NderianangaUmmy
Member
- Mar 2, 2015
- 5
- 1
wanajf kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa jf kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?
1.serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.serikali tatu.
N:b ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi
===============
shida si muungano.
Nionavyo mimi ni kutokuwepo kwa uwazi kuhusu muungano unaosababisha kuonekana kwamba kuna unyonyaji fulani.
Ndoa zinatengana itakuwa muungano usio na tija?????
Kwani ussr iko wapi?????
tatu,au moja
Tatu,au moja
Serikali tatu sababu zangu ni sawa na zile za Jaji warioba za kitaalamu zaidi.
😛eace: 2 TU ZATOSHA!!!!
serikali tatu...Sababu alishaeleza warioba
Huoni kwa sasa kuna watu hawaridhiki...anyway ulisoma hesabu za seti?
Achana na mambo ya Muundo wa Muungano katika kipindi hiki. Nenda kwanza kajiandikishe kupiga kura kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Masuala ya Muundo wa Muungano yalijadiliwa sana katika Bunge Maalum la Katiba ambalo nina hakika hukulisikiliza na hukujua kama lilikuwepo kwa maana kipengele hiki kilijadiliwa na maamuzi yake kufikiwa. Labda kwa kukusaidia muundo ni wa Muungano unaoundwa na serikali mbili. Soma Katiba Inayopendekezwa na usichanganye madawa kwenye forum. Kwa heri.3. Serikali 3
Wewe si ulifungiwa au kifungo umemaliza. Pole karibu kwenye forum lakini zamu hii uwe makini usije ukarudi gerezani.ASANTE KWA USHAURI WAKO NA MUHIMU WASOME HAPA
Uhusiano na Uratibu wa Mambo ya Muungano (Ibara za 127 – 128)
Katiba Inayopendekezwa inaimarisha Muungano wetu kwa kuanzisha Tume ya Usimamizi na Uratibu wa Mambo ya Muungano. Chombo hiki, pamoja na mambo mengine, kitakuwa na jukumu la kukuza na kuratibu ushirikiano baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Mojawapo ya malengo ya uratibu huu ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Serikali hizi mbili na kukuza kiwango cha utoaji huduma kwa wananchi wote.
Kwa utaratibu wa sasa ipo Kamati inayoshughulikia masuala ya Muungano ambayo inaongozwana Makamu wa Rais. Kwa Katiba Inayopendekezwa chombo hiki sasa kitakuwa na nguvu ya kisheria na hivyo kuweka mfumo madhubuti zaidi wa kushughulikia changamoto za Muungano na pia kuratibu masuala mengine yanayohusiana na ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kwa ujumla wake.
Achana na mambo ya Muundo wa Muungano katika kipindi hiki. Nenda kwanza kajiandikishe kupiga kura kuhusu Katiba Inayopendekezwa. Masuala ya Muundo wa Muungano yalijadiliwa sana katika Bunge Maalum la Katiba ambalo nina hakika hukulisikiliza na hukujua kama lilikuwepo kwa maana kipengele hiki kilijadiliwa na maamuzi yake kufikiwa. Labda kwa kukusaidia muundo ni wa Muungano unaoundwa na serikali mbili. Soma Katiba Inayopendekezwa na usichanganye madawa kwenye forum. Kwa heri.