Kurudisha kodi ya kichwa nyakati hizi za ulimwengu ulioendelea ni aibu kubwa. Mwigulu Nchemba kuwa na aibu. Mbona kuna vyanzo mbadala vingi



Unaweza kuainisha maeneo ambayo yanaweza kuwa vyanzo mbadala ya kodi? Kodi inahitajika sana maana maendeleo yetu na matumizi ya bunge na serikali, yanategemea ukusanyaji kodi.
Tuone aibu kama mpaka leo 40% ya budget inachangiwa na wahisani
 
Uvccm si mkalinde hizo meli zisiibe, au kazi yenu ni kukimbia na mabox ya kura tu?
Ahaaaaa, where have you been young brother tindo? Ahaaaa. Habari za kura zinaingia wapi hapa? Tunatakiwa tukusanye mapato kwa manufaa ya umma kuliko kuwa na kodi zisizo na tija.
 
Hii kodi safi sana!! Ni njia pekee ya kuhakikisha kuwa kila mtanzania analipa kodi!
 
Kwahyo ikitozwa kodi, hakutakuwa na makosa ya kujipatia kipato kwa njia ya udanganyifu??
 
Itakuwa vizuri mishahara yao hao wabunge nayo ikatwe kodi, wachangie BIMA ya afya, pia wachangie kiinua mgongo maana wanahubiri uzalendo lakini hakuna wanachochangia kutoka kwenye mishahara yao japo wanalipwa mamilioni, na bado nyumba bure, bima bure, kiinua mgongo wanapewa bure japo hawachangii, na mafta ya gari bure, yani kila kitu bure
 
Sasa weye hicho kichwa chako kina faida gani kwa ujinga huo ulioandika?Unatakiwa ulipishwe mara mbili zaidi!
 
Hivi ni lazima kila raia alipe kodi? Nini maana ya kuwa na vyanzo vya kodi vyenye nguvu?

Kodi ya voucher ni rahisi kukusanya lakini haina udugu. Maana hata bibi asiye na uwezo akiweka vocha anatozwa kodi.
Kila raia ni lazima alipe kodi. Kiprinciple inabidi iwe hivyo. Haujaja duniani ili uishi kwa jasho la wengine. Sasa linapokuja kiutekelezaji wote tunaelewa siyo kila mtu anaweza kulipa kodi: kwa mfano kodi kwa watoto itabebwa na wazazi wao, kodi kwa wazee na wasiojiweza inaweza kuwa compensated kutoka vyanzo vingine vya mapato.

Lakini serikali haikufuta kodi ya kichwa ili huo mzigo uwaelemee watu wachache sana -- wafanyabiashara na wafanyakazi tena sekta rasmi. Kufikiri nje ya box katika kuhakikisha kila mtu (anayestahili kulipa kodi) amelipa kodi inatakiwa sana, na kama kuja na kodi za voucher za simu ni moja ya fikra hizo basi nakubaliana nalo.
 

Mapato ya ubunge kwa ujumla pamoja na marupurupu ni kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi kwa mbunge. Hiki ni chanzo kingine cha kuongezea makusanyo ya uzalendo kuchangia kodi.
"Mshahara wa mbunge ni milioni 3.8 kwa mwezi, Posho ya Ubunge ni milioni 8 kwa mwezi, Posho ya
 
Direct taxes anazolipa mtumiaji wa Simu Tanzania:
1. VAT
2. Excise Duty
3. Kodi ya hilo chotora la Ilala
 
Kwani ni kipi bora kodi ya kichwa ama kodi ya kupora..
 
15 Juni 2021

Prof. Lipumba nchi haina uwezo wa kukusanya fedha za ndani kutosha kugharamia bajeti ya MAENDELEO YA 2021 / 2022


Prof. Lipumba ampa ushauri mzito Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa bajeti ya 2021 / 2022 hakuna uhalisia wa kuweza kukusanya kodi kugharamia miradi mikubwa iliyopo.

Sovereign credit rating ya Tanzania inazidi kuporomoka, riba ya kulipia mikopo ya kibiashara kupanda kutokana na kushindwa kulipa madeni kwa wakati, ukuaji wa Money supply / ujazo wa fedha umepungua katika ya mwaka 2016 - 2020, mikopo kwenye sekta binafsi imepungua sana huku riba imeongezeka marudufu na kupelekea biashara kuyumba na maana yake makusanyo ya kodi kupungua.

Mtu binafsi mwananchi kufungua akaunti ya akiba benki analipwa riba ndogo ya 2.3%, mtu binafsi akienda kukopa benki kama atapata bahati ya kukubaliwa atatozwa riba asilimia 20% .....

