Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
kama hatuna uchu wa madaraka, umimi na unafk, serikali moja (1) is the BEST OPTION....................
 
mimi sioni kama kutakuwa natatizo kwa upande wa tanzania bara ikiwa muungano utavunjika! Maana wazanzibar waliuomba wenyewe huu muungano! Nataka muundo wa tanganyika huru na zanzibari yao hainashda kabisa.
 
KURA YA MAONI: MUUNDO UPI WA MUUNGANO UNAFAA?

Muundo wa Muungano unaofaa ni wa SERIKALI MOJA
Sababu kwa nini Muundo wa Serikasli Moja unafaa ni kama ifuatavyo:

  1. [*=1]Lengo la awali la Muungano halikuwa kuanzisha ushirikiano baina ya Tanganyika na Zanzibar, bali kuunganisha hizi nchi mbili kuwa nchi moja - Katiba ya M Tanzania
uungano inatamka kuwa Tanzania ni nchi moja; baada ya Muungano jina la nchi hiyo mpya likawa Tanzania; Mkuu wa Serikali ya TanZania Visiwani (Zanzibar) akabaki kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa kwanza wa Rais (wa Muungano); kiongozi wa Serikali; Mkuu wa Serikali ya Tanzania Visiwani (kwa kutambuliwa kwamba ni kiongozi wa sehemu ya nchi moja) alitumia bendera ya Muungano na wimbo uleule wa Taifa.
2. Serikali moja itaondoa kile kinachoitwa kero za Muungano kwa sababu mambo yote ya Serikali yataendeshwa kwa pamoja na hivyo hakutakuwa na upande utakaovaa koti la Muungano - koti hilo la Muungano litakuwa limevaliwa kwa usawa, kwa maana hiyo hakuna upande utakaojihisi kuwa unamezwa. Mfano, watu wawili wakiamua kupika chakula kwa pamoja na wakapaukuwa katika sahani moja na kula pamoja hakuna atakayemlalamikia mwenzake kuwa amempunja; lakini wakipakuwa katika sahani mbili, ni rahisi kujitokeza hisia za kupunjana.
3. Serikali moja itapunguza mzigo wa uendeshaji ikilinganishwa na mzigo ambao nchi itaubeba kuendesha serikali mbili au tatu.
 
nataka tatu ikishindikana basi iwe moja tu, 7bu kero nilizozisoma hapo juu zizani kama zitatuliwa na muundo wa s2.
 
Tutabishana kwa mambo yasiyo ya maana wabunge ni WAWAKILISHI TU ikiwa wameshindwa kufanya tulichowatuma Kufanya kama WAWAKILISHI ni bora waturudushie mchakato huo WENYEWE TUPIGE KURA tuwaonyeshe nn tuna taka
lakini kwa kuwa wanatumia mabavu na collapse system zao watakataa na kutokubaliana na matokeo ya kura za wananchi wakumbuke hawajaenda kuonyesha
i) interest za u chadema, cuf wala u ccm
ii) Uislam wala Ukristo
iii) uzanzibar wala Utanganyika
Tunachotaka ni TANZANIA ya miaka mingi ijayo isiyo na matatzo kama yaliyopo sasa wakumbuke wao hawatakuwepo lakufanya
serikali mbili zimeonyesha Udhaifu kwenye muungano ikiwa serikali tatu zitatatua madhaifu hayo sawa ila HAKUNA KISICHO NA MADHAIFU hapa duniani lakini pia HATA CHENYE UDHAIFU KINA MEMA YAKE SASA Tutajuaje kipi kinatufaa ni kwa kuangalia mema kuliko madhaifu, chenya mema mengi kuliko madhaifu ndicho kinacho tufaa. ref ''concept of utilitalianism" Acheni hayo wekeni Uzalendo mbele na si mala zote wengi wape ingekuwa hivyo Nyerere asingekubali mfumo wa vyama vingi maana wengi waliukataa tukiogopa serikali tatu eti ni gharama wkt una mema mengi na eti kwa sababu wengi hawautaki si jambo jema hata kidogo
 
kama maana ya muungano ni kila nchi kusurender mamlaka yake na kujenga nchi 1 kama ilivyofanya Tanganyika basi na iwe hivyo kw ZNZ. kwa hiyo muundo sahihi wapaswa kuwa SERIKALI 1

Asante kwa kuwa na mawazo Kama yangu
 
Serikali 3. Mimi naunga mkono sababu zilizotolewa na Tume ya Warioba iliyokuwa imesheheni wasomi, maprofesha na madaktari wenye upeo wa hali ya juu.
 
Miungano ya hiyari kama wetu yote imevunjika na kwa kejeli na ubaguzi walionao ndugu zetu wazanzibari kuondoa hizo zinazoitwa kero ni vigumu. Mimi nadhani umefikia wakati muungano huu tuuvunje kwa amani kama walivyofanya Chekosolovakia. Tuweke muda wa mpito wa miaka miwili kila ajiandae.
 
Serikali 3 ndio suluhisho ya kero za muungano


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Serikali moja yenye majimbo mawili Tanganyika na zanzibar
 
mimi naona serikali tatu ni suruhisho pekee kwa sababu Zanzibar tayari walishavunja muungano kwahiyo itakuwa ni kujindaganya kuendelea na mfumo wa sasa labda wazanzibari warudi wakasahihishe hilo kwanza. Vingenevyo nitatizo kubwa.
 
Serikali 3. Sababu kubwa ni kwamba wazanzibari wamekuwa na serikali yao kwa muda mrefu na hawaezi kukubali kukabithi mambo yao yote kwa serikali ya muungano. Hivyo ili kuleta usawa, iwepo serikali ya muungano ianyojitegemea kama mapendekezo ya tume ya warioba, na serikali ya tanganyika irudi kama zamani.
 
Pendekezo langu ni serikali 3 na Profesa Kabudi keshafafanua uzuri sana sababu ya kuwa nazo ktk
kongamano la katiba na muungano zanzibar.
 
Pendekezo langu ni serikali 3 na Profesa Kabudi keshafafanua uzuri sana sababu ya kuwa nazo ktk
kongamano la katiba na muungano zanzibar.

Mkuu wengi tunakuunga mkono lakini kumbuka wabunge wengi ni wa CCM na wanataka serikali mbili hapa tutafanyaje wakati asilimia kubwa ya waTanzania tuko nje ya Bunge?
 
Mkuu wengi tunakuunga mkono lakini kumbuka wabunge wengi ni wa CCM na wanataka serikali mbili hapa tutafanyaje wakati asilimia kubwa ya waTanzania tuko nje ya Bunge?

Kupita kwa Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanznia hakuhitaji wingi wa uwakilishi wa ubunge upande wa chama tawala ccm,bali watanzania wote wana haki ya kuipigia kura kwa kukubali au kukataa na sio wingi wa wabunge wa ccm.Idadi ya wabunge wa ccm ndani ya bunge la katiba ni sawa na wanachama milion sita tuu ya watanzania,watanzania wengine hawana chama na kiasi kikubwa wanaunga mkono mawazo ya tume ya Warioba.
 
Naunga mapendekezo ya Tume ya Warioba la sivyo kama tumeungana kikwelikweli tuwe na serikali moja, Unguja iwe mkoa na Pemba iwe mkoa.
 
Back
Top Bottom