Kurudishwa kwa January Makamba ni dalili tosha kwamba Rais Samia ameanza kuliogopa kundi linalompinga ndani ya CCM!

Ukiambiwa njoo.mkesha kwa.mwamposa umiliki.na KUTAWALA unaogopa sadaka kazi kwakooooo

Wenziooo wanatoa sadaka wanatengenezwa misikiti na makanisa...
 
Ninachoona Marope amerudishwa rasmi kwa ajili ya kucheza na tarakimu angani wkt wa majumuisho ya matokeo ya kura za uchafuzi wa mpangaji wa jumba jeupe.
 
Kwa hiyo tutarajie mkeka muda wowote kuanzia sasa Makamba arudishiwe chakula. Kumbe utumishi wa umma siku hizi za utawala wa Samia ni ulaji.
 
Unaongea kwa kujiamini sababu unajua chama kinabebwa na dola(policcm)
Bila hao hamtoboi ndo maana ni muhimu kubadili katiba ya nchi!
 
Makamba alijikweza katika utatuzi wa suala la sekta ya anga akafanya kikao cha pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Kenya wakati utatuzi ulitakiwa uwajumuishe wakurugenzi wa mamlaka za anga wa nchi hizi mbili.

Samia hakupendezwa na hulka hiyo ya Makamba na akaamua kumtoa baada ya kumgundua tabia yake ya kujikweza kuliko wenye mamlaka akidhani kwamba yeye anayo hadhi sawa na rais anayekuwepo ikulu.

Samia kaamua kumrudisha kundini katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025 akitegemea kuutumia uwezo wake katika siasa za ushindani na labda baada ya uchaguzi kumalizika aje ampe nafasi nyingine serikalini.

Makamba anao udhaifu wa kupenda kujitutumua na kuwageuka viongozi wake wakubwa, kwa ufupi anajiona mtoto wa mjini kupita maelezo na anapenda kuwazunguka wanaompa nafasi serikalini.
 
Achana na sharubu watu wavuruga hadi ushuzi wa simba hadi MAVOOZI kaa utulie
 
Kama ni hilo mbona dogo sana, la kumuonya tu. Halikua na haja ya Samia ku-create enemies katika January na baba yake kwa ajili ya hili, huko ni kukosa busara.

Na pia, Makamba ataendaje kujadili issue za sekta ya anga wakati background yake ni lugha sijui, Kiingereza na Kiswahili ambavyo ndio vilipeleka Ikulu maka mwandishi wa speech za Kikwete? Ndio haya mambo tunasema wanasiasa wa Tanzania wanapeleka maoni yao ya kisiasa kwenye mikutano inayohusu ufahamu wa tekinolojia
 
Waliokuwa na vyeo wakati wa awamu ya kwanza hivi sasa wanashinda majumbani wakicheza na wajukuu, wamezeeka. Hawa machawa ni vijana waliozaliwa baadae wanajifunza uchawa kwa kuukuta huo mfumo wa zidumu pengine kwa kuusoma mahali fulani na kupitia tabia ya kupenda kuabudiwa, wanayoipenda wanasiasa wenye dhamana za uongozi.
 
January makamba kuwa rais ni jambo ambalo lipo damuni kwake ni suala la umri na muda tu ila one day yes mwamba anajitahdi sana sometimes ni mifumo tu inamuangusha.
 
Alidhani ataonekana anafanya kazi kubwa kwa Rais wake, akasahau ni masuala ya mamlaka ya anga TCAA yenye watendaji wanaoaminiwa na marais. Samia alimpigia simu mkurugenzi akiwa amekasirishwa na hicho kitendo.

Baada ya siku chache akamuondoa pale mambo ya nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…