Kura ya maoni kujiunga Urusi, tangazo la kuongeza askari wa akiba: Maneno ya Putin yanatimia kuhusu malengo ya uvamizi wa Ukraine?

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
Habari wana JF,
Siku nyingi zimepita sijaandika mjadala(thread) humu jukwaani. Leo nimesukumwa kuandika mtazamo wangu juu ya kinachoendelea nchini Ukraine wakati huu wa vita dhidi ya uvamizi wa Urusi(Russia).

Raisi Vladimir Putin mara kwa mara amekuwa akirudia kusema malengo yote ya nchi yake kuivamia Ukraine yatatimia. Amekuwa akibezwa na kuonekana anafanya propaganda tu uhalisia ni kuwa atafurushwa Ukraine baada ya kushindwa kwa aibu. Muda huleta majibu sahihi ya mambo yote hivyo tusubiri tuone itakuwaje.

Kwa jinsi mambo yanavyo endelea nchini Ukraine napata hisia maneno ya Putin yatatimia.
Sababu ya kwanza, nashiwishika kusema Russia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kushinda vita vya kiuchumi baada ya kuonekana vikwazo vina waumiza zaidi wale walio iwekea Russia vikwazo.

Sababu ya pili, kufanikiwa kuyakalia kwa muda mrefu majimbo ya Donbas na mengine yanayotaka kujitenga. Ni yale yaliyokaliwa na jeshi la Russia. Hapa nashawishika kusema malengo ya Russia yalikuwa kuyateka haya majimbo na kuyafanya yawe sehemu ya ardhi ya Urusi(Russia). Kwa mchakato wa kura ya maoni unaoendelea sasa inaonekana Russia wanaenda kufanikiwa. Sababu yakitangazwa kuwa sehemu ya Russia basi yeyote atakaye shambulia maeneo hayo atahesabika ameishambulia Russia hivyo atajibiwa kwa silaha na njia yeyote kama ilivyo elekezwa kwenye Russia Military/Nuclear Doctrine.

Sababu ya tatu, Raisi Putin kubadilishana wafungwa na Ukraine akiwemo Raia wa Ukraine ndugu Viktor Medvedchuk ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ukraine ambacho kiliongoza idadi kubwa ya wawakilishi wa bungeni kuliko chama tawala cha raisi Volodymyr Zelenskyy ambaye alikamtwa na kuwekwa kizuizini na serikali ya nchi yake. Jiulize kwanini mara nyingi Putin aliomba huyu jamaa aachiwe kwa kubadilishana wafungwa kiasi kwamba amekubali mtu mmoja raia wa Ukraine abadilishwe na askari hatari wa kinazi wa Ukraine wapato 200!! Inanoneka huyu ndio anaandaliwa kuwa kiongozi atakaye wekwa madarakani na Russia baada ya kufanikiwa kwenye kura ya maoni au baada ya kufanikiwa kumuondoa Zelenskyy.

Sababu ya nne, zoezi la kuongeza idadi ya askari kwa kuwaita askari wa akiba warudi jeshini wakajiunge na mapambano. Kama Russia akifanikiwa kwenye kura ya maoni ikatokea NATO, EU na Ukraine wakajaribu kuyavamia majimbo yaliyo jiunga Russia kutatokea vita kubwa sana na mbaya kuwahi kutokea tangu vita kuu ya pili ya dunia. Hawa askari wanatakiwa wakalinde maeneo yatakayochuliwa kwenye vita hii. Askari waliopo sasa ni wachache kuyalinda maeneo yaliyochukuliwa wakati wa vita hivi vya sasa.

Nitakuja kuongezea sababu ....
 
Swali la msingi ni; Russia imeitambua Crimea kuwa sehemu yake tangu mwaka 2014, je Crimea imeshambuliwa au haijashambuliwa?

Hayo majimbo yakishapiga kura na kujitenga yatatambulika kimataifa kama sehemu ya Russia?

Kuna mdau mmoja hapa jukwaani aliwahi kusema kwamba mtu mwoga ana Tabia ya kutoa vitisho.,na kisaikolojia ndivyo ilivyo,kwa hiyo vitisho vya Putin vinadhihirisha woga na hofu aliyonayo juu ya vita vyake alivyoanzisha huko ukraine kwamba anaelekea kushindwa

Alafu jiulize kama Kuna uwezekano wa kutumia nyukria Kuna haja gani ya kuongeza asikari wa akiba?[emoji848]
 
Habari wana JF,
Siku nyingi zimepita sijaandika mjadala(thread) humu jukwaani. Leo nimesukumwa kuandika mtazamo wangu juu ya kinachoendelea nchini Ukraine wakati huu wa vita dhidi ya uvamizi wa Urusi(Russia).

