Kurudisha mabinti waliopata mimba shuleni ni kunyoosha mikono juu na kulikabidhi taifa letu kwa wakoloni mambo leo kwa ajili ya mkopo wa bil 600

Kurudisha mabinti waliopata mimba shuleni ni kunyoosha mikono juu na kulikabidhi taifa letu kwa wakoloni mambo leo kwa ajili ya mkopo wa bil 600

Fikiria jamii ambayo ni halali kuoa binti mwenye miaka 13 lakini inashangaa wa miaka 14 kupata mimba.
Fikiria jamii ambayo inaamini mimba zote ni kutokana na uhuni wa mabinti zao.
Fikiria jamii ambayo inaamini kuwa mimba inaambukizwa.
Fikiria jamii ambayo haitaki kuwapa watoto wake elimu ya miili ( ambayo mabibi na mababu zao walikuwa wakiitoa) halafu wanashangaa wanapopata mimba.
Fikiria jamii yenye tatizo kubwa la mimba za utotoni ( sio kwa wanafunzi peke yao) lakini haitaki kuwapa contraceptives.
Fikiria jamii inayoamini watoto wote wanaofukuzwa shule ni wavuta bangi na wanastahili kufukuzwa.
Fikiria jamii inayoona heri kukosa mkopo utaowasaidia kujenga shule kwa ajili ya watoto kuliko kuruhusu binti aliyepata uja uzito kuendelea na masomo.
Baada ya kufikiria hivyo jiulize tena kwa nini nchi hiyo bado ina umasikini wa kutupwa miaka 60 baada ya kupata uhuru kutoka kwa mabeberu.

Amandla...
Unaangalia shilingi upande mmoja
 
Kwa hiyo ulitaka mabinti wasipate elimu? Ukimsomesha mwanamke umekomboa taifa

Mjadala ni mzito na unahusu wanafunzi wa kike waliopata mimba kurejea shuleni baada ya kujifungua. Bujibuji Simba Nyanaume umehitimisha kwa kaulimbiu inayotumika kutetea haja hiyo.

Lakini maswali ya msingi hayajadiliwi. Baadhi yao ni:
1) Aliyempatia mimba hatima yake ni ipi? Kifungo kwa mtu mzima akaacha familia inateseka ikiwa ni pamoja na binti zake ambao wako shule. Au kama ni mwanafunzi mwenzake aendelee na masomo?

2) Je, uhusika wa wazazi/walezi wa binti aliyepata mimba?

3) Vipi walimu ambao wanafunzi wao wa kike wanapata uja uzito wakati wao ndio wanakuwa nao muda mrefu na walezi mbadala?

4) Wizara ya Afya imeandaa mazingira rafiki ya kuhudumia wazazi-watoto, ambao kimsingi hawajawa tayari kubeba mimba na kuwa wazazi?
 
Hivi kuna elimu siku hizi au kuna historia ya watu wa Ulaya na vumbuzi zao za miaka ile ya zama damu? Yaani huu u-Mang'ungo wa Msovero, unaendelea hapa nchini unaweza kutamani mwanao aka changanywe na hao ' mtaji wa kisiasa'?

Kaa na mwanao nyumbani umfundishe kusoma na kuandika, kisha mfunze kujihami kisaikologia, mengine yote kazaliwa nayo ya kuushangaza ulimwengu, kaa kando utazame mienendo yake kila siku mpaka atakapoanza kujitegemea kwa kuitumikisha akili yake.
 
Maadili gani wewe kilaza, hapo ulipo una vimechepuko kibao unakuja kutupigia kelele za maadili hapa.To hell na maadili yako.
#ArudiShule
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa...
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shul...
Kwani wanaorudishwa shuleni ni wakoloni au watoto wetu wenyewe?

Waafrika tunaongoza kwa roho mbaya,yaani hadi mzungu anatufundisha kuwa na upendo kwa watoto wetu!

Mngekuwa na hayo maadili msingekuwa na nyumba ndogo,hopeless kabisa na unafiki wa kuzuia mbu na kuruhusu ngamia!

