Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Habari wana JF,
Siku nyingi zimepita sijaandika mjadala(thread) humu jukwaani. Leo nimesukumwa kuandika mtazamo wangu juu ya kinachoendelea nchini Ukraine wakati huu wa vita dhidi ya uvamizi wa Urusi(Russia).
Raisi Vladimir Putin mara kwa mara amekuwa akirudia kusema malengo yote ya nchi yake kuivamia Ukraine yatatimia. Amekuwa akibezwa na kuonekana anafanya propaganda tu uhalisia ni kuwa atafurushwa Ukraine baada ya kushindwa kwa aibu. Muda huleta majibu sahihi ya mambo yote hivyo tusubiri tuone itakuwaje.
Kwa jinsi mambo yanavyo endelea nchini Ukraine napata hisia maneno ya Putin yatatimia.
Sababu ya kwanza, nashiwishika kusema Russia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kushinda vita vya kiuchumi baada ya kuonekana vikwazo vina waumiza zaidi wale walio iwekea Russia vikwazo.
Sababu ya pili, kufanikiwa kuyakalia kwa muda mrefu majimbo ya Donbas na mengine yanayotaka kujitenga. Ni yale yaliyokaliwa na jeshi la Russia. Hapa nashawishika kusema malengo ya Russia yalikuwa kuyateka haya majimbo na kuyafanya yawe sehemu ya ardhi ya Urusi(Russia). Kwa mchakato wa kura ya maoni unaoendelea sasa inaonekana Russia wanaenda kufanikiwa. Sababu yakitangazwa kuwa sehemu ya Russia basi yeyote atakaye shambulia maeneo hayo atahesabika ameishambulia Russia hivyo atajibiwa kwa silaha na njia yeyote kama ilivyo elekezwa kwenye Russia Military/Nuclear Doctrine.
Sababu ya tatu, Raisi Putin kubadilishana wafungwa na Ukraine akiwemo Raia wa Ukraine ndugu Viktor Medvedchuk ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ukraine ambacho kiliongoza idadi kubwa ya wawakilishi wa bungeni kuliko chama tawala cha raisi Volodymyr Zelenskyy ambaye alikamtwa na kuwekwa kizuizini na serikali ya nchi yake. Jiulize kwanini mara nyingi Putin aliomba huyu jamaa aachiwe kwa kubadilishana wafungwa kiasi kwamba amekubali mtu mmoja raia wa Ukraine abadilishwe na askari hatari wa kinazi wa Ukraine wapato 200!! Inanoneka huyu ndio anaandaliwa kuwa kiongozi atakaye wekwa madarakani na Russia baada ya kufanikiwa kwenye kura ya maoni au baada ya kufanikiwa kumuondoa Zelenskyy.
Sababu ya nne, zoezi la kuongeza idadi ya askari kwa kuwaita askari wa akiba warudi jeshini wakajiunge na mapambano. Kama Russia akifanikiwa kwenye kura ya maoni ikatokea NATO, EU na Ukraine wakajaribu kuyavamia majimbo yaliyo jiunga Russia kutatokea vita kubwa sana na mbaya kuwahi kutokea tangu vita kuu ya pili ya dunia. Hawa askari wanatakiwa wakalinde maeneo yatakayochuliwa kwenye vita hii. Askari waliopo sasa ni wachache kuyalinda maeneo yaliyochukuliwa wakati wa vita hivi vya sasa.
Nitakuja kuongezea sababu ....