KURA: Je, ni nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu anayefaa zaidi kuiongoza CHADEMA kwa Sasa?

KURA: Je, ni nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu anayefaa zaidi kuiongoza CHADEMA kwa Sasa?

Je, ni nani kati ya Freeman Mbowe na Tundu Lissu anayefaa zaidi kuiongoza CHADEMA kwa Sasa?

  • FREEMAN AIKAEL MBOWE

    Votes: 124 18.2%
  • TUNDU ANTIPAS LISSU

    Votes: 559 81.8%

  • Total voters
    683
  • Poll closed .

Bezecky

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
494
Reaction score
897
IMG-20241209-WA0051.jpg

FREEMAN MBOWE-MTIA NIA
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••
IMG-20241209-WA0050(1).jpg
TUNDU AM LISSU-MTIA NIA
••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••••

Tanzania ni yetu sote!!

Habari kuu ndani ya CHADEMA ni mchuano mkali wa kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA baina ya Mwenyekiti anayemaliza muda wake aliyedumu kwa miaka 20 Mhe Freeman Mbowe na Makamu Mwenyekiti wake anayemaliza muda wake wa miaka mitano Mhe Tundu Lissu,

Kwa uwazi sana naomba tujipe masaa kadhaa ya kupiga kura hapa Jamii forum ili tuwezi kumpata mshindi wetu wa maoni ya awali katika nafasi hiyo muhimu kwa mustakabali wa ustawi wa Tanzània.

Mnafahamu kupitia Jukwaa hili la Jamii Forum zimekuwa zikiendeshwa kura nyingi za maoni mfano ni washindi wa Story of Change na washindi wengine mbalimbali katika Poll tofauti tofauti za kisiasa na Kijamii zilizowahi kuendeshwa kwa uwazi kabisa.

Angalizo, Matokeo haya hayatakuwa ni msimamo wa jukwaa hili la Jamii Forum wala Mimi mleta Uzi wenu ila ni maoni tu na maamuzi ya wapenzi, mashabiki na Wanachama wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi wao wa ndani ya chama.

Lakini ifahamike pia, haya yatakuwa ni maoni tu ambayo pengine yanaweza kubeba uhalisia au Laa hivyo yasipewe uzito sana na watakao ibuka vinara au kushindwa mwishoni mwa zoezi letu kwani yatabaki kuwa ni maoni tu kuelekea kwenye uhalisia.

MWISHO ANDIKA JINA LA ULIYEMCHAGUA NA SABABU ZAKO KAMA HUTOJALI.

•••••••••••••
 
Pigakura moja tu,

Kwanza, Gusa jina la Unayedhani anafaa kuiongoza CHADEMA kwa Sasa,

Pili, Bonyeza sehemu imeandikwa "Cast Vote"

Mwisho unaweza kuacha ujumbe wa kikampeni kwa wachangiaji wanafuata.
 
Chadema bado inamhitaji Mbowe kwa nyakati hizi. Wanaharakati kupewa Chama kwa nyakati hizi itawawia ngumu kufanya kazi kutokana na miongozo ya vyama vya siasa chini ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.
 
Back
Top Bottom