Kurudishwa kwa January Makamba ni dalili tosha kwamba Rais Samia ameanza kuliogopa kundi linalompinga ndani ya CCM!

MIMI NINACHOTAMANI KUJUA NI KITU GANI KIJANA ALIMKOSEA MAMA YAKE?MANA MAMA AMEKIRI KIJANA ALIKOSA NA KUMTENGUA NI KAMA ADHABU NA SASA AMEMSAMEHE."KOSA LA JANUARY NI LIPI?"
 
CCM ni bahari ya siasa na mwenyekiti wake ni mh.Rais Samia....yeye hamuogopi yeyote....hana wa kumhofia punje ukucha....

Mwenyekiti ana hekima na BUSARA kwa kuwa yeye ni MFARIJI mkuu na wote ni wake.....

#Nguvu ya mwenyekiti Samia ni kubwa mno !
 
Sawa Oktoba Rais ni Samia
 
Kwani amepewa wizara gani?
 
CCM kipindi hiki ina mgombea dhaifu na asiyekubalika kuliko kipindi kingine chochote tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe.
 
tatizo wabongo mnahadaika sana na maneno ya jukwaani..nyie mlitegemea samia aongee nini mbele ya umati wa watu zaidi ya alivyoongea..wanasiasa ni kawaida kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa ila sisi hatuwezi kujua yaliyo nyuma ya pazia baina yao kwani kuongea sio kutenda.
 
CCM ni bahari ya siasa na mwenyekiti wake ni mh.Rais Samia....yeye hamuogopi yeyote....hana wa kumhofia punje ukucha....

Mwenyekiti ana hekima na BUSARA kwa kuwa yeye ni MFARIJI mkuu na wote ni wake.....

#Nguvu ya mwenyekiti Samia ni kubwa mno !
Hamna kitu pale. Walioko ndani ya CCM wakiamua kutumia tu gia ya Uzanzibar wanamuondoa. Samia yuko very vulnerable
 
Kwani amepewa wizara gani?
Bado,itakuwa negotiation zinaendelea. Na hizi huwa ni negotiation hata baba yake anashiriki, kama alivyoshinikiza apewe wizara ya nishati.

Ila kitu kimoja, ni kwamba January anakubali kurudi kwa mama kwa matarajio kwamba mama atamtengenezea njia ya 2030. Hapo ndipo atakaposhangaa!
 
Hatukutegemea kitu tofauti, na alijua wazi lazima aongee kitu ambacho umati ule wa Bumbuli ungefurahia kwa sababu kinamfurahisha mbunge wao. Bila kuongea vile Samia angeweza hata kuzomewa na wananchi wa Bumbuli kwa kile ambacho wangeona amemfanyia mbunge wao. Ndio maana nikamwambia, aliyeshinda hapa sio January, ni Samia. Kishajihakikishia kura za Bumbuli na kumtoa January katika kundi la wapinzani wake wa ndani ya CCM
 
MIMI NINACHOTAMANI KUJUA NI KITU GANI KIJANA ALIMKOSEA MAMA YAKE?MANA MAMA AMEKIRI KIJANA ALIKOSA NA KUMTENGUA NI KAMA ADHABU NA SASA AMEMSAMEHE."KOSA LA JANUARY NI LIPI?"
Unaambiwa ni kosa ambalo January angekuwa China angehukumiwa kifo! Suala ni kwa nini Samia hataki kulisema? Kwa sababu lingeiaibisha CCM?
 
Si rahisi. Kurudi kwa mama kwa January kunamfanya aanze kutengeneza njia mbadala ya kumfikisha kwenye mbio za uraisi za 2020, badala ya ile ya kumtoa Samia. Sasa tatizo ni kwamba, Mwigulu nae anajiona ndio anaestahili 2030. January anaona yeye ndie anaefaa. Soon Nchimbi ataona ni haki yake yeye kuwa raisi 2030. Hapo ndio ngoma itakaponoga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…