Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Mimi binafsi napenda serikali tatu kwa sababu zifuatazo.
1. Kabla ya maridhiano ya mwaka 1964 hizi nchi mbili zilikuwa ni nchi huru zenye dola zake.
2.Wakati wa maridhiano wananchi hawakuhusishwa kikamilifu juu ya huu muungano kwa pande zote 2, walio husika ni viongozi wa serikali tu kutokana na utashi wao.
3. licha ya makubaliano ya vitu ambavyo viliainishwa kuwa vya muungano kwa sehemu kubwa vimekuwa vikikiukwa na kila upande wa muungano unaamua kivyake pasi kufuata katiba ya muungano.
4.Siasa ndo imeumiliki muungano wa s2 na si uhalisia wa watu.
5.Ili kuwa na Muungano imara kwa sasa ni huu wa shirikisho ambao unatambua mamlaka kamili ya hizi nchi 2 na hivyo kutengeneza muungano wenye kukidhi matakwa ya kikatiba na si kama ilivyo sasa.

Hasara za kutofuata muundo ya s2 au s1.
kwa upande wangu sioni kama kuna hasara yoyote inayo weza jitokeza kwa kutofuata miundo hiyo. kwa kuwa miundo hiyo inachangamoto nyingi na kubwa ikiwemo kutokukubaliwa na wananchi wengi.
 
Serikali tatu (3) ndio suluhu ya matatizo ya Watanzania.Serikali mbili tunadanganyana
 
Tanganyika mhimu kwetu.km zanzibar ilivyokua mhimu kwa wazanzibar then tukutane kwenye muungano
 
Serikal tatu ndio suruhishi maana itareta usawa wa kira pande ina itaondoa mtafaruku na marumbano yaliyopo kwa sababu wazanzibar wanataka nchi yao na watanganyika tunataka nchi yetu tunataka serikal tatu ni kwa ajili ya kuuenzi muungano na viongoz wetu wario tutangulia, bira hivyo ilikuwa kira nchi ibaki na chake, alafu niwashangae kidogo ndugu zangu wanao mg'ang'ania serikal mbili sijui ninani kawaroga! Hainiingii akilini kwamba mtu unaerim yako ya kutosha unashindwa kung'amua mambo madogo kama haya binafs nakuwa na wasiwawas na erim zao, zanzibar ina kila kitu chake kasoro ni fedha tu!Sasa pana muungano gani hapa?
 
Mimi huwa naamini katika umoja, kwa mambo mengi ya msingi hasa ya maendeleo. Hivyo basi muungano ni jambo jema kwa Taifa letu na Afrika kwa ujumla wake. Kwa hiyo ningependa kama leo tungekuwa tumekamilisha nchi moja yenye serikali moja ya watu wa Tanzania. Lakini ukweli uliopo ni kwamba Wazanzibar hawako tayari kwa kipindi chote cha miaka 50 ndani ya muungano wa serikali mbili kwenda kwenye serikali moja, maana yake sasa ni kwamba, muundo wa muungano wa serikali mbili unakosa maana na uhalali wake. Hivyo basi muungano wa serikali tatu haukwepeki. Kama kweli tuna imani katika kuungana basi tukutane kwenye serikali moja ya shilikisho la Afrika Masharki.
 
Nataka serikali moja ya JMT.Kama kuna watu wanaogopa kumezwa waamue tu kujitoka katika muungano.Hatuwezi kubembeleza wazanzibar eti tu kwamba hawataki kumezwa!Hii ni sababu ya kitoto kabisa,mbona wamasai hawajamezwa bali kutokana na utamaduni wao wanazidi kung'ara tu!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
ningesema Moja ila kwa mazingira ya sasa tatu (3) ndio yenye kuleta mantiki. hasara za kubaki kwenye 2 au kwenda moja zinanishawishi zaidi: huu ndio mwanzo wa nguvu ya Watanganyika kutaka Tanganyika yao irudi na Zanzibar haiwezi kubadili katiba yake tena kurudi kwenye mfumo wa miaka ya 60 na 70.
 
Kinadharia ningependelea serikali moja, ila kutokana na hali halisi iliyopo sasa hivi, serikali tatu ndio suluhusho na hiyo inawezekana kutekelezeka.

:clap2::clap2::clap2:
 
Pleae wakati unacomment hapa ni vyema ukaVote pale juu ili tuweze kuangal;ia Watanzania Wengi wanataka Muundo upi wa Selikali ambao utatatua kero za Muungano wetu
 
SERIKALI MOJA-wazanzibari kama hawataki, tugawane mbao tu.
ila mbili sitaki hata kuzisikia,bora 3 kwani naitaka TANGANYIKA yangu.
 
Habari ya muda huu wana jukwaa!
Hili ni swali ambalo najiuliza kama wananchi walio wengi wangesema wanataka serikali2 na wachache3 hali ingekuaje kwa wapinzani,hii ni kutokana na kasoro mbalimbali ambazo walio wengi bungeni uzitoa kama vile
=>kati ya maoni zaidi ya laki3 maoni laki1 tu ndio yaliyochambuliwa
=>kutupiliwa mbali kwa maoni ya mabalaza ya kata n.k
kwa kasoro hizo chache pamoja na nyingine je,UKAWA wangetoka kwa madai kwamba takwimu haziko sahihi?
 
Wangetoka tu kwani wao kazi yao ni kupinga kila kitu kinachowasilishwa na serikali.
Kwani wewe umesahau MBOWE alivyopinga kupewa gali la kiongozi wa upinzani bungeni, kwa mbwembwe na bashasha, BAADA YA SIKU CHAKE AKAENDA KULICHUKUWA KIMYA KIMYA NA MPAKA SASA ANALO?
Hiyo ndiyo kazi ya upinzani.WANGETOKA .
 
Serikali moja tu, gari gani lenye madereva wawili. Acheni mbwembwe.
 
Serikali tatu ndio chaguo langu na sababu ni;
1.Tutautendea haki muungano wetu kwa kuweka wazi washirika wa muungano yaani Tanganyika na Zanzibar.
2.Tutapunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya kero mbalimbali ambapo kila k mshirika atashughulika na mambo yake.
3.Mambo muhimu yanayohusu ushrkiano wa nchi zilizoungana yatashughulikiwa na serikali ya shirikisho kwa usawa pasi na upendeleo kama ilivyo sasa katika mfumo usio eleweka wa serikali mbili ambao kimsingi ni wa viongozi tu na si wa wananchi.
 
Back
Top Bottom