Raisi Vladimir Putin mara kwa mara amekuwa akirudia kusema malengo yote ya nchi yake kuivamia Ukraine yatatimia. Amekuwa akibezwa na kuonekana anafanya propaganda tu uhalisia ni kuwa atafurushwa Ukraine baada ya kushindwa kwa aibu. Muda huleta majibu sahihi ya mambo yote hivyo tusubiri tuone itakuwaje.

Kwa jinsi mambo yanavyo endelea nchini Ukraine napata hisia maneno ya Putin yatatimia.
Sababu ya kwanza, nashiwishika kusema Russia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kushinda vita vya kiuchumi baada ya kuonekana vikwazo vina waumiza zaidi wale walio iwekea Russia vikwazo.

Sababu ya pili, kufanikiwa kuyakalia kwa muda mrefu majimbo ya Donbas na mengine yanayotaka kujitenga. Ni yale yaliyokaliwa na jeshi la Russia. Hapa nashawishika kusema malengo ya Russia yalikuwa kuyateka haya majimbo na kuyafanya yawe sehemu ya ardhi ya Urusi(Russia). Kwa mchakato wa kura ya maoni unaoendelea sasa inaonekana Russia wanaenda kufanikiwa. Sababu yakitangazwa kuwa sehemu ya Russia basi yeyote atakaye shambulia maeneo hayo atahesabika ameishambulia Russia hivyo atajibiwa kwa silaha na njia yeyote kama ilivyo elekezwa kwenye Russia Military/Nuclear Doctrine.

Sababu ya tatu, Raisi Putin kubadilishana wafungwa na Ukraine akiwemo Raia wa Ukraine ndugu Viktor Medvedchuk ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ukraine ambacho kiliongoza idadi kubwa ya wawakilishi wa bungeni kuliko chama tawala cha raisi Volodymyr Zelenskyy ambaye alikamtwa na kuwekwa kizuizini na serikali ya nchi yake. Jiulize kwanini mara nyingi Putin aliomba huyu jamaa aachiwe kwa kubadilishana wafungwa kiasi kwamba amekubali mtu mmoja raia wa Ukraine abadilishwe na askari hatari wa kinazi wa Ukraine wapato 200!! Inanoneka huyu ndio anaandaliwa kuwa kiongozi atakaye wekwa madarakani na Russia baada ya kufanikiwa kwenye kura ya maoni au baada ya kufanikiwa kumuondoa Zelenskyy.

Sababu ya nne, zoezi la kuongeza idadi ya askari kwa kuwaita askari wa akiba warudi jeshini wakajiunge na mapambano. Kama Russia akifanikiwa kwenye kura ya maoni ikatokea NATO, EU na Ukraine wakajaribu kuyavamia majimbo yaliyo jiunga Russia kutatokea vita kubwa sana na mbaya kuwahi kutokea tangu vita kuu ya pili ya dunia. Hawa askari wanatakiwa wakalinde maeneo yatakayochuliwa kwenye vita hii. Askari waliopo sasa ni wachache kuyalinda maeneo yaliyochukuliwa wakati wa vita hivi vya sasa.

Nitakuja kuongezea sababu ....
Ili kulipa uhalali andiko lako hebu utujibu na hoja hizi pia.
(a) Hebu tuambie, kama haya ndio yalikuwa malengo ya Putin,ule msafara wa km 64 ulienda kufanya nini Kyiv;
(b) Tuambie mafanikio ya miezi nane ya Urusi kuteka maeneo nje ya Donesk na Luhansk ambayo yalikuwa yamejitenga tayari kabla ya hii vita.
(c) Kama jeshi proper imeshindwa kupata matokeo kwa wakati, je hili jeshi la akiba la amateurs litapindua meza kivipi?
(d) Hata haya maeneo yakitangazwa ni ya Urusi itabadili uwanja wa mapambano ? Lavrov alivyosema Crimea ikishambuliwa itakuwa ni judgement day, iliposhambuliwa kipi kilitokea?
 