Hali siyo nzuri.. kodi za majengo haziwezi kuwa za serikali kuu kama waziri Dr. Mwigulu Nchemba alivyotangaza ktk bajeti ya 2021 / 2022 ilitakiwa zikusanywe na Halmashauri za wilaya ili zitumike huko wilayani.

Prof. Lipumba anatizama lengo la serikali kuongeza Tozo za miamala kuwa karata ya turufu ya kuongeza mapato makubwa ya serikali, ni sawa na serikali kuzuia ukuaji wa kiuchumi wa kidijitali hivyo serikali imepotoka.

Source : ICON TV TZ
 
11 March 2021

Mh. Philip Mpango : Bajeti ya 2021 / 2022 inaweka wazi Misingi Jumla na kufafanuliwa , kupanua wigo wa walipa kodi, serikali yataka kuelewa kwanini wafanyabishara wadogo hawataki kulipa Kodi, sababu za Masharti magumu ya mikopo kwa serikali, kulipa deni la serikali, gharama za uendeshaji serikali, uchaguzi mkuu 2020 ulioendeshwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia fedha za ndani, kuleta nidhamu ktk matumizi ya serikali ....


 
20 Juni 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Ukosefu wa Fedha na Ubadhirifu Manispaa ya Kinondoni wakwamisha miradi 3 mikubwa Dar es Salaam

Miradi mitatu Kinondoni ya Makao Makuu ya Manispaa Kinondoni, Uwanja wa Michezo Mwenge, Kituo cha Mabasi Mwenge
Source: ITV Tanzania
 
Hivi ni lazima kila raia alipe kodi? Nini maana ya kuwa na vyanzo vya kodi vyenye nguvu?

Kodi ya voucher ni rahisi kukusanya lakini haina udugu. Maana hata bibi asiye na uwezo akiweka vocha anatozwa kodi.
Atatozwa kodi lakini atapata huduma nzuri za kijamii alafu mtu asiye na uwezo hata matumizi yake ya voucher yanakuwa ya nadira hivyo haitamuumiza huku na yeye anafanikisha kupata huduma nzuri, kama kusogezewa maji, umeme, barabara, shule kwa watoto na wajukuu na hospital karibu, inatakiwa huyo Bibi au babu asiwe mbinafsi kuacha kuandaa kizazi atakachokiacha kuishi kwenye jamii yenye mahitaji muhimu.
 
Hivyo vitatumika kuongeza ufanisi kwenye vile tutavyojenga kama kuongeza umeme, madaraja, shule nzuri, hospital nzuri, stendi nzuri na vitu vingine vizuri.
 
22 Jun 2021

Bunge lapitisha Bajeti ya Serikali 2021/2022 kwa 'kishindo'

Bunge limepitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 ambapo wabunge 361 sawa na asilimia 94 wamekubali huku wabunge 23 sawa na asilimia 6 hawakuamua

Source : mwananchi digital
 
22 Juni 2021
Dodoma, Tanzania

Bunge lapitisha Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2021 / 2022 Shs.36,681,897,765,000​


Bunge limepitisha Bajeti Kuu ya Serikali ya shilingi trilioni 36.68 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo Wabunge 361 sawa na asilimia 94 wamepiga kura ya ndio.

Akitangaza matokeo ya upigaji wa kura mara baada ya mjadala wa Bajeti ya Serikali uliofanyika kwa takribani wiki moja Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai amesema kuwa Wabunge waliopiga kura ni 385 ambapo waliopiga kura ya Ndio ni 361 sawa na asilimia 94, waliopiga kura isiyo ya maamuzi (hawajakataa wala kukubali) ni 23 sawa na asilimia 6 na Wabunge watano (5) hawakuwepo wakati wa zoezi hilo la upigaji kura.

Aidha, mara baada ya upigaji huo wa kura Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya kuidhinisha Matumizi ya Serikali wa mwaka 2021 (The Appropriation Bill, 2021) wenye dhumuni la kuidhinisha Matumizi ya jumla ya Shilingi 36,681,897,765,000.

Mara baada ya kupitisha Bajeti zote za Wizara pamoja na Bajeti kuu ya Serikali, Mkutano wa Tatu wa Bunge unatarajia kuendelea na ukamilishaji wa shughuli zilizobaki za Kiserikali na Kamati kabla ya kuahirishwa Juni 30 2021 . Source : Parliament of Tanzania
 
Mkuu Vessel kulalamika ni sifa ambayo sisi watanzania tuna haki ya kuiandika ndani ya CV zetu tukiwa tunaomba kazi, yaani ni sifa ya asili tuliyonayo.

Hizo foleni za kulipa shilingi elfu kumi zimeikosesha serikali pesa nyingi kwani wengi hawapendi hiyo kero ya kusimama siku nzima nje ya dirisha halafu shughuli nyinginezo ziwe zinakwama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…