View attachment 3172848
FREEMAN MBOWE-PIGAKURA
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
View attachment 3172851TUNDU AM LISSU-PIGAKURA
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
Happy Uhuru Day!!
Habari kuu ndani ya CHADEMA ni mchuano Mkali wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa baina ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake Mhe Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wake anayemaliza muda wake Mhe Tundu Lissu,
Kwa uwazi sana naomba tujipe masaa walau 12 ya kupiga kura hapa Jamii forum ili tuwezi kumpata mshindi wetu wa maoni ya awali,
Kupitia Jukwaa hili la Jamii Forum zimekuwa zikiendeshwa kura nyingi za maoni mfano ni washindi wa Story of Change na washindi wengine mbalimbali katika Poll tofauti tofauti za kisiasa na Kijamii.
Angalizo, Matokeo haya hayatakuwa ni msimamo wa Jamii Forum Wala Mimi mleta Uzi wenu ila ni maoni tu na maamuzi ya wapenzi, mashabiki na Wanachama wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi wao wa ndani ya chama.
Lakini ifahamike pia haya yatakuwa ni maoni tu ambayo pengine yanaweza kubeba uhalisia au Laa hivyo yasipewe uzito sana na watakao ibuka vinara mwishoni mwa zoezi letu kwani yatabaki kuwa ni maoni.
MWISHO ANDIKA JINA LA ULIYEMCHAGUA NA SABABU ZAKO KAMA HUTOJALI.
•••••••••••••