Mkuu swala la kilomita 64 lisikuchanganye maana zile zilikua Ni mbinu tu za kumchanganya adui asijue malengo ya uelekeo wake kiufupi urusi hakua na lengo la kuichukua kiev ndo maana unaona hata mashambulizi yake makuu hayafanyii kule yeye anadili na pembezoni tu laiti Kama angekua anaitaka kiev Sasa hivi ule mji ungekua umeshachakaa Kama miji mingine na Zelensk angeshakimbia kitambo Sana
 
Unayajua malengo ya Russia kuanzisha 'oporeshni' maalumu ya kijeshi nchini Ukraine?
Tuwekee hapa kisha tuangalie yanasemaje kuhuhusu huo msafara. Kama huyajui sema tukusaidie kukuwekea hapa tamko rasmi la Raisi Putin na waziri wake wa mambo ya nje, na waziri wa ulinzi.

(b) Tuambie mafanikio ya miezi nane ya Urusi kuteka maeneo nje ya Donesk na Luhansk ambayo yalikuwa yamejitenga tayari kabla ya hii vita.
Je, baada ya kujitenga serikali ya Ukraine iliacha kuwashambulia watu wa maeneo hayo yaliyo tangaza kujitenga?
Kama haujui Russia iliingia Ukraine kwenda kuwasaidia watu wa majimbo haya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya majeshi ya Ukraine. Hii ni mojawapo ya mafanikio, pia kitendo cha kudhibiti bandari muhimu na vitega uchumi wa eneo hili imesaidia kulipunguzia nguvu jeshi la Ukraine na kuzipatia serikali za maeneo haya vyanzo cha kiuchumi kwa kuzuia pesa itokayo kwao isiende Kiev ijenge maeneo yao.

(c) Kama jeshi proper imeshindwa kupata matokeo kwa wakati, je hili jeshi la akiba la amateurs litapindua meza kivipi?
Unatumia vigezo gani kupima' jeshi proper' la Russia limeshindwa kupata matokeo wakati kabla hawaja ivamia Ukraine maeneo haya yalikuwa chini ya udhibiti wa jeshi la Ukraine na sasa yapo chini ya udhibiti wa jeshi la Russia na la wakazi wa maeneo husika wanaotaka kujitenga?

(d) Hata haya maeneo yakitangazwa ni ya Urusi itabadili uwanja wa mapambano ? Lavrov alivyosema Crimea ikishambuliwa itakuwa ni judgement day, iliposhambuliwa kipi kilitokea?
Vita imeisha na bado Crimea inashambuliwa bila majibu? Kwanini unakimbilia kufanya hitimisho wakati hali bado ni tete uwanja wa vita? Pengine kutekwa kwa neo nyeti linalounganisha Crima na maeneo mngine ya Russia na Ukraine ndiyo hukumu yenyewe kwa kitendo cha kuishambulia Crimea. Labda Ukraine wasingeishambulia Crimea mano hayo yasingetekwa.

BTW, Yale juu ni maoni au mitazamo yangu siyo sheria au mabishano ya kujifurahisha kutokana na ushabiki.
Vita siyo kama mchezo wa kufurahisha au wa burudani kama soka n.k.
Kwenye vita akili na busara vinatakiwa vizidi ushabiki na mahaba, sababu vita ina ambatana na propaganda nyingi sana kiasi kwamba ni rahisi kuaminishwa kitu kisicho sahihi au kuaminishwa uongo kuwa ukweli.
 
Kujifariji tu, malengo yametimia kwani hayo majimbo ameyadhibiti? Si bado anashambuliwa na wanajeshi kurudishwa nyuma?

Putin hataki kuweka hayo malengo yake wazi sababu anajua watu watapata kipimo cha kumpima kama kafeli au kafaulu
 
Putin ameweka malengo wazi tangu mwanzo. Tafuta utayapata.
 
Umeongea vema sana ingawa mashabiki maandazi hawawezi kukuelewa.

Me pia nna mtizamo kama wako
 
Mkuu swala la kilomita 64 lisikuchanganye maana zile zilikua Ni mbinu tu za kumchanganya adui asijue malengo ya uelekeo wake kiufupi urusi hakua na lengo la kuichukua kiev ndo maana unaona hata mashambulizi yake makuu hayafanyii kule yeye anadili na pembezoni tu laiti Kama angekua anaitaka kiev Sasa hivi ule mji ungekua umeshachakaa Kama miji mingine na Zelensk angeshakimbia kitambo Sana
Hakuwa na Lengo ? Kile kikosi hatari cha wanajeshi wa miavuli kiliangamizwa chote pale Kyiv . Eti hakuwa na malengo ya kuiteka Kyiv
 
Back
Top Bottom