Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Hapa tutapiga kelele buuuure wenye kisu ndo wanaokula minofu...kW nn unajua hata mkipendekeza VP ishapangwa iwe ivo na Dhana ya ushirikishwaj inaletwa km kuwapiga changa la macho...mwisho wa cku waamuz ni waoooo
 
Jibu ni 1 au 3 baada ya 2 kushindwa. Muungano safi na imara utatokana na utashi huru wa watu au wananchi wa pande mbili na siyo ngivu ya dola.
 
(1) Serikali moja ya jamuhiri ya muungano wa Tanzania

au

(2) Serikari mbili yaani serikari ya Zanzibar na serikari ya Tanganyika, huku tukiwa na umoja wa Tanzania.

Sawasawa.Tuwe na Serikali moja tu ya Tanzania, huku Zanzibar ikiwa ndani ya Tanzania (kama ilivyo Mafia au Kigamboni) Alternatively, Muungano ufe na tuwe na separate Governments - Tanganyika na Zanzibar. Zanzibar wanaweza kuwa majirani zetu wema tu kama ilivyo Malawi, Burundi na Congo.

Huu uwongo wa miaka nenda rudi kwamba tunaweza kuvamiwa na maadui zetu kama tukiiachia Zanzibar hauna mantiki yoyote. Mbona maadui hawajatuvamia kwa kutokea DR Congo (through Ziwa Tanganyika) au Kutokea Malawi (through Ziwa Nyasa)?
 
Kutokana na nilivyomuelewa Jaji Warioba.
Lengo la Mwl. Nyerere ni kuitoa nchi katika nchi moja yenye serikali mbili kwny Tanzania moja yenye serikali moja.

Na alifanya hvy kwa vitendo kwa mazungumzo, tena kwa kufuata katiba. Ndiyo maana Jaji anaaema akiwa anatoka madarakani aliacha mmb ya muungano yakiwa zaidi ya 20 lakini alipoondoka na ss yameounguzwa tena ya Muhimu kbs.

Lkn kama hiyo haitoshi Zanzibar wakavunja katiba na kutunga katiba nyingine, ambayo kimsingi inapingana kabisa na Katiba ya Tanzania.

Watanzania wanahoji huko ndo kwenda kwny nchi moja yenye serikali moja? Matatizo ya muungano hayajashughulikiwa kwa ukamilifu na umuhimu wake. Zanzibar kwa sababu yoyote hawajaacha kulalamikia Muungano huu.

Na kwsbb kwa maana yyt Serikali hii imeshindwa kushughulikia hili kwa uzito wake. Imeweka nchi katika wakati mgumu sana.

Je Zanzibar iko tayari kurudi ilikotoka kwa hali ilivyo? Wote tuna jibu la swali hilo. Kama inawezekana basi serikali i-act sasa. Ila haiwezi.
Mambo yameenda mbali tayari.

Busara itumike sasa kuifanya nchi iwe moja na amani iendelee.
Kwa maelezo hayo. Mimi naunga mkomo wazo la Serikali tatu.
 
Waasisi waasisi kwani wao ni MUNGU eti walilopanga halibadiliki,,,,"Nyerere katika baadhi ya hotuba zake alikili kufanya madudu na akashangazwa na viongozi wanaochukua na kukariri Madudu na kuacha vya msingi,,,"Muungano tunautaka lakini kwa Serikali 3,,"Over.
 
waungwana ccm siku zote inacheza na akili za watu, inagawa watu katika makundi kisiasa na kidini na inafanikiwa itafutwe njia ya watu kuacha lengo kuu na kufuata lengo mahsusi
 
Kwa nini swali liwe muundo upi wa muungano unafaa na si kama muungano unafaa?
 
Back
Top Bottom