiasa.

Sema serikali ifanyeje kuongeza fursa za ajira kwa vijana ktk sekta rasmi?

Sema serikali ifanyeje kuongeza mapato ili iache kutegemea wahisani na ipunguze kukopa kwa miradi isiyo ya kibiashara?
Mkuu sasa kama wananchi ndio tutatakiwa kutoa majibu ya changamoto zetu, hiyo serikali kazi yake nini. Hayo uliyoyasema yote kuna watendaji uko serikalini wanalipwa pesa nyingi ili walete majibu.
 
Mkuu sasa kama wananchi ndio tutatakiwa kutoa majibu ya changamoto zetu, hiyo serikali kazi yake nini. Hayo uliyoyasema yote kuna watendaji uko serikalini wanalipwa pesa nyingi ili walete majibu.
Mwanzisha mada ametaka kuishauri serikali kuhusu ustawi wa vijana nchini. Mimi nimemshauri maeneo sahihi ili dhamira yake ya kuinua vijana itimie.
Kumbuka hao watendaji wanaajira zao tayari. Wenye uhitaji na ajira ni vijana tuliopo mtaani.
Sio dhambi kuishauri serikali mkuu.
 
Mwanzisha mada ametaka kuishauri serikali kuhusu ustawi wa vijana nchini. Mimi nimemshauri maeneo sahihi ili dhamira yake ya kuinua vijana itimie.
Kumbuka hao watendaji wanaajira zao tayari. Wenye uhitaji na ajira ni vijana tuliopo mtaani.
Sio dhambi kuishauri serikali mkuu.
Ni kweli kutoa ushauri na mapendekezo sio dhambi.
 
  • Thanks
Reactions: 30P
Kaka Msaka jr,, hayo ndiyo hasa mambo ambayo vijana wanataka yazungumzwe kwa seriousness badala ya propaganda za kisiasa kila siku.

Kwanza, kuhusu ajira za vijana kwenye sekta rasmi serikali haiwezi kutatua hili kwa kuajiri watu wote serikalini. Historia ya maendeleo ya mataifa inaonyesha ajira kubwa hutengenezwa na sekta binafsi yenye nguvu. Lakini sekta binafsi haiwezi kukua kwenye mazingira yenye kodi zisizotabirika, rushwa, upendeleo wa kisiasa, na mfumo ambao vijana wengi hawawezi kupata mitaji wala access ya haki kwenye fursa.

Ukimsikiliza kijana wa leo, analalamika zaidi kuhusu mfumo usio na meritocracy. Anaona connection zina nguvu kuliko uwezo. Anaona tender, nafasi, na fursa nyingi zikiwa karibu na mtandao wa kisiasa kuliko ushindani wa wazi. Hapo hata uchumi ukikua kwa asilimia nzuri kwenye karatasi, frustration ya vijana itaendelea.

Serikali ingefanya vitu vya msingi:

  • Kupunguza urasimu wa biashara ndogo na startups.
  • Kujenga mazingira ya venture capital na innovation badala ya uchumi wa mazoea.
  • Kuongeza uwazi kwenye zabuni na ajira.
  • Kuwekeza zaidi kwenye digital economy, manufacturing, na value addition badala ya kutegemea raw materials.
  • Kulinda uhuru wa taarifa na internet kwa sababu uchumi wa kizazi hiki unategemea taarifa na teknolojia.

Pili, kuhusu mapato ya taifa huwezi kujenga uchumi imara kwa mikopo pekee wakati uzalishaji wa ndani bado mdogo. Mataifa mengi yaliyopunguza utegemezi wa wahisani yalifanya vitu viwili: yalijenga taasisi zinazoaminika na yakapanua uzalishaji wa ndani.

Tatizo ni kwamba uwekezaji mkubwa unahitaji kitu kimoja ambacho mara nyingi wanasiasa hawapendi kukisikia: trust. Wawekezaji wa ndani na nje wanahitaji kuona mahakama zinazoaminika, sheria zisizobadilika kisiasa, na mazingira ambayo mafanikio hayatategemea ukaribu wako na mamlaka.

Hivyo haya si mambo ya kufikirika. Uchumi, ajira, na siasa haviwezi kutenganishwa. Historia ya dunia inaonyesha hakuna taifa lililojenga uchumi mkubwa wa kisasa huku vijana wake wakikosa matumaini, taasisi zikikosa kuaminika, na mfumo ukionekana kuwafungia nje watu wengi wenye uwezo.
Umetaja maeneo yanayopaswa kuwekewa mkakati. Andika 'story of change' kuhusu maeneo hayo Jamii inufaike na ubunifu wako mkuu.
 
Back
Top Bottom