Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Watanzania mnatoana macho bure kumbe ni kukosa uelewa.
Muundo wa Serikali 2 uliodumu kwa miaka 50 unawezekana kwa mfumo wa chama kimoja ambapo watu wanafungiana chumbani wanakubaliana lolote na wanavumiliana. Lakini kwa mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi mfumo huu wa serikali 2 hauwezi kudumu hata miaka 10 ijayo. Jinsi upinzani unavyozidi kupata ushawishi na ujasiri wa kusema ukweli ndivyo muugano wa serikali 2 utakuwa mashakani na hatari yake ni kuvunjika kabisa. Kwa hali hii Tume ya Jaji warioba ilifanya maamuzi sahihi na ya busara sana kwa maslahi ya Taifa letu ila bahati mbaya sana wapenzi wa ccm wamepata mashaka na wasiwasi hawapendi mfumo huu. Lakini kibaya zaidi hawataki kujifunza wala kuelewa ni ubishi usio na Tija au labda ni kwa sababu JK aliwaelekeza hivyo.
 
Hivi jamani nataka kufahamu zaidi maana bado nipo njia panda.

Hivi kwa nini Ukawa wanaing'ang'ania serikali tatu??
Na tayari imekwa wazi kuwa ni gharama??

Kama serikali tatu ni gharama basi hata serikali mbili na gharama pia..

Kwa nini tusiwe na serikali moja???

Ni maswali ya mtazamo ndani yake
 
Kwa Watanganyika na Wazanzibari

Mimi ninataka serikali mbili tu na hivi

1. Serikali ya tanganyika
2. serikali ya zanzibar

hakuna haja ya kuendeleza muungano usiokuwa na faida kwa pande zote mbili

muungano ulikuwa wa nyerere na karue na wao wamekufa huu muungano uko hai unafanya nini?

Mzanzibar Huru
 
Serikali tatu ili kuonesha usawa wa nchi zote tofouti iliyoposasa ni wapo ambao hawa nufaiki na muungano huu let be open
 
Kwa Watanganyika na Wazanzibari

Mimi ninataka serikali mbili tu na hivi

1. Serikali ya tanganyika
2. serikali ya zanzibar

hakuna haja ya kuendeleza muungano usiokuwa na faida kwa pande zote mbili

muungano ulikuwa wa nyerere na karue na wao wamekufa huu muungano uko hai unafanya nini?

Mzanzibar Huru

Mkuu nakuunga mkono, kuona unatambua kuwepo kwa Tanganyika na Zanzibar kama nchi. Ila hapa moja kwa moja tayari utakuwa umeua/umevunja MUUNGANO ambao ndio uliozaa TANZANIA baada ya kunganisha baadhi ya herufi za nchi hizi mbili. Je kama unataka hivyo uoni tayari kola nchi itakuwa imejitenga? Mimi ni muumini wa nchi moja TANZANIA, Zanzibar iwe ni sehemu ya Tanzania igawanywe kwenye mikoa. Liwepo bunge moja la TANZANIA, Serikali moja name Rais awe mmoja. Hapa ugomvi utaisha.
 
ayaaaaa imefungwa kabla mimi sijapiga.. mimi nainga mkono serikali 3
 
#Okinawa .. Zanzibar ni nchi kutokana na katiba yao ya mwaka 2010 which means hawaezi kukubali Serikali moja wala mbili na wanachoshinikiza ni muungano wa mkataba au Serikali tatu ili nayo pia iwe na mamlaka kamili katika masuala ya utawala na umiliki wa rasilimali.

Nadhani mfumo wa serikali tatu ni mgeni kwa wengi na unaonekana hautzkuwa na tija wala ufanisi hasa kwa watendaji kimuundo wa uongozi, napendekeza serikali moja tu.
 
serikali mbili, serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar NO MORE MUUNGANO, R.I.P Tanzania though the name was beautiful but old Tanganyika is the best
 
Back
Top Bottom