KURA YA MAONI: MUUNDO UPI WA MUUNGANO UNAFAA?
Muundo wa Muungano unaofaa ni wa
SERIKALI MOJA
Sababu kwa nini Muundo wa Serikasli Moja unafaa ni kama ifuatavyo:
[*=1]Lengo la awali la Muungano halikuwa kuanzisha ushirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar, bali kuunganisha hizi nchi mbili kuwa nchi moja - Katiba ya M Tanzania
uungano inatamka kuwa Tanzania
ni nchi moja; baada ya Muungano jina la nchi hiyo mpya likawa
Tanzania; Mkuu wa Serikali ya TanZania Visiwani (Zanzibar) akabaki kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na
Makamu wa kwanza wa Rais (wa Muungano); kiongozi wa Serikali; Mkuu wa Serikali ya Tanzania Visiwani (kwa kutambuliwa kwamba ni kiongozi wa sehemu ya nchi moja) alitumia bendera ya Muungano na wimbo uleule wa Taifa.
2. Serikali moja itaondoa kile kinachoitwa kero za Muungano kwa sababu mambo yote ya Serikali yataendeshwa kwa pamoja na hivyo hakutakuwa na upande utakaovaa koti la Muungano - koti hilo la Muungano litakuwa limevaliwa kwa usawa, kwa maana hiyo hakuna upande utakaojihisi kuwa unamezwa.
Mfano, watu wawili wakiamua kupika chakula kwa pamoja na wakapaukuwa katika sahani moja na kula pamoja hakuna atakayemlalamikia mwenzake kuwa amempunja; lakini wakipakuwa katika sahani mbili, ni rahisi kujitokeza hisia za kupunjana.
3. Serikali moja itapunguza mzigo wa uendeshaji ikilinganishwa na mzigo ambao nchi itaubeba kuendesha serikali mbili au tatu.