Sasa naelewa kwa nini shetani anachorwa kwa rangi nyeusi!
 
We Kada binti muhuni asiye na maadili Katu hawezi dungwa mimba.
Mbona vyuoni wanasoma wazazi na Wana wajukuu kabisa,elimu ni haki ya wote
Sasa kwanini wanaowapa mimba wanafungwa miaka 30? Wangefungwa binti akijifungua anatolewa jela akalee mtoto ili binti arudi shule.
 
Kulea watoto wa kwa maadili mema ni jukumu la jamii yote na si kuwafukuza shule.

Jamii nyingine kupata mimba ukiwa kwa wazazi ni taboo, ni laana. Tuwalee watoto wajue hivyo, tuwalinde. Mimba haziishi kwa kuwafukuza shule bali wao kujitambua. Huo ndio wajibu wetu.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kwanini wanaowapa mimba wanafungwa miaka 30? Wangefungwa binti akijifungua anatolewa jela akalee mtoto ili binti arudi shule.
Lengo ni kupunguza rate ya ufataki,isipofanywa hivyo watu awatoogopa kuwamimba wanafunzi.

Japo kumfunga baba kisa kampa mimba mama pia ni ukatili kwa mtoto atakezaliwa maana atauliza mama baba yupo wapi yupo jela kwa kosa gani alinipa mimba Ili uzaliwe wewe mtoto atauliza Ina maana baba kunizaa ni kosa?

Hili jambo linataka mjadala
 
Maadili gani wewe kilaza, hapo ulipo una vimechepuko kibao unakuja kutupigia kelele za maadili hapa.To hell na maadili yako.
#ArudiShule
Lack of sense=stupidity
 
Kuna binti jirani yetu,alikuwa na ki boyfriend chake enzi hizo mi wakusoma, ikawa tukikutana ananisimulia jinsi alivyokuwa anasikia raha yule boy akimkumbatia,akimbusu, akimpiga matouch[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]

Sasa na mimi nikawa natamani, lakini kila nikitongozwa nakumbuka kuna mimba,na shule yetu ukipata mimba unafukuzwa kwa fedheha hapo hapo genye zote zinakata[emoji2][emoji2][emoji2][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]

Shule niliyosoma tulikuwa tunapimwa mimba kila baada ya miezi 3,ilitusaidia kwa kiasi kikubwa kujilinda na ngono zembe!!!
 
Na hii nchi imejaa watu wengi zaidi wenye akili kama za hili dude Idugunde ndio maana hata maendeleo yanakuja kwa mwendo wa Kinyonga.
Kwani wanaorudishwa shuleni ni wakoloni au watoto wetu wenyewe?

Waafrika tunaongoza kwa roho mbaya,yaani hadi mzungu anatufundisha kuwa na upendo kwa watoto wetu!

Mngekuwa na hayo maadili msingekuwa na nyumba ndogo,hopeless kabisa na unafiki wa kuzuia mbu na kuruhusu ngamia!

Sasa naelewa kwa nini shetani anachorwa kwa rangi nyeusi!
 
Fikiria binti asiyekuwa na maadili na alipata malezi mabaya akaanza uhuni akiwa na miaka kumi na nne akapata mimba akiwa la sita. Alafu akajifungua kisha akirudi shule akawa anasoma na mabinti ambao hawajawahi kubikiriwa, hatakuwa na ushawishi mbovu kwao ili waonje utamu wa ngono? Tumejustify mapenzi kabla ya kumaliza shule

Fikiria kijana mvuta bangi ambae alikosa malezi na akaacha shule alafu ukrudisha asome kisa tu unalazisha amalize shule. Hii sio justification kuwa kuvuta bangi na utoro sio kosa?

Mkopo wa bil 600 umetufanya tujikabidhi kwa wakoloni mambo leo. Hivi kwa rasilimali tulizonazo ndio tumelainika kwa wakoloni namna hii?
Umeichukulia issue Kwa mtazamo finyu sana aisee

Umelelewa na familia ya aina gani isiyothamini utu wa mtu na kulinda watoto?
 
Back
Top Bottom