dikteta2020
JF-Expert Member
- Aug 14, 2018
- 595
- 3,991
Yani kuacha Magufuli na Lissu, unakuja kugundua kuwa mshindi aliyeshika nafasi ya tatu kati ya hao 15 ni kura zilizo haribika. Yani zaidi ya kura laki mbili ziliharibika. Ni kura nyingi kuliko za mgombea Ibrahim Lipumba ambaye alizunguka nchi nzima kuomba kura.
Ni kura nyingi kuliko kura za wagombea watano watano ukiweka kimafungu kuanzia aliyeshika nafasi ya tatu hadi mwisho.
Kwa maana nyingine, wapo watanzania zaidi ya laki mbili walienda kupiga kura huku wakiwa hawajui cha kufanya. Hii ni idadi ya juu sana. NEC walitoa elimu gani kwa mpiga kura?
Wapo watanzania waliojiandikisha kupiga kura ambao ni kaki mbili na ushee huku wakiwa na kiwango kikubwa cha ujinga vichwani mwao.
Haiingii akilini eti mshindi wa tatu kwenye uchaguzi mkuu anapitwa tena kwa mbali sana na idadi ya kura zilizoharibika (Ukizidisha kura za mshindi wa tatu mara tatu bado hukuti idadi ya kura zilizoharibika). Aisee sisi watanzania wengi wetu ni wajinga wa kiwango cha mwisho kwa idadi hii ya kura zilizoharibika.