Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Narudia tena serikali tatu ni mzigo kwa watanzania tukishindwa serikali moja, bora kugawana fito. Hizi bra bra za serikali tatu. Ni hira za wanasiasa.
Tanzania hatujawahi kuwa na serikali moja,sema serikali mbili zinatosha.
 
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 inasema kuwa maoni ya kutokuwepo kwa Muungani ni marufuku! Wewe unazungumzia "Nchi Mbili Huru" maana yake hakuna Muungano! Just imagine zile States za Marekani kila State moja iwe na kiti UN ku-represent nchi moja (USA) Sijui kwa nini suala la Muungano linawafanya watu ku-lose focus kiasi hiki!
Na hilo la ku-refer Katiba ya JMT, 1977 ni sawa kwa kuwa ndio inayotumika, au ulitaka nirejee rasimu ya Katiba Mpya? Be serious, plse!
Ni kwamba watu wanatamaa ya Uongozi. Ila kimsingi hakuna unuhimu wa kua na Serikali 3.

Kama tunataka Muungano ulio qa kweli, Serikali ni Moja ila iwe ya Majimbo ku deligate power kwa wazawa wa sehemu husika.

Serikali 3 ni kutaka kugawana Madaraka na posho tu hakuna kipya.

Niko palee nawasubiri
 
Ndugu mtanzania

Toa sababu za kitafiti, Kwa nini unasema Serikali Moja ?
MiMi naongelea kiuchumi zaidi.
Hivi hii pesa ya serikali ya tatu si ingesaidia kuwaajiri walimu kujenga maabara na karakana ili kuongeza ubora wa elimu? Kuna nini zaidi kipya zaidi ya kuongeza fursa kwa wanasiasa. Kirusi cha yote haya ni wanasiasa ambao wanajali matumbo yao baada ya kufikiria jinsi gani kuikwamua nchi ilipo wakati miaka ya 80 uchumi ulikuwa sawa na nchi kama Malaysia na Indonesia.
 
Nikama wanaforce sherehe hizi za muungano lakini hawako wazi na maendeleo, Siasa ndio zinawaumiza
 
Sababu kiuhalisia wanaopigania serikali tatu ni wanasiasa tu, wanalinda vyeo na madaraka yao. Mfano ukienda zanzibar, ukaangalia mikoa na wilaya zilivo ni usanii tu, kutoka mwenge hadi ubungo mataa tayari ni mikoa miwili na wilaya zake, zenye mamlaka kamili. Mimi kwangu ni usanii tu huu wa kulindiana chakula, na vyeo na sababu wananchi kwenye mada hii tunaamuliwa na wanasiasa/walinda vyeo bhasi tunabusruzwa tu tupiganie vyakula vyao. Hata wanaosema sejui mamlaka kamili ya Tanganyika, inakusaidia nini kama mwananchi wa kawaida?, ni vyeo tu vya watu na matamanio yao. Kwahiyo serikali iwe moja tu, na swala la muundo wa muungali lisiwe mada kubwa kuliko zote kwenye katiba mpya. Kuna mambo mengi mengine ya muhimu yanayohusu maisha na maendeleo ya watu wa kawaida.
 
1 Serikali ya Tanganyika
2. Serkali ya Zanzibar na
3 Serikali ya SHIRIKISHO
Hata hivyo Wananchi waamue kwa REFERENDUM maana kilichopo kiliamuliwa na watu wawili MMOJA mwenye MA Degree na mwingine Baharia sijui kama alikuwa ameusomea au by experience
KUELEKEA serikali moja Zanzibar itasema INAMEZWA
Serikali 2 ndo hizi zenye gharama ya kutatua kero
 
Leo nilikuwa napitia hapa katiba hii ya kiingereza nikakuta hivi.

"Mainland Tanzania" means the whole of the territory of the United Republic which formerly was the territory of Republic of Tanganyika.

"Tanzania Zanzibar" means the whole territory of the United Republic which formerly was the territory of People's Republic of Zanzibar and which was Previously referred to as "Tanzania Visiwani".

Sasa ukichunguza vizuri utaona ni kuwa Tanganyika ilipoteza mamlaka yake huku Zanzibar ikibaki na mamlaka yake na kupata kofia mbili juu yaani jina lake limebaki na bado ina serikali yake huku Tanganyika ikipoteza vyote.

Huu kweli utaitwa ni muungano ?
 
Kura ya maoni (referendum) inapitishwa na bunge lenye kuwakilisha wananchi wanopiga kura hiyo, haiitishwi na Putin na kusimamiwa na jeshi lake.
 
Kura ya maoni (referendum) inapitishwa na bunge lenye kuwakilisha wananchi wanopiga kura hiyo, haiitishwi na Putin na kusimamiwa na jeshi lake.

Kwanini Putin, na si Trump na jeshi lake!
 
Kwanini Putin, na si Trump na jeshi lake!
Putin ndiye bingwa wa kunyang'anya ardhi ya jirani kwa kutumia jeshi lake halafu jeshi hilo linapitisha kura ya maoni kwa mtutu wa bunduki na yeye kuhitimisha kwa kusema kuwa walifanya referendum na raia wa eneo hilo kuamua kujiunga urusi. Hebu angalia: Chechnya, Transnistria, Crimea, Donbas, Donestki, Abkhazia, South Osettia. Kote huko Putini aliingiza jeshi kwa mabavu, halafu akadai wananchi walipiga kura ya maoni.
 
Hiyo Katiba uliyosoma imeeleza jinsi nchi iliyoitwa Tanzania ilivyopatikana. Ni kwamba mwaka 1964 Serikali za nchi mbili ( Tanganyika na Zanzibar) zilikubaliana kuunganisha ardhi na serikali zao ziwe kitu (entity) kimoja. Kwa lugha rahisi nchi hizo, zikiwa huru, na pasipo kulazimishwa na mamlaka yo yote, ziliamua kuchanga ardhi zao kuunda nchi moja iliyoitwa Tanzania, chini ya serikali moja iloyoitwa Serikali ya Muungano. Lakini kwenye miaka ya 80, Zanzibar iliamua kuondoa ardhi yake kwenye muungano, na ikajirudishia mamlaka ya Serikali yake nje ya Muungano. Kwa kufanya hivyo ilikiuka makubaliano, na hivyo Muungano ulivunjika. Leo kujadili muundo wa serikali bila kutambua kwamba Muungano ulivunjika Zanzibar ilipojitenga ni kupoteza muda na kufuata matakwa ya MUUNGANO WA VYAMA VYA ASP NA TANU (CCM) ya kulazimisha kwamba Tanganyika ndiyo Muungano. Na hii yote ni kwa sababu bila Muungano wa nchi MUUNGANO WA VYAMA (CCM) hauna kazi, kwa sababu mwaka 1977 Chama cha Zanzibar (ASP), na Chama cha Tanganyika (TANU) vilikubaliana kuungana iliMuungano huo uongoze Serikali ya nchi (Tanzania) iliyotokana na kuungana kwa nchi zao. Hivyo bila Muungano wa nchi, Muungano wa vyama hauna maana kwa sababu hakutakuwapo Serikali utakayoiongoza. KWA HIYO KAMA TUNATAKA KUREJESHA MUUNGANO TENA, MUUNDO WA SERIKALI KWA HALI ILIVYO SASA NI LAZIMA IWE SERIKALI TATU - Serikali ya Zanzibar (ambayo tayari ipo); Serikali ya Tanganyika (ambayo itabidi iundwe); na Serikali ya Muungano (ambayo nayo itabidi iundwe).
 
Back
Top Bottom