Sisi sote tunaoishi wakati wa sheria ya Kristo; Kristo Yesu ametufundisha jinsi mambo yalivyo na yanavyotakiwa kuwa. Ametufundisha vilevile tunavyotakiwa kutenda na kuwatendea ndugu zetu. Kwa sababu hii, Kanisa ni kwa ajili ya watu wote: wenye dhambi na wasio na dhambi.
Kwetu sisi, ambao bado tupo duniani, Kanisa ni mahali pa kujitakasa au kuongoka. Ni mahali pa kujifunza ili kubadilika tabia kuwa watu wema, watakatifu - mpango wa Mungu.
Kristo hakuweka Kanisa ili liwe kwa ajili ya watu wema, wasio na dhambi. Kwa kweli lengo la Kanisa ni kuongoa na kutakasa. Kwa hiyo ni kwa ajili ya watu wote.
Kristo aliwaagiza aliowaachia mamlaka kuwafundishe watu wote duniani. Hii maana yake Kanisa linawakaribisha na ni kwa ajili ya watu wote na hali zao zote.
Kanisa kwa lenyewe halitendi dhambi, ni takatifu. Watu ndio wanaotenda dhambi. Mungu kupitia Mwanae wa pekee Yesu Kristo anawaalika watu wote na kipee kabisa wadhambi. Mungu mwenyewe anasema, katika biblia kwamba, "hakuja dunia kwa ajili ya watu wema bali wakosefu. Anaendelea anasema, wenye afya hawahitaji daktari ila wagonjwa".
Tunaweza kutokukubaliana kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na elimu ya vitu na uelewa wa mambo.
Kanisa kwa kuwapokea wadhambi halihalalishi uovu. Yesu aliwaeleza wayahudi wa nyakati zake waliotaka kumpiga mawe na kumwua mwanamke mzinzi; "asiye na dhambi na awe kwanza kurusha jiwe juu mwanamke huyu".