Kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge au Kamati za Bunge zikiwa kazini hakufai

Kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Vikao vya Bunge au Kamati za Bunge zikiwa kazini hakufai

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Mtu ukiwa unalima shamba huhitaji press. Vikao vya Kamati za Bunge na vikao vya Bunge ni vikao serious vya kikazi. Wananchi wanachohitaji kujua ni matokeo ya kile walichojadili sio zile porojo za sijui mbunge huyu akachekesha, huyu akatukana. Wananchi wanachohitaji ni final result za kikao.

Ukiweka live Wabunge wengi wanageuza vikao vya Bunge au Kamati za Bunge kuwa sehemu ya kuuza sura kwenye vyombo vya habari badala ku-concentrate kwenye kazi.

Nakumbuka kuna Mbunge mmoja alishawahi mkunja mtangazaji wa radio ya Kenya, KBC, akifoka kwa Kiingereza kibovu akisema ''You KBC why not announce my voice?'' Alimaanisha kwa nini huwa hawamtoi hewani akiongea bungeni.

Wabunge wetu kuwa serious na kazi za bunge hawahitaji kuwa live. Utafiti niliofanya binafsi nimegundua wachangiaji bungeni wamepungua toka bunge lilipoacha kuonyeshwa live. Lilipokuwa liko live spika alikuwa na kazi ya ziada ya kuamua ampe nafasi nani aongee kila mbunge alikuwa anataka kuuza sura hewani na asikike hewani.

Sasa hivi wachangiaji ni wachache walio serious tu. Wabunge wengi wameingia mitini bunge live lilipoondolewa. Spika kwenye mijadala Hana kazi kubwa.
 
Kwahiyo unafurahi Supika yenu kutokuwa na kazi wakati waliomchagua banategemea afanye kazi ili msgahara na marupumarupu yasiliwe bure
 
Ni maoni yake.

nje ya mada;

Ila nimeangalia Uganda spika anazima mic ya mtoa hoja bila taarifa yeyote na wala hasubiri hata mtoa hoja amalizie point hata sentensi tu wengine wanacheki mic kama inatatizo kumbe spika kaweka off.

Kwa hili Ndugai Oyeee
 
Hapa ndipo huwa napochukia mdudu anaeitwa SIASA.Mtu anasifia jambo kwasababu wakubwa zake wameamua siku wakibadilika tena wakasema BUNGE liwe LIVE utakuja kumsifia kiongozi wako kwa UZALENDO wa kuonesha BUNGE LIVE.Vijana mnaopata lishe kupitia hivi vyama vya SIASA em tumieni akili zetu,Msiruhusu wengine wafikirie kwa niaba yenu ni hatari kwa Taifa na familia zenu.Hili tatizo lipo katika vyama vyote vya siasa na wafuasi wao VIJANA WAMEKABIDHI AKILI KWA VIONGOZI WAO.AIBU SANA KIUKWELI.
 
Vipi kuhusu makinikia live, uteuzi live, kuapisha live, hotuba zinazojirudia live, kupokea gawio live, ziara live, uzinduzi live, nk. Huoni na hizo nazo zinatuchosha?

Kila siku unamuangalia na kumsikiliza mtu mmoja tu! Huku akizungumzia mambo yale yale! Mbona na sisi tunachoka sana? Tena hayo ma live yanafanyika muda na saa za kazi! Hivi yana tija yoyote kweli!!!
 
Kitu pekee chafaa kuwekwa siri na kufanyika sirini ni Tukio la wewe unavyolala na mwenzi wako...
Mengine yote hayafai kuwa siri ndo maana hata baada ya mambo yenu ya sirini kuna mmoja ambaye atabaki na ushahidi wa ujauzito... Na hata wakati wa kujifungua bado hakuna siri make kunakuwepo na jopo la wataalamu mbali mbali!

Sasa ukirudi kwa hawa tuliowapa dhamana ya uongozi hasa wabunge... Hawa ndo inabidi tuwazuie kufanya mikutano yao sirini na kwa usiri uliopo sasa!

Hawa wabunge tumewachagua sisi hivyo ni muhimu tujue wanavyooperate vikao vyao na wanavyofikia maamuzi yao!!

Ni haki ya wananchi ambao ndo mabosi wao kujua jinsi wafanyakazi wao wanayowasilisha mawazo yao..!!

