Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Masuala ya ardhi ya Zanzibar hayana tija kabisa kuifanya iwe ya wazanzibar wenyewe na isiwe ya Muungano.
Japan ni kakisiwa kadogo sana lakini kana idadi kubwa zaidi ya mara kumi ya Tanzania .Sasa iweje Zanzibar iwe na hofu ya watanganyika kuishi Zanzibar?
Tatizo sio ardhi .,ni kwamba wazanzibar hawataki mila,desturi na dini za makabila mengine huo ndio ukweli unaofichwa fichwa.
Tanganyika huo ubaguzi haupo hata Muungano ukivunjika achilia mbali kuwa wa serikali tatu.Hata ukiangalia ulaya hizi nchi zenye kutumia mila za kiarabu watu wake wamejaa ulaya lakini wao hawapendi watu wa ulaya waishi kwao.
Ni tatizo ambalo halisahabishwi na aina ya Muungano bali ni hulka za watu.
 
WanaJF Kwa mda mrefu sasa kuelekea utungaji wa katiba mpya kumekuwa na mjadala mkali kuhusu muungano wetu uwe wa muundo upi sasa ningependekeza tuwe na kura ya maoni hapa JF kuhusu muundo wa muungano, upi ni muundo sahihi?

1.Serikali moja.
2. Serikali mbili.
3.Serikali tatu.


N:B ukiweza kutoa sababu za muundo wa muungano unaoutaka itakuwa vizuri zaidi

serikali tatu inatufaa kwa sasa ili haki itendeke sawa
 
serikali 2 na muungano wa mkataba
Serikali inayohitajika ni MOJA TU.
Ukiangalia sana utaona ni nini chanzo cha hisia zinazo tukabili za kutaka serikali tatu huu ndio mwanzo wa umoja wetu kubomoka.
Muungano tulio nao ni moja ya hali za utaifa amabo ni wa kipekee, serikali mbili hazija tosheleza maswala ya umoja huu kikamilifu ndio maana kuna hisia za kujadili tena muundo upi wa serìkali unafaa.
Utofauti unao tuingia kimawazo unatokana na fikra potofu za kutokuwa na imani ya umoja wetu, sasa ni miaka hamsini ya umoja huu na tunacho jadili wakati huu tusipokuwa waangalifu tutafika pabaya sana na tutachekwa na dunia nzima. Macho ya dunia yanatuangalia na umoja wetu unamengi sana ambayo ni mazuri lakini hatuyaoni haya. Tutakuja kuyaona hapo baadae kama tutaendelea na udhaifu tunao uonyesha sasa wa kutokuwa na uamuzi wa maana ambao utatulinda kwa miaka mingi itakayo kuja.
Tufikirie kwa upana na marefu jinsi tunavyo jadili swala hili la muungano, maswali tunayojiuliza sasa majibu yake yako yapo machoni mwetu, MUUNGANO=UMOJA=SERIKALI MOJA tufikrie sana jambo hili.
Mister-G
 
Hivi serikali ya Tanzania ardhi yake ni ipi kwa sasa. Naona wazo lako ni zuri hivyo hata raisi hana ardhi maana amekaa kwenye aardhi ya mkoa, na mkuu wa mkoa aondolewe maana hana ardhi, amekaa kwenye ardhi ya wilaya na mkuu wa wilaya hana ardhi amekaa tarafani, afisa tarafa halikadhalika amekaa katani wakati ofisi za kata zipo kwenye ardhi za vijiji na mitaa. Kumbe nchi iwe ya vijiji na mitaa tu maana ndio wenye ardhi
 
ni serikali tatu tu
kwani haiwezi kuwa nchi mbili zilizoungana lakini kukawepo serikali mbili
ni lazima kuwepo kwa serikali ya kila nchi na baadae kuwepo na serikali hiyo inayoitwa ya muungano
kuwepo kwa serikali mbili ni kuonyesha wazi kuwa lazima kutakuwepo na unyonyaji wa upande mmoja wa muungano huo na nchi nyengne kutumia madara ya serikali mbili

hivyo ni lazima kwa nchi kama Tanzania kuwepo kwa muungano wa serikali tatu ili kuwepo na usawa kwa pande zote mbili


AHSANTE
 
Mbona serikali moja haipigiwi kelele sana? Kwangu mm napenda serikali MOJA. Tu.
 
Zanzibar wanatupotezea muda
Kwa nini hawaelewani wakaja na msimamo mmoja?.
Hawa wamelogwa au wanapenda kubebwa?
Nadhani hawajuwi utawala kitu gani .Wanahofu kuendesha nchi yao kwa pamoja,
HUU MCHEZO WA KUIGIZA AU WAKO SERIOUS?
 
serikali mbili maana tangu muungano hadi leo hii tanganyika haipo kuna zanzbar na tanzania viongozi tanganyika hipo wapi
 
serikali 2 ndo mpango mzima kwani faida zake na gharama za uendeshaji wake haulinganiki na ule wa serikali 3.ni ukweli usiopingika kuanzisha serikali ya 3 kutaongeza gharama na kuudhoofisha umoja wa kitaifa kiuchumi na kisiasa ikitokea serikali ya 3 ikaanguka
 
Back
Top Bottom