Hiyo Katiba uliyosoma imeeleza jinsi nchi iliyoitwa Tanzania ilivyopatikana. Ni kwamba mwaka 1964 Serikali za nchi mbili ( Tanganyika na Zanzibar) zilikubaliana kuunganisha ardhi na serikali zao ziwe kitu (entity) kimoja. Kwa lugha rahisi nchi hizo, zikiwa huru, na pasipo kulazimishwa na mamlaka yo yote, ziliamua kuchanga ardhi zao kuunda nchi moja iliyoitwa Tanzania, chini ya serikali moja iloyoitwa Serikali ya Muungano. Lakini kwenye miaka ya 80, Zanzibar iliamua kuondoa ardhi yake kwenye muungano, na ikajirudishia mamlaka ya Serikali yake nje ya Muungano. Kwa kufanya hivyo ilikiuka makubaliano, na hivyo Muungano ulivunjika. Leo kujadili muundo wa serikali bila kutambua kwamba Muungano ulivunjika Zanzibar ilipojitenga ni kupoteza muda na kufuata matakwa ya MUUNGANO WA VYAMA VYA ASP NA TANU (CCM) ya kulazimisha kwamba Tanganyika ndiyo Muungano. Na hii yote ni kwa sababu bila Muungano wa nchi MUUNGANO WA VYAMA (CCM) hauna kazi, kwa sababu mwaka 1977 Chama cha Zanzibar (ASP), na Chama cha Tanganyika (TANU) vilikubaliana kuungana iliMuungano huo uongoze Serikali ya nchi (Tanzania) iliyotokana na kuungana kwa nchi zao. Hivyo bila Muungano wa nchi, Muungano wa vyama hauna maana kwa sababu hakutakuwapo Serikali utakayoiongoza. KWA HIYO KAMA TUNATAKA KUREJESHA MUUNGANO TENA, MUUNDO WA SERIKALI KWA HALI ILIVYO SASA NI LAZIMA IWE SERIKALI TATU - Serikali ya Zanzibar (ambayo tayari ipo); Serikali ya Tanganyika (ambayo itabidi iundwe); na Serikali ya Muungano (ambayo nayo itabidi iundwe).