Bunge live ilisaidia sana kuwafahamu wawakilishi wetu kwa undani zaidi!

Wasituache gizani; make hawachelewi kufanya yao badala ya yetu!
 
Unajuaje uchache wa wachangiaji wakati huoni kinachoendelea ndani ya bunge?
Ramri zinaweza kuwa bado zina effect kubwa sana katika ulimwengu wa leo.
 
Napingana na wewe ila nayaheshimu mawazo yako
Nalog off
 
Vipi kuhusu makinikia live, uteuzi live, kuapisha live, hotuba zinazojirudia live, kupokea gawio live, ziara live, uzinduzi live, nk. Huoni na hizo nazo zinatuchosha?

Kila siku unamuangalia na kumsikiliza mtu mmoja tu! Huku akizungumzia mambo yale yale! Mbona na sisi tunachoka sana? Tena hayo ma live yanafanyika muda na saa za kazi! Hivi yana tija yoyote kweli!!!
Hii ni tofauti kabisa kwa sababu inakuwa ni baada ya kazi. ni events baada ya maamuz ( yaan ni matikeo ya kazi) ni sawa na wewe uwe ofisini kila kitu unachofanya kiwe live badala tupate mrejesho wa kaz mwisho wa siku (report)
 
Bashe hakuwa kuwa Mbunge wakati wa bunge "live kama lote"
Amekuwa Bungeni wakati huu "wamejifungia" na bado mrejesho wa michango yake na analysis zake tuliziona.

Wale wanaotaka kuwa live 24/7 mbona hata wakiwa "kizani" hatusikii wakikata issues?

Enzi za G55 ya akina Philip Marmo na Njelu Kasaka, mbona walipata mileage na bunge wala halikuwa live.

Kama unakata sensible issues hata ukiwa kizani utasikika tu.

Ila kama hamnamo kichwani basi ndo hivyo tena. Ni bahati tu imewaangukiwa baadhi kuwa waheshimiwa, however, some do not deserve.
 
Mtu ukiwa unalima shamba huhitaji press. Vikao vya Kamati za Bunge na vikao vya Bunge ni vikao serious vya kikazi. Wananchi wanachohitaji kujua ni matokeo ya kile walichojadili sio zile porojo za sijui mbunge huyu akachekesha, huyu akatukana. Wananchi wanachohitaji ni final result za kikao.

Ukiweka live Wabunge wengi wanageuza vikao vya Bunge au Kamati za Bunge kuwa sehemu ya kuuza sura kwenye vyombo vya habari badala ku-concentrate kwenye kazi.

Nakumbuka kuna Mbunge mmoja alishawahi mkunja mtangazaji wa radio ya Kenya, KBC, akifoka kwa Kiingereza kibovu akisema ''You KBC why not announce my voice?'' Alimaanisha kwa nini huwa hawamtoi hewani akiongea bungeni.

Wabunge wetu kuwa serious na kazi za bunge hawahitaji kuwa live. Utafiti niliofanya binafsi nimegundua wachangiaji bungeni wamepungua toka bunge lilipoacha kuonyeshwa live. Lilipokuwa liko live spika alikuwa na kazi ya ziada ya kuamua ampe nafasi nani aongee kila mbunge alikuwa anataka kuuza sura hewani na asikike hewani.

Sasa hivi wachangiaji ni wachache walio serious tu. Wabunge wengi wameingia mitini bunge live lilipoondolewa. Spika kwenye mijadala Hana kazi kubwa.

Punguani kabisa

Kenya wana move kua USA wewe unarudi kua Soviet Union?

Congressional hearings ziwe closed doors wakati maboss zenu wananchi wapo nje?

Hovyo kabisa!

Na katiba ya Warioba explicitly inataka congressional hearings ziwe broadcasted live!

Mapunguani kabisa!
 
sasa mbona zinduzi mbalimbali na ziara za yule "mshamba wa chato" tunaonyeshwa kila kukicha?
Kuzindua ni sherehe ndio maaana huitwa sherehe ya uzinduzi huwezi linganisha na kikao Cha bunge
 
Mrejesho unaupataje wakati mjadala hauonekani? Kwa njia ya TV habari au magazeti?
Bunge huwa linatoa yaliyofikiwa kwa vyombo vya habari baada ya Vikao vya bunge na kamati
 
Back
Top Bottom