Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Wanajamvi wote tumeshuhudia mvutano mkali wakati huu wa kutunga katiba mpya ya JMT. Wengine wakitaka katiba mpya iruhusu muundo wa serikali 1, 2 ama 3. Hotuba ya Jaji Warioba ilitamka wazi kwamba serikali 3 haziepukiki, huku zaidi ya 60% ya waliotoa maoni yao kuhusu muundo wa serikali walipendekeza kuwe na serikali 3.

CCM kama chama cha siasa wao wameagamia kwenye serikali 2 kwa kile kinachosemekana kwamba wana maslahi mapana na muundo wa serikali 2.

Naomba MODS mutwekee POLL ili na sisi wana JF tupate kupiga kura kupima hasa miongoni mwetu na asilimia ngapi wanataka muundo wa serikali 1, 2 ama 3.
 
Hili jambo la serikali tatu sidhani kama linahitaji kupigiwa kura. Ni jambo la wazi kwamtu mwenye akili timamu. Tayari tunazo nchi mbili, sasa utakwepaje serikali tatu?

Siyo swala la ushabiki. There is no need to accumulate crisis. Katiba ilishavunjwa kwakuwa na katiba zinazopingana yaani ya Znz na ya Jamhuri ya Tanzania.
 
hii tumeishaimaliza na selika 3 ilishinda kwa kula nyingi tu.

Andika vizuri wewe alaaaaaaa selikali kula ndio maneno gani;;umesoma wapi halafu utakuta mnajiita Mchumi 1st class nyambafuuuuuuu;;

Ila nakubaliana na wewe Serikali Tatu ndio njia kuu,serikali mbili ni mpango wa kando au mchepuko.
 
Ili tuwe na nchi moja yenye yenye mshikamano basi inabidi Serikali iwe moja tu.
Siungi mkono huu upuuzi wa kuwa na Nchi moja yenye Serikali mbili au Tatu.
Tofauti na hapo Muungano uvunjike kila nchi ijiamulie mambo yake kivyake.
 
serikali tatu lakini kusiwe na maraisi watatu

Mimi siyo mtaalamu wa utawala au politics. Walioba anasema jeshi la ulinzi, polisi, usalama wa taifa, mambo ya nje vitakuwa chini ya Rais wajamhuri ya muungano.

1) Je kwanini hawa wengine tuwaite marais ikiwa hawanavyombo vya usalama?

2) Rais wa muungano atawezaje kumiliki vyombo vya usalamana mambo ya nje bila fedha? Unaendesha jeshi kwa hela ya kuomba kutoka kwawashirika?

Huwa naamini Rais anakamilika akiwa na fedha na vyombo vya usalama
 
Hili jambo la serikali tatu sidhani kama linahitaji kupigiwa kura. Ni jambo la wazi kwamtu mwenye akili timamu. Tayari tunazo nchi mbili, sasa utakwepaje serikali tatu?

Siyo swala la ushabiki. There is no need to accumulate crisis. Katiba ilishavunjwa kwakuwa na katiba zinazopingana yaani ya Znz na ya Jamhuri ya Tanzania.

Watanganyika mlipokuwa mukiyaongeza mambo ya muungano kutoka 11 hadi kufikia 32 je hamjavunja muungano?nyerere alipoifuta tanganyika hajavunja muungano?zanzibar kwanza.
 
Back
Top Bottom