Kuruhusu watu binafsi kuzalisha na kuuza umeme inaweza kuwa suluhisho la tatizo la umeme?

Yaani itakuwa suluhisho la maana sana. Yaani kama simu tu..!! Zamani authority ya kumiliki huduma ya mawasiliano ilikuwa kwa TTCL peke yao (kama ilivyo sasa kwa umeme, bandari, TRA etc). Walipoondoa authority hiyo toka kwa TTCl, wengine wakaingia na ndo unafuu tunaoupata hadi leo. Fikiria, hapo ulipo una LINE mbili au zaidi za simu, opereta huyu akizingua ni kwamba wewe bado unapatika kupitia opereta mwingine. Fikiria hapo home kwako au ofisini una meter mbili au zaidi za umeme huku kila moja ina laini yake ya umeme, huyu akikata, Automatic Transfer Switch (ATS) inakuhamishia kwenye line yenye umeme bila hata umeme kukatika ndani kwako. Utakosa umeme pale tu line zote zinapokosa umeme
 
So wanataka uwauzie wao
Vyote hawataki kwasabu kuna makampuni yao wanawauzi Tanesco umeme unit moja bei kubwa zaidi ya bei ya Tanesco wanauzia wananchi tatizo linaanzia hapo,ndio maana kwenye ripot ya CAG Tanesco kila ukaguzi bila kupewa ruzuku na serekali ningumu kutoa huduma.
Nfano Tanesco Luku wanauza 80k bila gharama za ngunzo hii kazi ya kuuza Luku tu nikipewa nitauza Luku moja elfu 30,prepaid separate meters nitauza elfu 10k wao wako pale kuongeza matatizo kwa wananchi.
 
Adui wa mtu mweusi ni mtu mweusi.
 
True hata nguzo moja wanatuuzia laki tatu unusu wakati mkulima anauza nguzo moja kwa sh elf kumi njombe
 
Ni uingereza
 
Hiyo inafanyika katika maeneo mengi hapa nchini, zipo taasisi zinazalisha umeme kidogo kama 5MW lakini wanawauzia tanesco, Njombe kama sikosei.
Hii nikweli tanesco wananunua kwenye vyanzo binafsi, ikumbukwe IPTL pia walizalisha ikaizia tanesco
 
Uko sahihi sana mkuu.

Nje ya mada, huenda umenunua simu mpya, maana naona spelling error kibao!
 
Suluhu kubwa sana hiyo!
Nchi nyingine hata wamiliki wenye nyumba zenye solar systems wanaozalisha umeme wa ziada wanauza umeme kwenye national grid au kwa majirani zao!
Ni masuala ya mikataba tu. Yakiwekwa vizuri umeme upo mwingi sana!
Na kuuza umeme wa ziada ni biashara inayoingiza fedha bila stress!
 
Kwamba na wao watapitisha waya zao kwenye nguzo zao?
Ndiyo ikibidi kufanya hivyo!
Lakini fursa zipo nyingi!
Mfano: wewe unaweza kuwekeza kwenye Solar panels... ukazalisha umeme wa ziada ambao ukawauzia Tanesco (1. yaani wewe na Tanesco mkamalizana vizuri kwenye LUKU au 2. wakakulipa kwa units) au ukawasambazia majirani zako.
Fursa zipo nyingi sana kwenye biashara ya umeme!

Sijui ni lini TZ wataona kuwa umeme siyo anasa!
Piga picha kama tungekuwa tunaitegemea TTCL peke yake kwenye mawasiliano ya simu!
 
Pamoja na uwakili wako wa shetani, asante sana kwa andiko ha hoja nzuri. Mitizamo kama hii ni muhimu kwa maendelea ya taifa letu. Teknolojia hii ya kuzalisha umeme binafsi na kuingiza kwenye gridi imetumika ktk mataifa yaliyoendelea, mfano Ubelgiji. Huu ni utatuzi mkubwa sana kufidia kuliwango kinachopungua kwenye gridi. Tunapaswa kuwa na sera ya uzalishaji, kuuza na kununua umeme. Serikali inawekeza kwenye tejnolojia ikihusisha vifaa ambavyo watu wataweza kuvinunua ili kuweza kuunganisha umeme wao na ule wa gridi.
Tunaweza kukubaliana kisera kuwa unit moja kutoka Tanesco ni Tsh 300, nami nikizalisha ziada itakwenda kwa Tanesco kwa Ths 150. Maana yake nini nini? Wengi tunazalisha umeme mchana, muda tusioutumia kwa kutumia sola. Umeme huu ungetumika sana viwandani wanakouhitaji. Usiku tunapokuwa na mahitaji makubwa majumbani, tanesco inatoa umeme wake kufidia upungufu.
 
Umenikumbusha usafiri wetu wa UDA = Usafiri Dar es salaam ,
Mpaka mabasi ya ghorofa yalikuwepo πŸ™πŸ™
Miaka inaenda mbio sana. !
 
Serikali kuruhusu watu binafsi kuzalisha na kuuza umeme
shida siyo uzalishaji, shida ni usambazaji
kimsingi demand ya umeme Tz ni ndogo kuliko supply
shida ni miundombinu ya usambazaji

imagine, ikishenya mvua, tayari ushakatika
kukiwa na upepo tayari ushakatika
mara transfoma ndogo, inakata kata fuse kila mda
mara mti limedondokea nyaya, mara nyoka kashotisha nyaya
mara nguzo kuoza na kadhia tele
 
Nchi hii ina kila aina ya resource inayohitajika kuzalisha umeme , Jua, maji, upepo, makaa ya mawe, uranium, gesi and many other things !!

Utashi ndio sifuri ! Watu wanataka quick money πŸ’° !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…