kwanini maji ya mabwawa na maziwa kupwa na kujaa kwake hakuonekani kama ilivyo baharini?
- Tunachokijua
- Kupwa na kujaa kwa maji ni kitendo kinachosababisha kutembea kwa maji ikiwa ni athari ya moja kwa moja iliyosababishwa na nguvu ya uvutano (Gravitational attraction) inayosababishwa na jua pamoja na mwezi ambapo nguvu hiyo huivuta dunia kuelekea upande wa mwezi au jua. Kupwa na kujaa kwa maji baharini huthibitika katika pwani ya bahari ambapo kupungua na kuongezeka kwa kiwango cha maji hudhihirika.
Kwa mujibu wa tovuti ya National Geographic Kupwa na kujaa kwa maji baharini ni mabadiliko ya uwiano wa maji baharini unaopanda na kushuka kila siku. "maji kupwa" ni hali ya chini ya usawa wa maji na maji kujaa ni hali ya usawa wa juu wa maji ya bahari, ambapo Mwanafizikia Sir Isaac Newton alielezea kuwa kitendo hicho ni matokeo ya mvutano kati ya mwezi na dunia ambapo pindi mwezi uwapo karibu na jua hushirikiana kuivuta dunia.
Tovuti hii ya national Geographic inaeleza Sababu inayosababisha kupwa na kujaa kwa maji ni kani ya mvutano (Gravitational attraction) iliyopo kati ya mwezi na dunia ambapo mwezi hujaribu kuivuta dunia, ukaribu kati ya mwezi na dunia huchochea kuongezeka kwa kani ya mvutano. Kani hii ya mvutano hutokea hata kwa jua kuivuta dunia lakini kani hiyo ina nguvu zaidi kwa mwezi kwa sababu mwezi upo karibu zaidi na dunia.
Mvutano huu (Gravitational attraction) huikumba sayari nzima ya dunia lakini kumekuwa na athari ndogo sana dhidi ya uso wa dunia kwa sababu ardhi haitembei tofauti na ilivyo katika bahari hasa upande unaotazamana na mwezi ambapo kani ya mvutano huwa mkubwa tofauti na upande wa dunia ambao kwa wakati huo hautazamani na mwezi huwa na kani ya uvutano ambayo inaenda kinyume na kani inayoivuta dunia kutoka kwenye mwezi.
Watu wamekuwa wakiuliza ni kwanini maji ya mabwawa na maziwa hayakupwi na kujaa kama ilivyo kwenye bahari licha ya wingi wa maji katika baadhi ya mabwawa na maziwa.
Je uhalisia wa jambo hili upoje?
Ukweli ni kwamba kitendo cha kupwa na kujaa kwa maji kwenye maziwa na vyanzo vinginine vya maji hutokea lakini kuonekana kwake si rahisi kama ilivyo baharini kutokana na tofauti ya ukubwa kati ya bahari na maziwa au vyanzo vingine
Kwa mujibu wa mamlaka ya ya taifa ya huduma za bahari ya nchini Marekani kiwango cha usawa wa maji katika maziwa mara nyingi hutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.
tafiti zinaonesha kupwa na kujaa kwa maji kwenye maziwa makubwa pia kunaweza kusababishwa na kani ya mvutano ya jua na mwezi, lakini kutokana na udogo wa maziwa ukilinganisha na ukubwa wa bahari, ambapo katika maziwa makubwa ni sawa au chini ya sentimita tano, yakiwa ni Mabadiliko madogo ambayo hufichwa na mabadiliko makubwa ya usawa wa maji kwenye maziwa yanayosababishwa na upepo na mgandamizo wa anga.
Kinachotokea katika maziwa na vyanzo vingine vidogo vya manji kitaalamu hujulikana kama Seiches ambapo hutokea kutokana na upepo mkali au mgandamizo wa anga ambapo husukuma maji kutoka mwishoni mwa upande wa chanzo hicho kwenda upande mwingine na upepo unaposimama maji hurudi upande mwingine, kitendo hiki kinaweza kuendelea kwa masaa kadha hata zaidi ya siku moja.